Asili ya neno hela

Asili ya neno hela

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,882
Reaction score
828,452
Hapo Zamani wakati Wagerumani(German East Africa) Walipokuja TANGANYIKA ambayo sasa ni Nchi ya Tanzania Walifanya Biashara Kutumia Sarafu ya HELLER

-1904 Sarafu ya Shaba yaani Bronze Hela 1/2 na Hela 1 ilitengenezwa.

-1908 Hela 5 ya Shaba na Hela iliyo na Tundu Katikati ya madini ya Cupro-Nickel Hela 10 pia iliundwa.
-1913 Hela 5 ya Cupro-Nickel iliyo ya Tundu Katikati pia iliundwa.

-1916 Wakati wa Vita vya Dunia ya Kwanza ya Dharura Sarafu ya Hela zilitengenezwa katika Wilaya ya TABORA
Hivyo Basi 302,940 Hela 5 ya Shaba ziliundwa
325,000 Hela 20 ya Copper na Shaba pia Ziliundwa.
Wakati huo katika kubadili Hela

1 Rupie au Indian Rupee=100 Hela
Mpaka wa leo Watanzania Sarafu zao zinajulikana kama Hela.
Credit: mdau FB
1759320928995.jpg
1759320925725.jpg
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu. Hizo hela nilizitumia wakati wa utoto kabla hazijabadilishwa kuwa shilling ya afrika mashariki.
Senti moja iliweza kubadilishwa kwa ndizi kisukari tano. 😂
Nilizikuta zinaishia zile senti 5 zenye yule samaki papa upanga.. Moja ilikuwa inanunua bazoka 5
5-senti-tano-1973_15099_51164710c89f65L.jpg
 
Kiswahili ni kigumu sana, kuna Hela, Pesa, Fedha, Mpunga, Maokoto, Noti, Mkwanja n.k ni mladi vulugu tupu, inakupasa kuwa makini kuelewana na watu wa aina mbalimbali.
 
Kiswahili ni kigumu sana, kuna Hela, Pesa, Fedha, Mpunga, Maokoto, Noti, Mkwanja n.k ni mladi vulugu tupu, inakupasa kuwa makini kuelewana na watu wa aina mbalimbali.
Kiswahili siyo kigumu ila waongeaji ndiyo wagumu kujifunza. Sasa kama wewe tayari umeshabadili maneno kama ''mradi'' unaandika ''mladi''. ''Vurugu'' unaandika ''vulugu''. Shule ulikwenda kufanya nini?
 
Nilizikuta zinaishia zile senti 5 zenye yule samaki papa upanga.. Moja ilikuwa inanunua bazoka 5View attachment 3481934
Wazee wengi wa kichaga walikuwa wanaita fedha ''heleri''. Ni kutokana na hilo jina la kijerumani. BTW Mshana Jr hata neno ''shilingi'' siyo letu. Mizizi yake iko Uingereza na Ujerumani. Waingereza zamani sana walikuwa na neno ''Scilling'' kwenye mambo ya account na baadae fedha.
 
Shule hakuna kipindi nilikua nakipenda kama mapumziko...
 
Wazee wengi wa kichaga walikuwa wanaita fedha ''heleri''. Ni kutokana na hilo jina la kijerumani. BTW Mshana Jr hata neno ''shilingi'' siyo letu. Mizizi yake iko Uingereza na Ujerumani. Waingereza zamani sana walikuwa na neno ''Scilling'' kwenye mambo ya account na baadae fedha.
Yeah shillingi limetoholewa toka kwenye kimombo shilling
 
Nilizikuta zinaishia zile senti 5 zenye yule samaki papa upanga.. Moja ilikuwa inanunua bazoka 5View attachment 3481934
Acha hizi, ni sarafu za mwanzo kabisa kutolewa baada ya BOT kuanza kutengeneza shilling ya Tanzania. Mimi nimezikuta hizo hela zenye tundu katikati. Zilkuwa zinafungwa kamba kwa mafungu!... Hela za Tanganyika baada uhuru zile.
 
Hizo nilibahatika kuziona lakini zikiwa tayari zimeshatolewa kwenye mzunguko
 
Back
Top Bottom