GE2025 Asha-Rose Mtengeti Migiro ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Achukua nafasi ya Balozi Nchimbi

GE2025 Asha-Rose Mtengeti Migiro ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM. Achukua nafasi ya Balozi Nchimbi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa imemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ambaye ni Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
Pedeshee Makala karibu FM ACADEMIA, leo tupo Tegeta kwa Ndevu
 
Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa imemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ambaye ni Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
huyo Mchimbi anagombea kwenye uchaguzi gani/upi
 
Hajastafu tu, ok hii ni ya kimkakati mana cv za huyu mama ni kubwa ikiwemo kuwa katibu mkuu wa kwanza mwanamke mweusi kwenye shirika kubwa kipind kile, jamaa washa jipanga zamani sana Kuna jamaa nmemwambia Hawa ccm wamesha jipanga zamani sana kama nikuwazuia tushachelewA

Fullstop, kwishaaaa
 
Kutoka naibu katibu mkuu UN mpaka katibu mkuu ccm kutukanana na akina Heche.bonge moja ya dharau
 
Aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Mtengeti Migiro amethibitishwa na CCM kuwa Katibu MKuu wa CCM akichukua nafasi ya Dkt Emmanuel Nchimbi ambeye aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa rais Samia nafasi ya urais 2025

Pia CCM imelithibitisha jina la Kenani Kihongosi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Arusha kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi, na Mafunzo akichukua nafasi ya Amos Makalla
unaibu Katibu mkuu alifukuzwa UN
 
Hajafikisha miaka 80 kweli huyu mama

Yote kwa yote abalikiwe sana
Namtakia majukumu mema
80 hajafikisha, lakini kishavuka umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Katibu mkuu ni full time employee wa chama, hatakiwi awe zaidi ya miaka 60.
 
Watu wale wale walioshindwa ndio wale wale wanaletwa kweli hii nchi itakuwa kazi Sana kuikomboa

Huyu naye ni wale payroll Rostam

Kazi ipo!!
 
Back
Top Bottom