Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪#‎TegetaEscrow‬. Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri? Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?
Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale.
Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa
1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO
2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania
3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo
Source ukurasa wake wa FB
kama hiyo siyo ndoto basi mtupie hizo hoja tatu ulizoshauria na yale mengine ya maamuzi ya Bunge yanayosubiri utekelezaji wake-uone ataruka kiasi gani!Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale.
Kujikombalishious
Kachanganyikiwa jamani msimlaumu
Muhongo - Kuna kijana mmoja yuko upinzani ni mlafi sana wa rushwa...
Muhongo - Nashukuru chama chake wamemfukuza....
Mchange - Muhongo alijiuzuru with confidence...
ACT ni chama cha watu wenye msongo wa mawazo...
zitto anaongea fact, mburula atapinga kwa umbullula wa kutokujua mambo
Hiki ndiyo kinachonifanya nimkubali sana Mh. Zitto. Kwenye ukweli huwa anaongea ukweli japo wakati mwingine huwa nahisi anatumiwa na hawa wafanyabiashara wezi wanaojiita wazawa.
Inawezekana mkuu.
Huyu jamaa miaka hii ya karibuni siasa zake nimeshindwa kuzielewa kabisa. Leo atasema hivi, kesho vile. Siyo mtu wa kuaminika.
Huu ndio msimu wa ZZK kujikomba sana kwa watawala...
Fahamu zake zote zimeshamtoka pale alipo..
Kisa... uenyekiti wa PAC.
Professional Mnafiki!
Ina maana PAC ilikurupuka?
Ina maana Bunge lilifikia maazimio husika bila ya kujiridhisha?
Zitto alibadilika bungeni wakati wa mjadala husika na kuhamia upande wa pili wa hoja. This is Self defense mechanism at work. It is also a a pre -emptive strike kuelekea bunge lijalo, kwa maelekezo ya chama kilichomsaidia ubunge (CCM). Kitila Mkumbo alishaweka wazi kupitia gazeti la Raiamwema kwamba lengo kuu la ACT ni kupambana na upinzani (Chadema), sio chama tawala. Hizo ndio siasa za upinzani wanazotaka CCM. Ndio maana chama hiki kikahakikisha kwamba kinamsaidia Zitto arudi bungeni. Bila ya juhudi za CCM Kigoma (Zikiongozwa na Kikwete), kumzima Kafulila na kumpaisha Zitto, huyu mtu asingerudi bungeni.
Huu ni mwanzo tu, tutarajie burudani zaidi kutoka kwa Zitto.
...sijawahi na wala sitakaa nikaamini hako kajamaa,mpk kamati zote za bunge zitakapopata wenyeviti ndio labda nitaanza kukasikiliza.
Kameshakimbilia upande wa ccm,coz kanajua ccm ndio wengi wenye uwezo wa kumpa kamati bungeni,nothing elz!
the double minded man, unstable in all his ways. james 1:8
continustion of lack of INTEGRITY.
VITAL CHARACTER OF TRUE LEADERSHIP.