Asante!!!

Nashangaa watu wanabania wakati sio pesa.

@SL. . . nakusamehe kwa sharti la kuninunulia vitumbua kesho asubuhi.Au soda na biskuti baadae.
Asante Lizzy, mie najitolea kununua vitumbua kesho asubuhi...
 
we na (TS) kwani mmeamkia wapi leo?
Hope unamaanisha TF hapo kwenye mabano... Bishanga mie kama kawaida nimeamkia nyumbani na The Finest pia kama kawaida ameamkia............(jaza mwenyewe manake unajua) na huko ndiko alikoambiwa 'Thank You'
 
orait tunakwenda by elimination,Husninyo njoo ujazie hizi desh desh!
 
Even if she was crying, a little cooperative after the "DO", look her in the eyes, smile by your eyes, then say "thanks"! Ooh men, this is a poison! The power of asante. Ninaweza sahau kushukuru menu, lakini si kwenye hili jambo.
 
Nadhani baadhi yetu kama sio wengi tunajua nguvu ya neno asante na umuhimu wa kushukuru pale mtu/watu wengine wanapokua wamejituma, jitolea kwaajili yetu.Kwa kushukuru mtu anapokuwia mkarimu inafanya kesho awe tayari kuwa mkarimu tena mwako, kwakushukuru pale mtu anapokua amejituma/jitahidi kufanya kitu kwaajili yako kunafanya huyo mtu aongeze juhudi. Kinyume cha hapo ndio unakuta mtu anafanya na kulipua kitu kwasababu analazimika na ingekua uamuzi wake asingefanya kabisa.

Mimi nimewahi kukutana na watu ambao hata kusema asante kwa chakula hawajui au sijui niseme hawawezi.Mimi niliwashangaa kwa kutokushukuru na wao walinishangaa kwa kuuliza mbona hawashukuru, ila baada ya kuwaeleza kwanini nadhani ni muhimu kufanya hivyo wakanielewa na kuanza kulitumia neno "ASANTE" ipasavyo.

Je wewe kama wewe mara mwisho umemwambia dada wa kazi, mzazi wako, mwenzi wako asante baada ya kula ni lini?
Mara ya mwisho kumwambia mtu asante baada ya kutekeleza kitu chochote kile ulichomwomba/mwagiza afanye ni lini?
Mara ya mwisho umemshukuru hata mpishi/mhudumu wa hoteli au mgahawa ni lini?
Mara ya mwisho kumshukuru mwenzi wako kwa kuwa na wewe bega kwa bega ni lini?
Mara ya mwisho kumshukuru dada wa kazi kwa kukulelea mwana/wanao ilikua lini?
Mara ya mwisho kumshukuru mtu yeyote yule kwa sababu yoyote ile ni lini?

Kama hukumbuki au ilikua muda mrefu sana badilika.Hata mtu unaemlipa anastahili asante kwasababu angeweza kufanya anachofanya kwa kulipua pamoja na kwamba unamlipa.Jifunze kushukuru uwape watu morale ya kuendelea kukusaidia na kukutumikia kikamilifu, pia raha ya kuwa karibu nawe.

Jumatatu njema.

Ahsante sana Lizzy. Neno hili kama ambavyo ilivyo kwa maneno matatu "I love you" lina nguvu sana. Kwa wengi bado wanalitumia sana kama inavyostahili kila mara wanapoona umuhimu wa kulitumia neno hilo. Sijui kama neno hili nalo limeshachakachuliwa na hivyo kupoteza maana yake halisi. Hata hapa jamvini kuna wengi sana wanalitumia neno hilo.
 
Hii thread inaonyesha umuhimu wa kurudishwa kwa kifute cha "Thanks". Maana kui-like tuu sidhani kama inatosha. May be Watanzania tunapenda zaidi ya kushukuru? Kwamba kupenda na kupendwa is the way forward? Kwenye nchi za wenzetu, maneno yanayotamkwa mara kwa mara ni "Thank you" na "Sorry". Kwetu unaweza pitisha wiki bila kuambiwa "asante" au "samahani" au hata kusikia mtu mwingine akitoa asante au kuomba samahani.

Kwa hapa JF, mara mwisho kusema "Thanks" publicly ilikuwa kwenye hii thread (https://www.jamiiforums.com/tech-ga...s-facebook-and-twitter-accounts-hacked-4.html), though tokea hapo nimeshasema asante kadhaa kwenye PMs. Anayehitaji Asante ani-PM tuu.
 
Hii thread inaonyesha umuhimu wa kurudishwa kwa kifute cha "Thanks". Maana kui-like tuu sidhani kama inatosha. May be Watanzania tunapenda zaidi ya kushukuru? Kwamba kupenda is the way forward? Kwenye nchi za wenzetu maneno, maneno yanayotamkwa mara kwa mara ni "Thank you" na "Sorry". Kwetu unaweza kupitisha wiki bila kuambiwa "asante" au "samahani".

Mkuu EMT, mie huwa napenda sana kuangalia reaction ya watu kwa mfano mtu amekutangulia na hamfahamiani akafungua mlango halafu akakushikia nawe ukaingia, ukitoa thank you unamuona anaachia tabasammu la nguvu kabisa kuonyesha kuridhishwa/kufurahishwa na shukrani uliyompa. Hilo la kwetu ni kweli kabisa.
 
Mkuu kwa wenzetu wanajua maana ya Asante. Kwetu wengine hata ukimwambia Asante kwa kitu kidogo tuu anakushangaa. Unaweza kumwambia dereva wa daladala asante kwa kukufikisha salama uendako? Kwanza atakushangaa sana. Na huyo msafiri atadai atampaje asante dereva wakati nauli amelipa? Who know may be kusema tuu "asante kwa kunifikisha salama" inaweza hata kupunguza madereva wa mabasi kuendesha ovyo as they will feel appreciated kwa kazi wanayoifanya? Lakini mara nyingi asante za Tanzania ni rushwa. Unamwambia mtumishi wa umma asante kwa kushughulikia tatizo lako kwa kumpatia rushwa. Asante ya maneno haitoshi na ukirudi tena lazima akuzungushe.
 
Ahsante sana Lizzy. Neno hili kama ambavyo ilivyo kwa maneno matatu "I love you" lina nguvu sana. Kwa wengi bado wanalitumia sana kama inavyostahili kila mara wanapoona umuhimu wa kulitumia neno hilo. Sijui kama neno hili nalo limeshachakachuliwa na hivyo kupoteza maana yake halisi. Hata hapa jamvini kuna wengi sana wanalitumia neno hilo.

Tuko pamoja BAK.
Kuhusu neno kuchakachuliwa sijui kwakweli, maana kua mtu alichangia mapema akasema kwamba asante nyingi ni za kinafiki ila hakufafanua zaidi ya hapo. Mimi bado naamini kwamba kila anaepewa asante anastahili kwa namna moja ama nyingine, na wale wasiotoa ni kwamba wamekosa appreciation.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hii thread inaonyesha umuhimu wa kurudishwa kwa kifute cha "Thanks". Maana kui-like tuu sidhani kama inatosha. May be Watanzania tunapenda zaidi ya kushukuru? Kwamba kupenda na kupendwa is the way forward? Kwenye nchi za wenzetu, maneno yanayotamkwa mara kwa mara ni "Thank you" na "Sorry". Kwetu unaweza pitisha wiki bila kuambiwa "asante" au "samahani" au hata kusikia mtu mwingine akitoa asante au kuomba samahani.

Kwa hapa JF, mara mwisho kusema "Thanks" publicly ilikuwa kwenye hii thread (https://www.jamiiforums.com/tech-ga...s-facebook-and-twitter-accounts-hacked-4.html), though tokea hapo nimeshasema asante kadhaa kwenye PMs. Anayehitaji Asante ani-PM tuu.

Kuomba samahani na kusema asante kwa baadhi ya watu ni sawa na kujidharaulisha. Yani haoni maana ya kumpa mtu ambae yuko chini yake kielimu/kifedha/kicheo (madereva taxi, waalimu, wamachinga, wahudumu, wapishi, masecretary, kaka na wadada wa kazi n.k) asante, pole ama samahani. Hivyo dharau nayo inachangia kutokua mkarimu wa hivyo vitu.

Hehehehehe ntakuPM "ASANTE" ili na mie unipe maana hutaki kutoa hadharani.
 
Mkuu EMT, mie huwa napenda sana kuangalia reaction ya watu kwa mfano mtu amekutangulia na hamfahamiani akafungua mlango halafu akakushikia nawe ukaingia, ukitoa thank you unamuona anaachia tabasammu la nguvu kabisa kuonyesha kuridhishwa/kufurahishwa na shukrani uliyompa. Hilo la kwetu ni kweli kabisa.
Kweli kabisa BAK. . .hata mimi nikimshikia mtu mlango alafu asiposema asante sitabasamu, ila akisema asante najisikia raha sana.
 
Tuko pamoja BAK.
Kuhusu neno kuchakachuliwa sijui kwakweli, maana kua mtu alichangia mapema akasema kwamba asante nyingi ni za kinafiki ila hakufafanua zaidi ya hapo. Mimi bado naamini kwamba kila anaepewa asante anastahili kwa namna moja ama nyingine, na wale wasiotoa ni kwamba wamekosa appreciation.

Nakubaliana nawe kabisa Lizzy.
 
Kweli kabisa BAK. . .hata mimi nikimshikia mtu mlango alafu asiposema asante sitabasamu, ila akisema asante najisikia raha sana.

Unaona!!! au umeingia kwenye Elevator ukamuona mtu nyuma yako naye anawahi ukamshikia ili naye awahi kuingia akikushukuru basi hujisikia raha sana :):) Mie nazitoa nyingi sana kwa siku lakini sidhani kama zimefika 100 :):) kwa siku na pia nazipata nyingi sana.
 
Heheehhe mwingine anaingia hata salam hakupi kajinunia zake utadhani wewe ndo uliyemwamsha asubuhi.

Hehehehhe we toa tu hata kama ni moja alimradi anaepata anastahili.
 
Heheehhe mwingine anaingia hata salam hakupi kajinunia zake utadhani wewe ndo uliyemwamsha asubuhi.

Hehehehhe we toa tu hata kama ni moja alimradi anaepata anastahili.

Kuna mtu alianzisha thread hapa jana akilalamika alimwagijwa mboga ya maharagwe kwenye mgahawa. Jamaa hata hakuomba radhi bali alidai angepitaje wakati mgahawa ulikuwa umejaa vile.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom