Asante Vodacom Kwa Kunifanya Niwagundue BABA LAO!

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Nilikuwa navifurahia sana vifurushi vya CHEKA BOMBASTIK vilivyokuwa vikiuzwa na mtandao wa Vodacom. Kipengele cha 'Kwenda Mitandao Yote' kwenye hicho kifurushi kilikuwa mkombozi wangu. Vodacom sijui walipata ushauri kutoka wapi, ghafla wakarekebisha kipengele cha 'Kwenda Mitandao Yote' na kupunguza mvuto wake. Kwa kuwa nahitaji mawasiliano na watu wangu walio kwenye mitandao mingine, nilianza kazi ya kutafuta mtandao mbadala. Tafuta yangu ikanifikisha mtandao wa Airtel. Hawa, wana vifurushi maridadi sana kuliko huko nilikotoka!Vifurushi vya siku ni kwa kila aina ya mfuko, kuanzia sh 399 mpaka 999 unachagua. Mimi hujiunga kile cha sh 999 ambacho unapata dk 40 kupiga mtandao wowote Tz, meseji 1000, na MB 300 za intaneti. Mungu anipe nini zaidi? Voda wasingenitibua, nisengegundua haya mambo ndo maana nawashukuru!
 

uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,220
2,000
hivi hawa airtel bado tatizo la kuingiliana mawasiliano linaendelea , mimi nilitoka airtel kwa kuwa walikuwa hawalijali sana swala hili la muungiliano
 

Ringtone

JF-Expert Member
Nov 21, 2013
489
0
Omba na hao "baba lao"wasije badili hivyo vifurushi.
Hi umesahau baba lao,walikuwa ni celtel,zain..........next sheikatel
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
5,961
2,000
Unajiungaje?mimi nilipewa eti nipige namba fulani na hao hao airtel nilivyoipiga naambiwa haipatikani!Michisho tu hii mitandao hata hakuna cha baba la nani sijui

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Lastname

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
922
195
airtime nayowekewa na ofisi nauza siku hizi kwa anayetaka. mpaka uchaguzi upite 2015
 

foshizzle

JF-Expert Member
Dec 4, 2013
374
0
Mkuu mimi utamu wa mitandao naupata kupitia mtandao mpya wa BOL. Nikiweka 5000 nasahau kabisa mambo ya vocha. Jaribu uone. Internet inakua free mwezi mzima.
 

Chen Hu

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
3,241
2,000
Jamani Vodacom wapo katika wakati mgumu sio siri.
Jana nilienda Mlimani City kwa ajili ya hao voda, sasa katika foleni kuna brother alinitangulia. Yule braza akawa analalamika kuwa kila siku wanamwibia hela na huwa anavumilia ila kwa jana walimwibia 2000 asubuhi, akaweka 10,000 wakamwibia tena wakati hajafanya matumizi yeyote.. Sasa yule mhudumu akajibu kinyodo nyodo. Lol, ilinibidi nirudi hatua moja kweye foleni na niliyemwachia foleni naye akakimbia na kuniacha mimi. Hii ni kutokana jamaa kuwaka kwa malalamiko lukuki huku kubwa ni kuwa haondoki mpaka arudishiwe pesa yake yote na hatoki mpaka kieleweke. Dada ikabidi awe mpole kwa kumwonesha lile dirisha la upande wa kushoto.
Kutokana na jamaa alivyokuwa na hasira akauliza aingie ndani kabisa? dada kwa upole akajibu hapana kaka, ni hapo dirishani tu.
Nilichojifunza ni kuwa bila kuwa mkali kwenye haki yako, utaendelea kuibiwa daima.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom