Serikali ya CCM imeandaa bajeti ambayo ina mlenga zaidi mlala hoi kwa maana ya kumpunguzia mzigo wa kodi huku ikiwabana wenye vipato vya kati na vya juu!!
Katika bajeti hii ya serikali ya mwaka 2013/2014, imeondoa kabisa kodi ama kupunguza kodi kwa kiwango cha kuridhisha kwenye maeneo fulani fulani ambayo yana athiri sana watu wenye vipato vya chini.
Maeneo ambayo serikali imeondoa kabisa kodi ama kuipunguza kwa kiasi cha kuridhisha ni kama ya yafuatayo;
1. Boda boda na Bajaj hakuna kodi, hivi ni vyombo vya usafiri ambavyo injini zao ni chini ya 501cc, vyombo hivi vimekuwa msaada mkubwa kwa vijana wengi kwani vimeweza kuwapatia vijana vipato na kuwaletea maendeleo.
2. Mafuta ya taa hayata kuwa na ongezeko la kodi, kwa kutambua kuwa nishati hii inatumiwa sana na watu wa kipato cha chini, serikali itaendelea kutoza ushuru wa Tshs. 400/= kwa lita.
3. Ununuzi wa magari mapya marufuku, kwa kutambua kuwa gharama kubwa utumika kwa manunuzi ya magari mapya, serikali imepiga marufuku manunuzi ya magari mapya ili kupunguza matumizi ya kawaida.
4. Kodi ya mshahara itakuwa 13%-14%. Kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi sasa kimesikika na serikali kuwapa unafuu kwa kupunguza kodi kwenye mishahara.
Ila kama ilivyo ada, hakuna zuri lisilo ambatana na lawama, dhihaka na kejeli, wapinzani na watu wasio na mapenzi mema na taifa wamelaumu eti hii bajeti itaongeza ukali wa maisha hasa kwa watu wa vipato vya chini. Haya maneno hayana ukweli wowote kwani dhumuni la hii bajeti ni kupunguza mzigo kwa walipa kodi ili kupunguza ukali wa maisha.
Aidha, watu wengi wanao lalama ni wenye vipato vya juu, kwani wengi wao wanajua kuwa kodi kubwa imeelekezwa kwao, hasa wale watumiaji wa mvinyo, kwa ule mvinyo wa dhabibu za nchini utatozwa sh 160 kwa lita badala ya sh 145, mvinyo wa dhabibu za nje ushuru umepanda kutoka sh 1641 mpaka sh 1775 kwa lita, huku vinywaji vikali vikitoka sh 2392 mpaka sh 2631.