Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?

Kuna muda Pascal Mayalla anarudi na kujiteka mwenyewe. Niseme pia maisha ni bahati unaweza ukasifia sana na usibahatike kamweee

Unaweza ukatumia akili mno na usipate kitu, unaweza kuwa mropokaji na ukapata kila kitu mpaka usivyokua ukihitaji.
Mkuu Tape measure sijui ni kwanini watu humu mnadhani natafuta uteuzi?. Hili mbona nimelisema sana tuu humu! Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza! na hata makala nimeliandikia
Hiki ninachofanya sasa
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=rvw5xRKq8ry8fDN_Kina maslahi makubwa kwa taifa kuliko ningeteuliwa position yoyote!.
P
 
Bandiko hili liliomba mambo 4.
1. "tunaamini soon Rais Samia ataruhusu mikutano ya vyama vya siasa,:"
2. ataifanyia marekebisho Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuifanya kuwa tume huru zaidi na shirikishi,
3. atazifanyia marekebisho sheria kandamizi zinazonyima haki
4. sheria batili, kwasababu zinakwenda kinyumbe cha Katiba ya JMT, ubatili huo, bado umechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!.

Rais Samia ametimiza mambo matatu, bado moja hili la katiba.
Tuendelee kumuombea ili hili aliweze.
P
 
Mkuu Lax karibu pande hii ushuhudie.
P
 
Reactions: Lax
Kwa vile leo ni birthday ya Rais Samia, nawaomba wana jf wote ambao ni well wishers, tuungane kumu wish Happy Birthday this lovely lady Rais wetu mpendwa, Rais wetu mpenzi, Rais wetu kipenzi, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, Chifu wa kabila kubwa kuliko makabila yote Tanzania, ambayo Kanda ya kabila hilo ndio Kanda determinant ya kura za urais wa JMT, Chifu Hangaya. View attachment 2497334
Happy Birthday.

P
 
Wakati anachukua madaraka yes, alishakutana na makonki na kajifunza leo hii ni mtu mpya kabisa
 

Samia is not humble, wewe hujui tabia zake? Rais huyu ni wa ovyo, kimsingi hafai.
hawezi kuwa wa ovyo na hafai wakati mpaka hapa tulipo tayari ameisha tufaa sana tuu!,au kwako licha ya kufanya hili jema wewe kwako bado ni mtu wa hovyo na hafai?。
P
 
hawezi kuwa wa ovyo na hafai wakati mpaka hapa tulipo tayari ameisha tufaa sana tuu!,au kwako licha ya kufanya hili jema wewe kwako bado ni mtu wa hovyo na hafai?。
P
Subiri uteuzi wa CCM, maana wewe hueleweki unabadilika badilika kama kinyonga. Au wewe ni katika wale wasaidizi wake wanaobaka na kulawiti watu wasio na hatia?
 
Ulikurupuka bwana Njaa.
 
Naona ume umma na kupuliza
 
hawezi kuwa wa ovyo na hafai wakati mpaka hapa tulipo tayari ameisha tufaa sana tuu!,au kwako licha ya kufanya hili jema wewe kwako bado ni mtu wa hovyo na hafai?。
P
Wewe ndiye uliyefanya Eric Kabendera aumizwe na jiwe. Acha kuongea onge sana mambo ya uchonganishi au ya kutania, Watanzania wanatekwa, wanalawitiwa na wanabakwa wewe huoni hilo.
 
Ukiongea unayoyaongea wakati mwingine kwa question marks, wale ambao hawana akili wanafanya kufuata maelekezo. Haya mambo tunayaona yanatokea katika nchi yetu (hii ni nchi yetu sote, siyo ya Samia, Abdul, Mwanu na Mcherengwa wenyewe). Maria Sarungi alitekwa mara baada tu ya huyo mjinga kusema, Padre Dr. Kitima alijeruhiwa mara baada ya yule mjinga wa mkutano mkuu kusema, Kila anayeongea kitu haipiti wiki moja au mbili kinatendeka. Hiyo ni hulka ya watu wasiojua kupanga, wanafanya mambo yao kwa kuwa "activated". Siyo mimi tu nasema haya, kila mtu anaona. Kwani ukinyamaza bila kuchonganisha, unakosa nini? Off course Karma itakuja tu.....Still we have time.
 
Kweli ni msikivu
 
moja kati ya maandiko ya kiduanzi hili mojawapo.
 
Ok, hatuna nia mbaya na wewe. I hope Karma won't get you.
The law of karma is the law of the cause and effects of your actions, you get what you do, unavuna ulichokipanda, ukipanda mema, unavuna mema!, ukipanda.uovu, unavuna bakora za kutosha na malipo ni hapa hapa duniani.

Hata kama mtu ana nia mbaya na wewe, ana ku wish mabaya, kama wewe sio mbaya, hayakupati!.

Karma haina mswalie Mtume, wala haujui nani ni nani!, ndio maana niwasisitiza watu humu tuwaze mema, tuseme mema, tutende mema!
P
 
Wanabodi,

Asante Mungu kwa Rais Samia, ni Baraka kwa nchi yetu!, naomba lile jicho, liuone na ubatili huu ndani ya katiba yetu, lituondoshee kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025!.

Mungu Mbariki Rais Samia,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
It's very unfortunately, jicho la Mama, Halikuuona ubatili huu, haya sasa ni matokeo ya ubatili huu!.
Mkuu Kozi Kodineta Course Coordinator, bandiko lako hili GE2025 - Majina haya ya Wabunge waliokatwa majina kwa Visasi vya Mwenyekiti limenigusa sana
Haya ni matokeo ya Watanzania kuukubali ujinga wa kuingiza siasa kwenye katiba ya nchi kwa kuchomekewa kifungu batili cha kulazimisha wagombea wadhaminiwe na chama cha siasa.

Ibara ya 5 ya katiba imetoa haki kwa kila Mtanzania kumchagua kiongozi unayempenda, na ibara ya 21 imetoa haki kwa kila Mtanzania kugombea bila shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa.

Hao wote waliokatwa na chama chao, kama ni vipenzi wa wananchi wao, walipaswa wasimame kama independent candidates na wangechaguliwa na wananchi wao.

Hiki kipengele cha mgombea kudhaminiwa na chama cha siasa ni dhulma kubwa kwa Watanzania.

Kuna baadhi ya laana nchi yetu inazipata kutokana na dhulma kama hizi!.

Nimekuleta ili uone jinsi tulivyopigia kelele dhulma hii.

Huyu naye alipoanza tulikuwa na matumaini makubwa kuwa atatenda, kumbe ....
Naomba nisimalizie ...!

Ila Mungu Yupo!.

Paskali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…