Asante Magufuli, sasa umetukumbuka Rungwe, Mbeya

Asante Magufuli, sasa umetukumbuka Rungwe, Mbeya

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,647
Reaction score
14,645
Kimya kingi kina mshindo.
Baada ya vilio vya kutaka barabara wilayani Rungwe, sasa Magufuli katukumbuka.
Kura yangu iliyokuwa na ukakasi sasa unayo baba Magufuli.
20181123_074407.jpg
 
Sugu kwisha habari yake

Kila akipewa hela ya mfuko wa jimbo anatafuna tu hela kwenye kihoteli chake uchwara, badala ya kuwaletea maendeleo wananchi
 
Nimeona Jamaa wanabishana kuwa Tz ni nchi ya ahadi, sikuelewa, kumbe maana yake ni nchi raia wake wamezoea kuishi kwa ahadi.
 
Sikudhani kama we jamaa ni mnyonge kjijinga namna hii , maendeleo ni haki yenu ya msingi na wala si fadhila za mtu yeyote , huna haja ya kugalagala chini ili kushukuru , huyu unayemshukuru muda wake ukifika ataondoka lakini Rungwe itabaki ,

umejidhalilisha sana mkuu .

IMG-20180811-WA0018.jpg
 
Ana haki ya kushukuru maana ni mda wa miaka mingi anaahidiwa bila kutekelezewa, mfano hata awamu hii hizo hela ingezipangia kazi zingine haki yake hiyo angeionaje au haki yake ni kuahidiwa bila kutekelezewa?, mwaacheni ashukuru kwa kuletewa sasa angeweza kusubiri hiyo haki yake mpaka aingiapo kaburini
 
Sugu kwisha habari yake

Kila akipewa hela ya mfuko wa jimbo anatafuna tu hela kwenye kihoteli chake uchwara, badala ya kuwaletea maendeleo wananchi
Mkuu habari yako! Sugu ni Mbunge wa Mbeya mjini,Busokelo ni jimbo linalojitegemea na lina Mbunge wake anaitwa Mh.Fred Mwakibete,mara ya kwanza liliitwa jimbo la Rungwe Mashariki kwa Mh.Mark James Mwandosya.
 
Ni Tanzania pekee wanaoona kuletewa huduma ni favor na sio wajibu wa serikali.

Ulishawahi ona TRA wanakubembeleza na kukushukuru wewe kulipa kodi?

Unamshukuru kwa kukujengea barabara wakati ni wajibu wake.
 
Back
Top Bottom