Asante Bashiru, tumewajua machawa Halisi

Asante Bashiru, tumewajua machawa Halisi

"mali ya mtu mmoja au kikundi cha watu wachache ambao wao ndio huwa sheria, anayepinga watakayo huoneshwa cha mtema kuni"
Sio kila siku ni Jumapili,kuna saa na siku ubao utasimeka tofauti na mazowea!

Kwa kina Ayatolah-khomein,hawakutarajia wanachokiona leo pale Tehran!

You Can Fool Some People's SomeTime,But You Cant Fool All The People at All Time!
 
Ccm wanatengeneza viungo ambao hawapaswi kujenga hoja ni kusifu na kuabudu. Na ili limeanza kutengenezwa kuanzia ngazi ya vijana ya uvccm.

Wanaamini aliye juu yako kimadaraka wala hawezi kosea. Ata maofisini bosi ukosea na unaweza mueleza.

Yote aya ni zao ya huyo huyo bashiru aliyekua anafurahi muda wa kusifu na kuabudu jiwe
Kusifu sio kosa,bali kusifu yale yasiyostahili ndio kosa!
Wala hatukatai kusifu au kusifiwa,bali tunakataa sifa za "Uongo" na "Unafiki"
 
Usipoijua historia yako vizuri huwezi kujua ulipotoka, ulipoangukia na unapoelekea.
Na aliyewaroga watanzania ni huyu anayewaambukiza ugonjwa wa kupigana na historia,badala ya kupambana na yaliyopo kwa sasa!

Mnauziwa ubaya wa waliopita,huku mkiliwa na waliopo,kwa kujikaanga na mafuta yenu wenyewe!
 
Bashiru ni mwiba na Bashiru ni mwamba. Kuna vijeba na watoto wadogo ndani ya CCM wanadhani wanaweza kumteteresha kirahisi Bashiru, huyu mwamba kubwa lao.

JK anamwelewa vizuri sana Bashiru kama yeye Bashiru anavyomwelewa vizuri sana JK na CCM yetu. Amekuwepo hata kabla ya "REDET" na akawepo baada ya "mtandao" na sasa yupo nyakati za "bibi tozo".

Akiamua kusimama wa kuweza kusimama naye hawafiki hata 5 kwa CCM yetu ya leo, chama anakijua na chama kinamjua nje ndani. Chama kimemtumia na chama kakitumikia kwelikweli Bashiru

Mengi anayo Bashiru ila tupeane nafasi katika kuongea
 
Bashiru ni mwiba na Bashiru ni mwamba. Kuna vijeba na watoto wadogo ndani ya CCM wanadhani wanaweza kumteteresha kirahisi Bashiru, huyu mwamba kubwa lao.

JK anamwelewa vizuri sana Bashiru kama yeye Bashiru anavyoielewa vizuri sana CCM, amekuwepo hata kabla ya REDET na akawepo baada ya "mtandao" na sasa yupo nyakati za bibi tozo.

Akiamua kusimama wa kuweza kusimama naye hawafiki hata 5 kwa CCM yetu ya leo, chama anakijua na chama kinamjua. Chama kimemtumia na chama kakitumikia Bashiru

Mengi tunayo ila tupeane nafasi katika kuongea
Na huo ndio ukweli halisi ambao wana CCM- Saa100 hawataki kuuelewa!
Sijui ni kwa bahati mbaya au ni kwa kujitoa ufahamu shauri ya tamaa ya mali!

Muda ndio utakaowafundisha ukweli halisi.
 
CCM Imegeuzwa Chaka la "Wahuni!"
Madokta wa "kihuni" kama #Kigwangalla!
Vijana Wa "Vihoja" kama #Kihongosi!
Wazee wa "Mipasho" kama #Bulembo!

CCM imegeuka chaka la wahuni,msemakweli ndie adui yao!

Hapo hakuna "Taasisi",bali kuna "Wahuni" na
"Wanaupiga Uhuni Mwingi"

Unapokuwa na Wasomi wa Makaratasi kama Kigwangalla!

Aliyetumia uwaziri kustarehe na wasanii kwa gharama za wizara!

Aliyetumia muda mwingi wizarani kugombana na katibu mkuu wake,kisa anakiuka maadili ya uwaziri!

Hatimae Rais akafanya vyake,katibu mkuu akawa waziri kwa sasa.
Huku Kigwangalla ni "Chawa" kwa sasa!

Ukawa na vijana wa Vioja kama Kihongosi.

Ambaye amekomaza shingo kuachia ngazi,pamoja na kuhusishwa kwenye kashfa za kuiba fedha za jiji la Arusha kupitia mkewe!

Halafu leo na yeye anapata ujasiri wa kumkosoa aliyesababisha hiyo CCM ikabaki ilipo!

Tunajua ma-CCM mengi yanao uchungu na #Bashiru,sio kwa sababu ya kumtetea mama yao!

Bali kwa hasira za kukatishwa ulaji na Tume ya kukagua na kuratibu mali za CCM.
Iliyoongozwa na Bashiru

Ni kupitia hiyo tume ndio kina #Bulembo walitemeshwa ulaji kutoka mauzo haramu ya shule za "TAPA"
Jumuia ya wazazi wa CCM!

Ni hiyohiyo tume ya #Bashiru,iliyowatemesha kina #Nape magari ya CCM waliyojimilikisha bila haya mchana kweupe.
Ila kwa tume ya #Bashiru,na misimamo ya #JPM.
Vyote vilirudi.

Wanaompinga Bashiru leo,ndio hao walikiuza kiwanda cha uchapaji cha CCM.

Ndio hao waliokuwa wamemuuzia Yusuf Manji kituo cha television cha CCM cha "Chanel Ten"

Yoote yaliharibika,baada ya #Bashiru kufanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa!

Tunajua kabisa,sababu zilizowafanya walamba Asali waanze na kumuweka #Bashiru pembeni mapema!

Ni kwa sababu uwepo wake kama katibu mkuu,yanayotokea sasa,yasingewezekana kamwe!

Ni mengi na Ni wengi waliotemeshwa ulaji!

Ila pia tunajua walamba asali walivyoratibu zoezi la kuwafagia wazee wakweli ndani ya CCM.

Wengine wakiponea tundu la sindano,kina Mang'ula!

Ambao hawakubahatika ndio ikawa historia.
Mmoja wa waliosalimika akazawadiwa U- Vaisi- presoo!

Tunaomba mumpinge #Bashiru kwa "HOJA" badala ya "VIOJA"

Bashiru anayajua mengi ndani ya hicho chama,tena anayajua "MABAYA" yenu kuliko "MAZURI"

Kaeni mkijua kwamba Baba wa Taifa aliacha waosia huu....

"UPINZANI WA KWELI WA CCM,UTATOKA NDANI YA CCM YENYEWE"

Yangu ni hayo kwa sasa!

Enyi Wavimba Macho wa Kuumwa na "Nyuki" wa "Asali"

Mmepigwa kauli moja tu....mnatapatapa kila kona!

Mvua yenyewe bado inakuja! Hayo ya #Bashiru ni dalili zake tu!

View attachment 2423276View attachment 2423302View attachment 2423304

Nimetumia haki yangu kusema "UKWELI" huu!

Alamsikhi
10101.
Wahuni wa sa100 hao ...
Hofu yao ni kifo cha JPM
 
Kipekee, napenda kumpongeza Dr. Bashiru Ally kwa kuyatoa MAJOKA pangoni, maana kwa kauli moja tu aliyoitoa kukemea MAJANGILI yanayoitafuna Nchi yetu, MAJOKA mengi yamejitokeza huku yakikemea, kulaumu na kukejeli bila kujibu hoja.
 
Bashiru anakosa moral authority ya kukosoa maana yeye ndio muasisi wa kishindo cha awamu ya gwalla yaani ilikuwa ni kero hata kuangalia runinga ya taifa sababu ilizidi sasa ni kama tulikuwa ni fascist state aisee, atulie sasa zama zake zilipita ama asubirie enzi zake zirejee.

Hata u KMK aliupata kimchongo na yeye anafahamu hilo.
 
We jamaa nimekudharau saana, unaonekana unateseka sana na umasikini sasa hasira zako zimehamia kwa watu wengine! mkuu pambana tafuta maisha majungu hayawez kukufikisha popote!
 
Sisi tutasimama na Dr Bashiru Mwanzo Mwisho !!

Tanzania inahitaji Akina Bashiru wakutosha

Achaneni na Hawa wapinzan uchwara na WanaCCM machawa ,mafisadi
Kaka Tanzania Hakuna upinzani. Vipo vyama maslaitu. Wewe umeona machungu yote tunayopitia watanzania umeona chama gani kinapaza sauti? Wamevimbiwa na Asali.

Magufuli Alisha washtukia kwamba ni wahunitu.


Naamini upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM ndio hawa wazalendo wachache kama dkt kakurwa wataibuka na kuwasemea wanyonge.
 
Back
Top Bottom