Arusha yarindima kwa risasi! Jambazi laua polisi

Hawa polisi sijui kwanini hawajifunzi kuwa makini wanapoenda kufanya 'raid'. Mimi nakumbuka nilishawahi kumtishia polisi mmoja na bastola ya toy, yaani alitoka nduki huyo utasema mwanamke anakimbia wabakaji.

Hawa polisi wetu, wanaweza kudhibiti waandamaji na sio majambazi
 
Hizi taarifa naomba ziwekwe vizuri jamani mbona hazieleweki vile. Tunataka tuzipate kikamilifu kwani nasikia OCD amepigwa risasi ya bega na polisi mwingine kauwawa sina hakika which is which

Mkuu soma hapo juu nimejaribu kupachika taarifa za awali nilizozipata kutoka chanzo cha kuaminika.
 
Askari aliyeuawa ni wa upelelezi anaitwa Kijanda Mwandu na ni wa siku nyingi kidogo Arusha na kipindi cha siku za karibuni alikuwa anafanyia kazi kwenye ofisi ya OC CID wakishirikiana na mwenzake Renatus kupangilia kesi mbalimbali za ki uchunguzi. R.I.P Kijanda.

Derimto najua uko well informed je unaweza kutupa details kidogo kwani kila mtu anatoa habari zake. ni kweli OCD amejeruhiwa begani au ni askari mwingine. Na ni kweli huyu jambazi ametoroka na familia yake au uzushi n ni eneo gani tukio limetokea hapa arusha kwani mimi nipo hapa mjini karibu na AICC sipati picha.
 
polisi wetu wamezoea kupiga waandamanaji je ingetokea kama huko columbia majambazi wanakuja ful vifaru,mizinga,longgun,helcopta na briged nzima?
 
Tatizo la polisi wa TZ wanafanya zaidi mambo ya kisiasa kuliko yale majukumu yao ya msingi. sasa huyo jamaa yuko peke yake akua polsi , je wangekuwa 10 si wangefunga central police station na OCD na OC CID? ushauri wa bure, polisi jifunzeni kazi acheni kujifunza kutumia washawasha
 
Arusha imetikiswa na mrindimo ya Risasi eneo la Bara bara mpya kuelekea Tangeru baada ya daraja la nduruma, baada ya polisi kuvamia nyumba moja ili kulishikilia jambazi sugu, inasemekana kuwa baada ya kuzunguka nyumba yake jambazi huyo alitoka na kupiga risasi hewani na kumuuwa polisi moja na mwingine kujeruhiwa vibaya... habari kamili tutawaletea baadae

Nawasilisha

kuwa makini na utoaji wako wa taarifa mkuu. How come ''jambazi amepiga RISASI HEWANI '' na KUUA askari? Agh, huu uzi ni takangumu!
 
tatizo hapa hatuna kikosi maalumu cha uvamizi ambacho kinakuwa na vifaa kamili kama marekani kinaitwa SWAT. Polisi wetu ni legelege wamebakia kuwakamata wanasiasa ambao hawana silaha yoyote
 
Hawa polisi sijui kwanini hawajifunzi kuwa makini wanapoenda kufanya 'raid'. Mimi nakumbuka nilishawahi kumtishia polisi mmoja na bastola ya toy, yaani alitoka nduki huyo utasema mwanamke anakimbia wabakaji.

Na hilo nalo la kujisifu? ama kweli.
 
tatizo hapa hatuna kikosi maalumu cha uvamizi ambacho kinakuwa na vifaa kamili kama marekani kinaitwa SWAT. Polisi wetu ni legelege wamebakia kuwakamata wanasiasa ambao hawana silaha yoyote

Hili ni tatizo la kimfumo tusiwalaumu polisi kama binadamu. Hapa hapa JF kuna kilaza kaanzisha uzi akiuliza kama kuna mtua anajua Ukiwa na degree, diploma na cheti unapata cheo gani kwenye jeshi la polisi. Kama watu wanaenda kuingia jeshini kwa dira ya mishahara na vyeo bila kufikiri majukumu kama mtumishi wa umma kwa kazi hiyo unategemea nini? Sasa hii ndio namna yetu ya kuajiriana, haijalishi background ya mtu wala potentials zake, what matters ni kiasi gani analipwa, KUNA NINI HAPO?
 
Nimeongea na chanzo kutoka ndani ya polisi,ni kwamba aliyepigwa risasi ya bega ni OC:CID Faustine,na sasa yupo Hospital,askari mwingine ameuwawa baada ya kupigwa risasi ya shingoni,na jambazi kukimbia,hadi sasa jambazi hajapatikana
 
Back
Top Bottom