Sura 33:50
Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako ulio wapa mahari yao, na ulio wamiliki kwa mkono wako wa kulia katika alio kupa Mwenyezi Mungu,
na mabinti ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama yako walio hama pamoja nawe; na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwa Nabii, kama mwenyewe Nabii akitaka kumwoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Sisi tunajua tuliyo wafaridhia wao katika wake zao na wanawake ilio wamiliki mikono yao ya kulia. Ili isiwe dhiki kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Mambo ya walawi 18
Na Yehova akaendelea kusema na Musa, na kumwambia: [SUP]
2[/SUP] "Sema na wana wa Israeli, nawe utawaambia, ‘Mimi ni Yehova Mungu wenu.
+ [SUP]
3[/SUP] Jinsi inavyofanya nchi ya Misri ambamo mlikaa, msifanye;
+ na jinsi inavyofanya nchi ya Kanaani, ambamo nitawaleta, msifanye;
+ na katika sheria zao msitembee. [SUP]
4[/SUP] Maamuzi yangu ya hukumu
+ mtayatenda, na sheria
+ zangu mtazishika ili kutembea katika hizo.
+ Mimi ni Yehova Mungu wenu. [SUP]
5[/SUP] Nanyi mtazishika sheria zangu na maamuzi yangu ya hukumu, ambazo ikiwa mtu atazifanya, yeye pia ataishi kwa hizo.
+ Mimi ni Yehova.
+ [SUP]
6[/SUP]
"‘Yeyote kati yenu asimkaribie mtu yeyote wa jamaa yake, wa kimwili, wa karibu ili kufunua uchi.+ Mimi ni Yehova. [SUP]
7[/SUP] Uchi wa baba yako
+ na uchi wa mama yako usiufunue. Yeye ni mama yako. Usiufunue uchi wake. [SUP]
8[/SUP] "‘Uchi wa mke wa baba yako usiufunue.
+ Ni uchi wa baba yako. [SUP]
9[/SUP] "‘Nao uchi wa dada yako, binti ya baba yako au binti ya mama yako, awe amezaliwa katika nyumba hiyo hiyo au amezaliwa nje, usiufunue uchi wao.
+ [SUP]
10[/SUP] "‘Nao uchi wa binti ya mwana wako au binti ya binti yako, usiufunue uchi wao, kwa sababu wao ni uchi wako. [SUP]
11[/SUP] "‘Nao uchi wa binti ya mke wa baba yako, uzao wa baba yako, kwa kuwa yeye ni dada yako, usiufunue uchi wake. [SUP]
12[/SUP] "‘Uchi wa dada ya baba yako usiufunue. Yeye ana uhusiano wa damu na baba yako.
+ [SUP]
13[/SUP] "‘Uchi wa dada ya mama yako usiufunue, kwa sababu yeye ana uhusiano wa damu na mama yako. [SUP]
14[/SUP] "‘Uchi wa ndugu ya baba yako usiufunue. Usimkaribie mke wake. Yeye ni shangazi yako.
+ [SUP]
15[/SUP] "‘Uchi wa binti-mkwe
+ wako usiufunue. Yeye ni mke wa mwana wako. Usiufunue uchi wake. [SUP]
16[/SUP] "‘Uchi wa mke wa ndugu yako
+ usiufunue. Ni uchi wa ndugu yako. [SUP]
17[/SUP] "‘Uchi wa mwanamke na binti yake usiufunue.
+ Binti ya mwana wake na binti ya binti yake usimchukue ili kuufunua uchi wake. Wao wana uhusiano wa damu. Ni mwenendo mpotovu.
+ [SUP]
18[/SUP] "‘Nawe usimchukue mwanamke pamoja na dada yake awe mshindani
+ ili kuufunua uchi wake, yaani, pamoja naye akiwa angali hai.