MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,330
Mkoa wa Arusha waandamwa na mabomu.
Habari zilizotufikia punde kutoka mkoani Arusha zinasema kuwa viongozi wawili wa dini ya kiislamu mkoani humo, wamejeruhiwa kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na wamelazwa katika Hospitali ya mkoa huo, Mount Meru asubuhi hii.
Tunafuatilia zaidi kupata taarifa
=======
Kutoka Arusha taarifa ambayo imetangazwa kupitia Leo tena ambayo imetolewa kama breaking news ni kuhusu Sheikh wa msikiti wa Qiblatan, Sood Ally Sood (37) uliopo eneo la Kilombero jijini Arusha kulipuliwa na bomu la kurushwa kwa mkono nyumbani kwake wakati akila daku na kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imedaiwa kuwa Sheikh huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbali ikiwemo miguu yake yote miwili sehemu za mapajani pamoja na Kifuani na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.
Mbali na Sheikh huyo pia kuna mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) ambaye ni mkazi wa Dar es salaam naye amejeruhiwa na wote wamelazwa katika hospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya matibabu.
==========

TAFRANI kubwa imeukumba mtaa wa Majengo jijini Arusha, baada kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kulipuka kwa kishindo na kuwajeruhi wawili akiwamo Ustadh mmoja na mgeni wake kutoka Nairobi nchini Kenya, FikraPevu imefahamishwa. Tukio hilo lililotokea usiku wa Alhamisi Julai 3, 2014 na kuthibitishwa na polisi limeibua tahauki kwa wakazi wa Arusha na kusababisha waumini wa dini ya Kiislamu kushindwa kufanya ibada ya salanya Alfajiri leo Ijumaa.
Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas, ameiambia FikraPevu Julai 4, 2014 tukio hilo lilitokea jana saa 11:15 usiku nyumbani kwa, Ustadhi Sudi Ali Suli, wakati wakila daku na mgeni wake kutoka Nairobi nchini Kenya, Mhaji Hussein.
Wakiongea na FikraPevu baadhi ya wananchi katika eneo hilo wamesema baada ya kupata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo waliingiwa na hofu na kuwafanya baadhi yao kushindwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya swala ya alfajiri. Kamanda Sabas alisema Ustadh Sudi na mgeni wake aliyefikia nyumbani kwake walijeruhiwa katika tukio hilo.
"Wakati bado wakiendelea kupata chakula walisikia kishindo kikubwa ambacho kilipasua kiyoo cha dirisha na bomu hilo likarushwa ndani na kusababisha mlipuko mkubwa uliowajeruhi miguuni lakini kwa bahati nzuri hakujatokea kifo katika tukio hili," alisema Sabas.
Amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa bomu hilo limetengenezewa kiwandani, na kuwa mtu aliyetekeleza tukio hilo alikimbilia kusiko julikana usiku huo baada ya kulitupa ndani ya nyumba hiyo na kuwa majeruhi wamejeruhiwa vibaya sehemu za miguu.
Amesema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuweza kubaini kama kuna kundi la watu au mtu mmoja aliyehusika na kuwa majeruhi hao wanapata matibabu katika Hospitali ya mkoa huo ya Mount Meru.
Watatu wauwawa kwa kupigwa risasi
Wakati huo huo katika tukio jingine majambazi watatu wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya majibizano na Askari wa jeshi hilo waliokuwa wakiwadhibiti kwa kutaka kufanya uhalifu.
Sabas, amesema kuwa majambazi hao walikamatwa katika eneo la Unga limitedi Relini jijini humo, ambapo baada ya majambazi hao kugundua kuwa wanafuatiliwa na polisi walianza kuwashambulia polisi kwa risasi na polisi nao wakajibu mapigo.
"Tukio hili lilitokea jana Julai 3, 2014 saa 10:20jioni, na hawa majambazi walikua na gari aina ya Toyota Corola yenye namba T 762 CWE pia katika majibizano hayo ya risasi majambazi watatu waliuawa na tayari wamepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya mkoa ya Mount Meru, watu hao bado hawajatambuliwa rasmi" alikaririwa Sabaa.
Amesema majambazi hao wamekutwa na bunduki aina ya Shoot Gun yenye namba A947514 (Pump action) iliyotengenezewa nchini Marekani ikiwa na risasi 3 na ganda moja, ambapo amesema inadaiwa walipanga njama ya kuiba katika duka linalouzaji vigae la Arusha Islamic Center.