Arusha: Wananchi walia na ushuru mkubwa wa Taka

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,850
15,266
Wananchi mkoani hapa wamekuwa wakilalamika ushuru wa kiasi cha sh. elf mbili kwa mwezi wanaotozwa kwa ajili ya taka kwa madai kuwa ushuru huo ni mkubwa tofauti na taka wanazozalisha majumbani.

Baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa kwa maisha ya kawaida wanakoishi majumbani wengi hawazalishi taka nyingi kiasi Cha kutozwa sh. Elfu mbili kila mwezi hivyo imekuwa mzigo kwao kwani wamekuwa wakilalamika kila wakati lakini hakuna utatuzi wa jambo hilo.

Halmashauri ya jiji la Arusha imekuwa ikitoza she elfu mbili kwa mwezi kwa kila kaya na sh. Elf tano kwa mwezi kwa kila duka kwa ajili ya uzoaji taka.
 
Waambie waache upuuzi, 2000 bado ndogo sana, kuhudumia hilo gari na kulipa wafanyakazi sio rahisi hivo.
Binafsi Nadhani ili majiji yawe safi itozwe 5000 hutaki rudi kijijini
 
Wananchi mkoani hapa wamekuwa wakilalamika ushuru wa kiasi cha sh. elf mbili kwa mwezi wanaotozwa kwa ajili ya taka kwa madai kuwa ushuru huo ni mkubwa tofauti na taka wanazozalisha majumbani.

Baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa kwa maisha ya kawaida wanakoishi majumbani wengi hawazalishi taka nyingi kiasi Cha kutozwa sh. Elfu mbili kila mwezi hivyo imekuwa mzigo kwao kwani wamekuwa wakilalamika kila wakati lakini hakuna utatuzi wa jambo hilo.

Halmashauri ya jiji la Arusha imekuwa ikitoza she elfu mbili kwa mwezi kwa kila kaya na sh. Elf tano kwa mwezi kwa kila duka kwa ajili ya uzoaji taka.
lipa ada, tii sheria bila shurti kumbuka kutokulipa ada ya usafi faini ni 50,000/= au jela miezi 6 au vyote kwa pamoja kupitia mahakama ya jiji. kumbuka kuweka mazingira safi.
 
Back
Top Bottom