Ndugu yangu,
Si mara zote kwamba kutokea kwa variations kunatokana na kwamba mizani ni mbovu; la hasha! System yenyewe ya upimaji ndiyo mara nyingi huleta variations. Kinachotokea ni kwamba, kama Load Limit ni 56 tonnes (as per Tanzania); hiyo 56 tonnes inakuwa equally distributed kwenye number of axles. Maana yake ni kwamba, ikiwa gari ina 7 axles, hapo maana yake ni kwamba wakati wa kupima hakuna axle inayotakiwa kuzidi 8 tonnes! Sasa ikiwa huko barabarani mlikuwa mnafukuzana to the point mzigo ukaegemea upande mmoja; then it's obvious kule ambako mzigo utaegemea axle weight itazidi hata kama hapo kabla ilikuwa sawa! Kwahiyo wanaposema kuna variation not necessarily kwamba mizani huwa zinakuwa mbovu; no! Lakini hata hivyo, hivyo ndivyo inavyofanyika katika kila nchi duniani....axle weight considered na hakuna suala la +5%!! But all in all, tusisahau kwamba variation kwenye measurement si jambo la ajabu hata kidogo. Ukitoka filling station A na kuweka lita 10 kisha ukaenda station B, it's more likely kutakuwa na variation tu!
Lakini ukija upande mwingine, Tanzania ni miongoni mwa nchi duniani amako maximum load weight ni kubwa sana; yaani hiyo 56 tonnes! Nchi zingine za East African Community ilibidi mwaka jana zibadilishe viwango vyao ili kuendana na hivi vya Tanzania ili kuweza pia ku-facilitate transportation. Before that, Tanzania ilikuwa ndo nchi pekee inayoruhusu uzito mkubwa; coz' Uganda na Burundi wao; and i think na Rwanda ilikuwa 53 tonnes wakati Kenya ilikuwa only 48 tonnes ambazo hata hivyo walisema wasingebadilisha hadi 2015. TANROAD ya Kenya, KeNHA washapelekwa sana Mahakamani na kusababisha migomo ya malori mara kadhaa, lakini waliendelea kukomaa coz' wanafahamu wanachojali wafanyabiashara ni faida tu na si vinginevyo!
Kwa bahati mzuri, wafanyabiashara wa Tanzania wakacheza na akili za Watanzania na watu wakawa upande wao bila kufahamu kwamba ilikuwa ni ghiriba tu.