Arusha Vs Moshi Town

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
538
shalom ndugu zangu wote wanaJF pamoja na techinical team yote ya JF, napenda kutanguliza pongezi zangu nyingi kwa kazi ngumu mliokua mnaifanya kwa kipindi chote hicho, infact u deserve lots of congrats for what u did.

back to my topic:

Nimeona haitakua mbaya nikianza na hii thread kwenye hii system mpya.

siku si nyingi nilikua arusha lakini kuna kitu ambacho sijakifurahia kabisa kwa sababu sikutarajia mji ambao unajina kubwa namna hiyo duniani kwote kuwa mji mchafu kiasi kile, mji hauna barabara za kueleweka, kama zipo ni nyembamba mbaya zaidi hapohapo watu wanafanya biashara chini kwenye matope kama vile hamna serikali kabisa. Kwa kweli nilishindwa kuelewa kwanini mji unaojulikana kama geneva of africa unakua vile, mji unabiashara nyingi zinazoingiza hela kibao pale lakini hamna kitu chochote.

kitu kingine nachoshindwa kuelewa ni kuhusu ukimya wa manispaa, je hawaoni zile barabara? na je kuhusu sheria ndogondogo za mji hazipo??

je hamna kitu cha kujifunza kutoka mji jirani wa moshi?? ukizingatia mji kama ule unatembelewa na wageni mashuhuri kibao sasa wanandoka na picha gani??
 
Zion my dear usemayo ni kweli tupu
Arusha ni chafu kuliko mtu unavoweza kuamini
its a beautiful place if only it could have been kept well
kama usemavyo, barabara hovyo, takataka ovyo ovyo tu
wasipoangalia watakuwa kama Dar.....
 
jamani sehemu kama hiyo inakuwa chafu tena mikutano yote ya kimataifa inakuwa huko ..utalii unapita mitaa hiyo kulikoni?
 
Tatizo wenye dhamana ya kutekeleza hayo majukumu fikra zao zote zipo kwenye ULAJI tuuu
 
jamani sehemu kama hiyo inakuwa chafu tena mikutano yote ya kimataifa inakuwa huko ..utalii unapita mitaa hiyo kulikoni?

we acha tu..kimbembe kinakujaga pale kukiwa na mikutano na mkuu wa nchi ndio host mbona tunajiju na hayo mafoleni ya kupita vichochoroni...mweee
 
we acha tu..kimbembe kinakujaga pale kukiwa na mikutano na mkuu wa nchi ndio host mbona tunajiju na hayo mafoleni ya kupita vichochoroni...mweee
hivi wa kwetu, huku kwetu kuna hata mabwana/bibi afya kweli?
jamani kuna maeneo ikinyesha sithubutu hata kupita.....huji ukanyage wapi
frm vinyesi vya watu to vinyesi vya wanyama
taka laini to taka ngumu
all over the place
disgusting.....mji kama huu hta matumizi ya vyoo bado ni msamiati wayiiiiiii!!!
 
Management
Leadership ya Manispaa ya Arusha ina shida kubwa sana, wengi wanaoishi Arusha wana idea na mgogoro uliopo huko!
Kuna aina fulani ya ugomvi wa Wazawa(Waarusha) Vs Wa-kuja katika kuongoza Maniispaa.
Shida kubwa ni kwamba ugomvi huu unakuwa supported bila aibu na Vigogo wakubwa kabisa waliokuwa serikalini siku za nyuma wakajiuzulu!...Wazawa wameshindwa kazi, na akija mtu mwingine, anapigwa vita ya hatari!....Nina mifano ya jamaa zangu kibao ambao wamezalishiwa matatizo kibao na kesi mahakamani, kisa ni wakuja, na wanataka kubadilisha system za uendeshaji!
Kwahiyo, shida ya Arusha inataka jicho la tatu kuiondoa....
 
Juzi wamekuja na suala la kuanzisha Satelite Cities au Towns Matevezi Usa River Arusha wenyewe na mwingine yaaani... Sijui walikuwa wapi...
 
Management
Leadership ya Manispaa ya Arusha ina shida kubwa sana, wengi wanaoishi Arusha wana idea na mgogoro uliopo huko!
Kuna aina fulani ya ugomvi wa Wazawa(Waarusha) Vs Wa-kuja katika kuongoza Maniispaa.
Shida kubwa ni kwamba ugomvi huu unakuwa supported bila aibu na Vigogo wakubwa kabisa waliokuwa serikalini siku za nyuma wakajiuzulu!...Wazawa wameshindwa kazi, na akija mtu mwingine, anapigwa vita ya hatari!....Nina mifano ya jamaa zangu kibao ambao wamezalishiwa matatizo kibao na kesi mahakamani, kisa ni wakuja, na wanataka kubadilisha system za uendeshaji!
Kwahiyo, shida ya Arusha inataka jicho la tatu kuiondoa....
itabidi uisaidie polisi mpwa!......
jeshi letu la polisi linataka watu wa aina yako
njoo kituo cha polisi cha jirani na kwako.
nipo hapa nakuona.........
 
Management
Leadership ya Manispaa ya Arusha ina shida kubwa sana, wengi wanaoishi Arusha wana idea na mgogoro uliopo huko!
Kuna aina fulani ya ugomvi wa Wazawa(Waarusha) Vs Wa-kuja katika kuongoza Maniispaa.
Shida kubwa ni kwamba ugomvi huu unakuwa supported bila aibu na Vigogo wakubwa kabisa waliokuwa serikalini siku za nyuma wakajiuzulu!...Wazawa wameshindwa kazi, na akija mtu mwingine, anapigwa vita ya hatari!....Nina mifano ya jamaa zangu kibao ambao wamezalishiwa matatizo kibao na kesi mahakamani, kisa ni wakuja, na wanataka kubadilisha system za uendeshaji!
Kwahiyo, shida ya Arusha inataka jicho la tatu kuiondoa....

bro u r right hili tatizo la muaru (as in muarusha) na wakutoka mkoa ni sugu
nadhani nimezaliwa na nazeeka sasa likiw halijapatiw aufumbuzi
matokeo yake ndo kama hayo mji wetu sasa unanuka.....upinzani wa kipoyoyo usiokuwa na maslahi yoyote kwa maendeleo ya such a beautiful tourist point. inasikitisha na sijui tunaenda kudumbukia wapi mto themi au........??
 
Ni ufinyu wa fikra za viongozi wetu pamoja na kubebana!!
mf.mkuu wa mkoa pale kwa sasa kashazunguka mikoa karibu na karudishwa
tena kwa hiyo anaona sawa kwani kesho akitoka anaenda kwingine
 
banae mi nachojua ni kuwa watendaji wa umma 95% ni hawajui job description zao, pia hakuna anaekufuata kama hujatimiza wajibu wako, mbele kwa mbele ukistaafu unakula chako anaingia mzee mwenio, and life goes on!
 
wakuu mnachozungumza wote mpo right ingawa kuna mengine mapya tumeyasikia hapa jamvini, mi nachoshindwa kuelewa ni raia wa arusha kukaa kimya juu ya hili swala huku mkijua kabisa kuwa mkoa wenu unakusanya kodi nyingi kutoka kwenye makampuni kibao yaliopo hapo mjini, hizo barabara zinaonekana kabisa hazijatengenezwa mda mrefu kupita kiasi, na kuhusu hao manispaa kutofanya kazi je ni nani muhusika wa kuwakosoa?? serikali inapokaa kimya raia ndo wakuiamisha na sio wote kukaa kimya....infact mi siwaelewi watu wa arusha kwa huo ukimya. inamaana wanapotoa report za mapato na matumizi raia wanakua wapi?? na je kwenye zile plan/budget za kila mwaka isue za barabara mnaziweka nafasi gani?? na je nikiwauliza kwa miaka mitano hiyo manispaa imefanya nini mtanijibu kitu gani??
 
Back
Top Bottom