Arusha tuliujua Kama mji wa kitalii ila kwa niliyoyaona umekuwa mji wa machinga toka Dar

Mzee Shirimaa

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
1,539
3,440
Arusha tuliujua Kama mji wa kitalii ila kwa niliyoyaona umekuwa mji wa machinga toka Dar.

Nimeingia Arusha Jana jioni Mji umekuwa wa ovyo sana Town Kati kila chocho, barabarani machinga wamejazana tu najiuliza machinga wa Dar mbona Kama ndo wamehamia Arusha? Maana nakumbuka kipindi kile hiace zimepigwa marufuku Jijin Dar wamiliki wote wa vi hiace waliviamishia Moshi na Dar ina onekana na kwa Machinga imekua hvo .

Town pale kuanzia Jogoo house kupanda mpka mianzin na viunga vyake hamna ustarabu kabisa hiace nyingi vi panki ndo usiseme barabara ndogo kwa sababu ya machinga kuvamia sehem za barabara,uendeshaji wa ovyo ovyo ukizubaa mguu huna.

Nilichoka baada kuona watu wanapanga furniture used mjini kabisa pembezoni mwa barabara ,wanapanga ma viti yalichoka, mabati yaliyo oza ukitoka round about pale karbu na pin point kwa juu kidogo geti Dogo la kuingilia Arusha Technical pale ndo biashara za ovyo bila utaratibu zinafanyika.

Kila kitu kikiwa na utaratibu inapendeza kwa hili nililoliona Arusha Operation ya machinga iendelee miji yote watafutiwe sehem zao.
 
Aisee inasikitisha hakuna tena kitu inayoitwa Geneva of Africa kwasababu mabanda mji mzima ile mitaa ya kuvutia mfano kutoka Clock Tower hadi Impala zamani ilikuwa ni kusafi na kupendeza sasahivi mabanda njia nzima au Florida to Mataa ya Mianzini mavitu machakavu yamejaa barabarani inasikitisha lakini kwa tunakoelekea mama atapabadilisha atawapanga tu.
 
... Florida to Mataa ya Mianzini mojawapo ya mitaa ya "kupendeza" Arusha? Labda sijui maana ya kupendeza!
 
Pale karibu ba Kibo Palace pamekuwa uchafu kabisa kwa kisingizioncha soko la madini
 
Gambo akiona hivyo anafurahi sana, lakini siku zao zunahesabika. Hivi nani alijua uzungunguni pale Kibo palace patajaa mama ntilie ?
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom