Arusha- Ukweli mchungu!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Niko hapa Arusha tangu juzi. Nimetembea viunga mbalimbali vya Arusha kuongea na kujionea hali ilivyo hapa. Nimesikia na kuona. Jana, name nilikoswa na mabomu ya machozi pamoja na risasi (za mpira na moto)pale Soweto.

Leo, nilikuwa Mahakamani kushuhudia kufikishwa na kusomewa mashtaka viongozi kadhaa waandamizi wa CHADEMA Taifa pamoja na watu wengineo waliokamatwa jana Soweto.Wamo Mbunge Said Arfi na Mawakili Wasomi Tundu A.M. Lissu na Mustafa Akoonay. Wamesomewa mashtaka tuliyoyazoea. YALE YALE. Kufanya kusanyiko lisilo halali. Nimeacha maombi ya dhamana yakiwasilishwa.

Wana-Arusha wanataka CHADEMA. Wanaishi na kuiamini CHADEMA. Mioyo yao inaongozwa na CHADEMA. CHADEMA inapendwa kwakuwa inahoji,inaahidi,inafanya pamoja na wananchi,inazungumza nao na kushiriki nao kijamii.Wako hivyo. Kwa hapa Arusha, 'chama tawala' ni CHADEMA. Hali hii inakera watawala-CCM. CCM wanajiona wanapuuzwa Arusha. Hawasikilizwi.Hawaheshimiwi. Hawashangiliwi. Hawasindikizwi. CCM inataka 'kutawala' Arusha.Ni jambo linalowezekana.

CCM ifanye mema na kuishi na wanachi wao vile wapendavyo.CHADEMA wanaweza kuzidiwa kwa ukarimu na utekelezaji na usimamiwaji wa Ilani ya CCM tu. Si vinginevyo. Ni dhahiri kuwa wana-Arusha walishachagua Madiwani wao hata kabla ya kuahirishwa uchaguzi kufuatia mlipuko wa bomu pale Kimandolu.Wanawajua na kujulikana. Ni wa CHADEMA.

Siasa safi inatoa nafasi ya kujipanga na kujiuliza kuelekea kujiboresha. CCM yaweza kujipanga,kujiuliza na kujiboresha hata kama hakitapata hata Kata moja ya Arusha. CCM bado ina wanachama wengi tu watiifu hapa Arusha.Iwatumie hao kuimarisha chama hapa. Siasa ina matunda yake. Matunda ya ushindi kwa CCM yaweza kupatikana. Penye nia,pana njia!

Lakini kwa namna ilivyo sasa, CHADEMA waachwe 'watese' katika jiji la Arusha.


Mzee Tupatupa (kwasasa Arusha)
 
Waingereza wanasema usiku unakuwa na giza nene sana muda mfupi kabla ya kupambazuka. Tuzidishe uvumilivu kidogo tu kwa sababu punde kutapambazuka. VIVA wana Arusha
 
...walitaraji uchaguzi utaahirishwa mpaka baada ya miaka mitatu wakaaibika na mabomu yao...
 
Mkuu VUTA-NKUVUTE umemaliza yote.
Mwenye masikio na asikie!
 
Hahaa, unataka tuamini ulichoandika kwakuwa upo Arusha?? Kuwa Arusha pekee haileti maana yoyote ile....
 
Umeona mbali ukaamua kusema yaliyo mema, bahati mbaya CCM hawaoni huo umbali mnaoona wengine na hata wakiambiwa na wanaoona mbali kuwa upande huu msinde au muende kwa tahadhari wenyewe wamelalia masikio, kwa sasa ndani ya CCM anasikilizwa mtu mmoja tu Nchemba.
 
Hao mACCM hadithi hiyo inawakoroga na kuwasababishia jaziba wako tayari kuua, wako tayari kutesa wananchi aibu moja kubwa wamepata ni wakati walitaka kutumia udini kuwaghiribu wahanga wa mauaji ya polisi familia zimezika upumbavu wa IKULU, Mkuu wa mkoa na Polisi ndivyo mioyo ya wanaarusha ilivyoipokea CHADEMA, hakuna kipande cha thumuni kitakachowageuza.
 
Iringa hapo awali haikuwa na chama cha upinzani wananchi wa kule walikuwa hawaelewi nini maana ya upinzania, walitafsiri upinzania kama vita. Kutokana na umbumbumbu wa wananchi kuhusu vyama vingi CCM ilibweteka ikajisahau na ikaendelea na "Viahadi Feki kama ilivyozoea" Wakati hayo yakiendelea wananchi wakawa wanafunguka taratibu kuelewa dhana ya vyama vingi. CCM ni ZIMWI HATA KULE IRINGA!! CCM ni kama jini mahaba kwa wananchi wa Iringa ambalo kamwe hawataji liingilie ndoa yao na Chadema!!!




CCM ni JINI MAHABA
 
Nina mashaka makubwa na mada yako.Haiwezekani hata siku moja kupenda chama kinachoua wananchi kinaowatawala.Hii itakuwa ni kiini macho.Acha kutudanganya.Hao ccm wakafanye hayo unayoyasema sehemu nyingine na sio Arusha.
 
Huna lolote mnafiki wewe. Tunataka siasa safi. Kwani Arusha peke yake ndio CHADEMA ina nguvu? Mbona Mwanza hatuoni fujo, Mbeya je? Kinacho waharibia Chadema ni ufinyu wa akili wala sio CCM.
 
PHP:
[QUOTE][quote="VUTA-NKUVUTE, post: 6623987"][COLOR=#222222][FONT=Verdana]Niko hapa Arusha tangu juzi. Nimetembea viunga mbalimbalivya Arusha kuongea na kujionea hali ilivyo hapa. Nimesikia na kuona. Jana, name nilikoswa na mabomu ya machozi pamoja na risasi (za mpira na moto)pale Soweto.[/FONT][/COLOR]

[COLOR=#222222][FONT=Verdana]Leo, nilikuwa Mahakamani kushuhudia kufikishwa na kusomewa mashtaka viongozi kadhaa waandamizi wa CHADEMA Taifa pamoja na watu wengineo waliokamatwa jana Soweto.Wamo Mbunge Said Arfi na Mawakili Wasomi Tundu A.M. Lissu na Mustafa Akoonay.Wamesomewa mashtaka tuliyoyazoea. YALE YALE. Kufanya kusanyiko lisilo halali. Nimeachamaombi ya dhamana yakiwasilishwa.[/FONT][/COLOR]

[COLOR=#222222][FONT=Verdana]Wana-Arusha wanataka CHADEMA. Wanaishi na kuiamini CHADEMA. Mioyo yao inaongozwa na CHADEMA. CHADEMA inapendwa kwakuwa inahoji,inaahidi,inafanya pamoja na wananchi,inazungumza nao na kushiriki nao kijamii.Wako hivyo. Kwa hapa Arusha, 'chama tawala'  ni CHADEMA. Hali hii inakera watawala-CCM. CCM wanajiona wanapuuzwa Arusha. Hawasikilizwi.Hawaheshimiwi. Hawashangiliwi. Hawasindikizwi. CCM inataka 'kutawala' Arusha.Ni jambo linalowezekana. [/FONT][/COLOR]

[COLOR=#222222][FONT=Verdana]CCM ifanye mema na kuishi na wanachi wao vile wapendavyo.CHADEMA wanaweza kuzidiwa kwa ukarimu na utekelezaji na usimamiwaji wa Ilani ya CCM tu. Si vinginevyo. Ni dhahiri kuwa wana-Arusha walishachagua Madiwani waohata kabla ya kuahirishwa uchaguzi kufuatia mlipuko wa bomu pale Kimandolu.Wanawajua na kujulikana. Ni wa CHADEMA. [/FONT][/COLOR]

[COLOR=#222222][FONT=Verdana]Siasa safi inatoa nafasi ya kujipanga na kujiuliza kuelekea kujiboresha. CCM yaweza kujipanga,kujiuliza na kujiboresha hata kama hakitapatahata Kata moja ya Arusha. CCM bado ina wanachama wengi tu watiifu hapa Arusha.Iwatumie hao kuimarisha chama hapa. Siasa ina matunda yake. Matunda ya ushindi kwa CCM yaweza kupatikana. Penye nia,pana njia![/FONT][/COLOR]

[COLOR=#222222][FONT=Verdana]Lakini kwa namna ilivyo sasa, CHADEMA waachwe 'watese'Arusha.[/FONT][/COLOR]

[B][COLOR=#222222][FONT=Verdana]Mzee Tupatupa (kwasasa Arusha) [/FONT][/COLOR][/B]
 
[B]Vuta Nikuvute [/B]CCm sikio la kufa
 
Hata kwetu Mbeya Chadema ni chaguo la wana Mbeya, unaweza kutembea umbali mrefu bila kuona bendera za kada wa CCM, watu wanaishi chadema wanawaza chadema ndio maisha yetu, Naamini hali iko hivyo mikoa mingi isipokuwa hii michache: Lindi, Tanga, Dsm, Singida, Dodoma kwani still haijashuhudiwa mwamko mkubwa. Naamini kabla sijafa nitaiona serikali yetu ya Tanganyika ikirejea usiku huo naamini sitolala nitaimba na kumshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto zangu. I always fantasize Tanganyika!
 
Nina mashaka makubwa na mada yako.Haiwezekani hata siku moja kupenda chama kinachoua wananchi kinaowatawala.Hii itakuwa ni kiini macho.Acha kutudanganya.Hao ccm wakafanye hayo unayoyasema sehemu nyingine na sio Arusha.
Hata aibu huna!
 
Kwanini CCM wanalazimisha Arusha? Hivi huku Mwanza tujiandae, maana hii manispaa inaonekana hivyo. kwani Mzeee TUPATUPA, 2015, tutalipuliwa kila mkoa wenye wapenzi wa CHADEMA? Maana ndo tuanze kujiandaa!!

SP
 
Mzee Vuta-Nikuvute hakika umewapatia ukweli lakini jamaa zako walivyo wabishi hawakubaliani na ukweli huu wametia masikio yao NTA hawasikii, machoni wamevaa miwani ya mbao hawaoni. Mfano ni huyu hapa angalia hiki kinyesi alichoandika hapo chini.


hahaa, unataka tuamini ulichoandika kwakua upo arusha?? kua Arusha pekee haileti maana yoyote ile....
 
Huna lolote mnafiki wewe. Tunataka siasa safi. Kwani Arusha peke yake ndio cdm inanguvu? Mbona mwanza hatuoni fujo, mbeya je? Kinacho waharibia cdm ni ufinyu wa akili wala sio CCM.

Bwa'mdogo tulia. Acha kiherehere kama kuku anayetaka kutaga. Sehemu zote ambako CDM imeshinda (hususan hizo ulizotaja) kuna mvutano kati ya CDM na hayo majambazi yanayojiita watawala. Tofauti ni kiwango tu.
 
Kukubali kuielewa na kuikubali historia ya arusha kutaifanya ccm pia kukubalika arusha,japo kwa taratibu mno,Mbunge wa mwisho wa halali kutoka ccm hapo arusha alikuwa ni Kanali kinana,tokea hapo ccm haikuwahi kuwa na mbunge aliyechaguliwa kihalali arusha,anguko la ccm arusha halikuanza awamu hii ya chadema kama ma whistle blower wao wanavyodhani,wala wana arusha si tu waumini wa chadema kama inavyofikirika,bali ni wapenda mabadiliko,mabomu ya machozi na risasi za moto hazijaanza wala kuletwa na chadema,mabomu yalipigwa kwenye mkutano wa Augustine mrema akiwa nccr,yalipigwa akiwa Tlp,mabomu na risasi vilirindima kipindi cha uchaguzi uliompa mh Malla ubunge ulioporwa baaadaye na ccm,Mh lema alipogombea kupitia Tlp pia mabomu yalihusika,naweza sema nimeyajua mabomu kabla y kuijua Chadema,Nikiwa kijana mdogo 18- nilipewa dili na ccm la kuwakusanya vijana wakamata nyoka,ili kwenda kuvuruga mikutano ya mrema(Augustine)walichokifanya vijana wale ni kudondosha nyoka katikati ya mkutano na kisha kupiga kelele kuwashtua watu ili wasi concentrate na mkutano,Arusha haikuwahi kurudi nyuma kwenye field ya mabadiliko,Tatizo la ccm ni kujilazimisha na kulazimisha dunia iamini kwamba Chadema ndiyo tatizo,they are in the wrong track,wakitaka kweli kulielewa tatizo la arusha wasifupishe upeo,waangalie mbali zaidi ya miaka kumi iliyopita,na wataona michirizi ya tatizo ilipotokea,na huko wanaweza kulibaini tatizo,tena ndani yao wenyewe.
 
Back
Top Bottom