Kwa hiyo lema alikuwa anavunja amani kwa mawazo yake?.
THE UNSEEN IS ILLUSTRATED BY THE SEEN.
Jamani pamoja na yote yaliyosemwa kwa hili tusipotoshe umma, nimesoma vyema hotuba yake ya leo na sijaona sehmu ambayo kikwete amebainsha aliyoyatoa mtoa mada. Tupingane lakini isifike wakati wa kuleta yale ambayo hayapo. Hebu someni hotuba yake kwanza ndiyo u-comment. sawa sisi ni wapinzani wake na chama chake cha magamba lakini isifikie hatua hii.
Jk kweli ana vituko vurugu za arusha chanzo ni yeye na ccm yake anafikiri tumesahau anachotakiwa kufanya ni kuwaomba msamaha watu wa arusha na Mheshimiwa Lema kwani siku zao kutawala Tz zina hesabika
Nilishasema na narudia kusema tena kuwa "Peace should never mean ONLY the absence of Guns and Bomb Blasts" It is more than that. Watu wako kimya lakini mioyoni mwao kuna kelele balaa. Mwambieni aende Arusha kuhutubia hadhara aone kama watu wa kumsikiliza hawatasombwa kwa malori kutoka vijijini!!!!!
matatizo ya kusoma kwa kuruka ruka yanakusumbua...hebu soma hapa chini
Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
Power of SISIMWEWE? Come on........... you can't be serious!!!!!!ZINDUKA! You are underestimating the power of CCM!