Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Shehena ya Madini ya Tanzanite yenye uzito mkubwa imenaswa katika hotel ya Pallson ya jijini Arusha Mara baada ya maofisa wa Madini wakiwa wameambatana na askari polisi wenye silaha za moto wamevamia hotel hiyo na kufanikiwa kukamata Madini hayo yaliyokuwa yamefishwa kinyume cha sheria.
Maofisa hao wa Madini ambao hawakuwa tayari kutoa ufafanuzi walivamia katika hotel hiyo majira ya saa mbili usiku wa leo katika operesheni inayoendelea ya kutafuta Madini yaliyofishwa majumbani kwa wafanyabiashara wa Madini na kufanikiwa kukamata Madini hayo.
Hata hivyo baadhi ya wamiliki wa hotel hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu Mollel alimaarufu askofu wamedai kuwa Madini hayo sio Mali yao Bali yalikuwa Mali ya marehemu askofu ambaye alikuwa mfanyabiashara wa Madini .
Polisi waliondoka na baadhi ya wahusika wa hotel hiyo wakiwemo wahudumu kwa ajili ya mahojiano na kwenda kuthaminisha thamani ya Madini hayo .
Baadhi ya wafanyabiashara mkoani hapa wamekuwa wakipekuliwa majumbani mwao kusaka Madini hayo Mara baada ya kubainika kuwa baadhi yao wameficha Madini hayo majumbani mwao kinyume cha sheria.
.