ARUSHA: Polisi yanasa shehena ya Madini ya Tanzanite katika hotel ya Askofu

jembejembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Messages
462
Points
1,000

jembejembe

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2016
462 1,000
Shehena ya Madini ya Tanzanite yenye uzito mkubwa imenaswa katika hotel ya Pallson ya jijini Arusha Mara baada ya maofisa wa Madini wakiwa wameambatana na askari polisi wenye silaha za moto wamevamia hotel hiyo na kufanikiwa kukamata Madini hayo yaliyokuwa yamefishwa kinyume cha sheria.

Maofisa hao wa Madini ambao hawakuwa tayari kutoa ufafanuzi walivamia katika hotel hiyo majira ya saa mbili usiku wa leo katika operesheni inayoendelea ya kutafuta Madini yaliyofishwa majumbani kwa wafanyabiashara wa Madini na kufanikiwa kukamata Madini hayo.

Hata hivyo baadhi ya wamiliki wa hotel hiyo iliyokuwa ikimilikiwa na marehemu Mollel alimaarufu askofu wamedai kuwa Madini hayo sio Mali yao Bali yalikuwa Mali ya marehemu askofu ambaye alikuwa mfanyabiashara wa Madini .

Polisi waliondoka na baadhi ya wahusika wa hotel hiyo wakiwemo wahudumu kwa ajili ya mahojiano na kwenda kuthaminisha thamani ya Madini hayo .

Baadhi ya wafanyabiashara mkoani hapa wamekuwa wakipekuliwa majumbani mwao kusaka Madini hayo Mara baada ya kubainika kuwa baadhi yao wameficha Madini hayo majumbani mwao kinyume cha sheria.
.
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2009
Messages
16,460
Points
2,000

BONGOLALA

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2009
16,460 2,000
Hivi ukichimba madini na ukapata ni lazima uuze saa Hiyo hiyo au?na nikipata natakiwa ni report mahali au niyaweke wapi wakati nasubiri kuyauza?

Mbona mazao watu wanaweka stock majumbani siku bei nzuri ndiyo wanapeleka sokoni?

Usishangae ukasikia madini hayo yameyeyka huko polisi maana hata mwenye mali Askofu alishafariki.

Awamu hii ni kudhulumu tuu mali za watu.

Mabureau de change mara nyumba watu walizonunua nhc korosho na hii ya madini
 

Lavan Island

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2015
Messages
1,874
Points
2,000

Lavan Island

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2015
1,874 2,000
Majitu majinga hayoo peleka ndani uhujumu uchumi unaiba madini halafu unaficha ndani, wakati nairobi ukienda unauza faster tu na boda ya namanga ndio chocho la kuvushia ki ulaini mlishinwaje kuyauza umbwa nyie kwenda jela tu.
 

Kesaboso

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2019
Messages
263
Points
250

Kesaboso

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2019
263 250
Wanaficha madini? Kivipi yaan

Kwahiyo kama madini ni yangu niyapeleke wapi kwa mfano?

Shwain
Ukitaka kuyatunza kwanza kalipie kodi kisha tunza hakuna shida, tatizo ukayatunze bila kodi ndo yakikutwa huna lisiti ya kodi imekula kwako, wanasema ndo mwanzo.wa kuyatorosha bila kodi.
 

Forum statistics

Threads 1,380,969
Members 525,922
Posts 33,784,785
Top