Arusha na silaha

jamani arusha ni kitu nyingine kama unafikiri natania njoo arusha unywe bia zako ulete za ki darisalame uone maneno yako.

kule bwana hawatanii,nilishuhudia moja pale sakina jamaa waliingia kuchukua mauzo kwenye super market palikuwa hapatoshi.
wazee wa kazi walipopiga zao kumbe machalii nao wanazo.
dar ukipiga simu polisi wanakuja baada ya saa moja arusha polisi mpaka wahakikishe zimetulia wanaongeza masaa mawili ndipo wanakuja.

nakumbuka sana huo wizi mkuu ilikuwa balaa wezi walifunga mtaa mzima.
 
Jamani huku Arusha karibu kila kijana mwenye maisha mazuri kiasi anamiliki bastola . Sijui kama kuna mkoa watu wanamiliki silaha kama huu . Ni kwanini inakuwa hivi ? Nipe sababu zako.
Mbona kila mmasai ana sime na husemi..,au mbona Rage kule Igunga alipanda na hiyo kitu hukusema..,?tujadili hoja za msingi..,sio za masaburi..!
 
Mbona kila mmasai ana sime na husemi..,au mbona Rage kule Igunga alipanda na hiyo kitu hukusema..,?tujadili hoja za msingi..,sio za masaburi..!

kweli we una matatizo mwili mzima . Unalinganisha bastola na sime ? Unaupungufu wa kitu flani kichwani.
 
Ni dalili ya ushamba. Wameambukizwa na nchi jirani ya Kenya.
Hata sehemu za Starehe utawakuta na Silaha , Bastola au Kisu mfukoni, ni wanaume wasiojiamini.

Asante kwa kunijulisha!!kumbe m2 akimiliki silaha ni dalili za ushamba na kutojiamini?
 
Mimi huwa najiuliza kama unaamini Mungu yupona anakulinda usiku na mchana kwanini unatembea na Bunduki/Bastola kiunoni?
 
arusha wababe ni wengi,ukiwa umelemaa imekula kwako,beto,screwdriver,bastola ni muhimu sana ukitembea ucku,hadi watoto huwa wanabeba uma wakitoka ucku. . .kwj majumbani kuwa na gobore ni jambo la kawaida tu.ukitaka kujua ziko nyingi karibu usherekee mwaka mpya ngaramtoni,utadhan popcorn zinapasuka.arusha ni balaa

mkuu nakumbuka dingi alikuwa anagobore lake analificha darini ikifika mida ya jioni kama saa moja moja hivi basi anaachia mambo hewani kama mara tatu. yote hiyo anakwambia ilikwa ni kufukuza wezi au kuscare away thieves.
basi ilikuwa ikipigwa mitaa yote kimya... arusha ni nomaaa. vijana wa a-tz hatujakaa kimama ukilianzisha tunaparangana shwain....
 
Wakuu naomba kuuliza, bastola ipi ni bomba zaidi kuwa nayo? Nasikia zipo za aina nyingi eg Star, CZ na kadhalika.

Ipi iliyo kiboko zaidi?
 
njoo bwana hamna vita huku . Watu waarusha tunaupendo sana .
Unamdanganya mwenzako,kuwa mwangalifu ukija Arachuga,alafu wageni wengi huwa wana ma'ankra za kutosha kama hizi Aaa!lov it.jpg
 
Hayo ndio maendeleo tunayotaka! Hongera CDM, Hongera WACHAGA!
Maandishi yako yanaashiria 'uchama na ukabila'. Arusha imejaa majambazi ndio maana watu wengi wana silaha za kujihami. Ww unaita hayo ni maendeleo?
 
Wakuu naomba kuuliza, bastola ipi ni bomba zaidi kuwa nayo? Nasikia zipo za aina nyingi eg Star, CZ na kadhalika.

Ipi iliyo kiboko zaidi?

kuna nyingi kiboko sasa sijui utapendelea ipi . Kuna za usa ,cz , ubelgiji , rusia na israel.
 
Back
Top Bottom