Filipo
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 9,347
- 5,553
Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano hadi asubuhi imewasababishi usumbufu wakazi wengi wa jiji hili. Wapo ambao hawakulala wakishindana na maji ya mvua. Yanaingia ndani, wao wanayatoa. Wapo waliolazimika kuchimba miferegi usiku huo, huku wakinyeshewa ili kuyakwepesha maji na nyumba zao.
Wapo waliolazimika kwenda kazini leo kwa usafiri wa umma au miguu yao baada ya barabara kuharibika. Upo usumbufu mwingi umetokea licha ya kwamba mvua waliimiss sana na walikuwa wakiitamani kwa muda mrefu. Binafsi nashukuru Mungu sikuupata na ninawapa pole waliopatwa na maswahibu hayo!