Arusha: Mkuu wa Magereza Godson Mwanagwa akanusha Ole Sabaya kufanya vurugu gerezani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,918
141,883
Mkuu wa magereza mkoani Arusha afande Godson Mwanagwa amekanusha taarifa zilizozagaa mitandaoni kwamba mh Lengai Ole sabaya aligoma kuoga na kufanya vurugu gerezani.

Afande Mwanagwa amesema Ole Sabaya alipokelewa vizuri na hakuna tatizo lolote gerezani.

“Alipokelewa vizuri tu hakuna vurugu zilizotokea, hakuna tukio kama hilo lililotokea huyo unayemtaja aliyetoa taarifa mngemuuliza amezitoa wapi mimi muhusika nakuambia wanaoripoti ni waongo”

Amesema Godson Mwanangwa Mkuu wa magereza mkoa wa Arusha
Screenshot-2021-06-06-at-08.22.51-660x400.jpg

Source: Ayo tv
 
Yupo Kwenye ‘Denial Situation’ Kwamba kumbe Dunia hii ni duara na apandae juu kuna muda atashuka na mtetezi wake kaondolewa na nguvu kubwa maana ilikuwa kama hatumuwezi hawa wengine vi Dagaa wanapondwa na Karma tu na hivi bado vijana ndo walipie na kujutia na labda mbeleni wawe Inspirational/ Motivational Speaker kwamba kwa kila ulitendalo kuna matokeo yake yatakuwa mema ama mabaya na hasa ukimwaga damu za wenziwako na ufirauini kama huo wa kuvunja miji ya watu na kuingilia wenzake bila idhini zao na kupora jasho la watu.

Muda ukienda siyo tu ataoga bali atakuwa anakimbilia hata ugali wa foleni huko gerezani kwa sasa kama haamini kwamba huwa vitu vina geuka atakaa sawa tu muda ni dawa haha.
 
Jamani kule ni dunia ingine kabisa ndani ya dunia hii ya ustaarabu muacheni siku 14 akirejea mtamuona full discipline mpole na anafuata yote atayoambiwa....sasa anazoea mazingira na anri zote kuchuchumaa ndio amri no 1 ukiongea na askari jela atanyooka hamtaamini....heshima zote pale ataliwa hela sana miezi 4 mwanzo ....time will tell
 
Mamaee zake ukimwangalia tu sura lilivyokuwa nyeusi ka kapinduka na gari la kiwi, japo ana umateumate lkn kutokana na roho mbaya yake kashindwa hata kutia rangi,, sasa sikwambii huko mahabusu na kibaridi cha arusha akitoka atakuwa ka buti la mgambo.. jitu likawe lina roho ka shetani, Kwani yeye ndo mtumishi wa kwanza wa serikali kushtakiwa, lkn mbona raia wamemkalia sana kooni. Hii ni kutokana na matendo yake, na kuna mwingine yule aliyekuwa mpambe wa rais nae huko aliko sasa hivi mimavi mbwambwambwa,, bashite
 
Back
Top Bottom