Mzee
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 13,620
- 5,863
Habari za Muda huu
Kila nikiangalia Siasa za Arusha zinaonyesha kiwango cha Ujinga wa Watanzania. Naomba kuuliza
i. Makonda ana vinasaba gani na Mkoa wa Arusha. Hata kama Arusha kila mmoja ana haki ya kugombea, Makonda amekaa Arusha kwa kipindi gani mbali na kuwa Mkuu wa Mkoa
2. Je! katika Uhalisia, kati ya Mbunge na Mkuu wa Mkoa nani ana nafasi nzuri ya kusaidia mchakato wa Maendeleo.
Mkuu wa Mkoa yupo Upande wa Serikali na Serikali ndio inayotoa Fedha ikiwa na maana Mkuu wa Mkoa ana nafasi nzuri ya kutumia Mamlaka kuhamasisha Mchakato wa Maendeleo.
Jambo gani ambalo Makonda kashindwa kulifanya kama mkuu wa Mkoa anadhani akiwa Mbunge atafanikisha??
3. Gambo akiwa mkuu wa mkoa alitifuana na Lema akiwa Mbunge. Mwisho Lema akaondoka akabaki Gambo. Mtifuano ule ambao Gambo alikua anaufanya kwa Lema ukahamia kwa Watumishi. Alitifuana sana na Watumishi.
4. Arusha baada ya kukubali utambulisho wao kuwa "Wadudu" hapo nikajua kuna tatizo kubwa sana. Namna gani mkoa unaweza kubariki kuwa na utambulisho wa Wadudu.
Watu wa Arusha mnapaswa kujitathmini kwa Huu Ujinga.
Wasalam.