Arusha - Mauaji ya kutisha jana tishio kwa wimbi la mageuzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha - Mauaji ya kutisha jana tishio kwa wimbi la mageuzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Apr 22, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Vijana wanne wauawa kikatili Arusha

  • Wote ni waendesha pikipiki
  Mauaji ya kutisha yametokea eneo la Chekereni wilaya ya Arumeru mkoani Arusha ambapo watu wasiojulikana wamewaua vijana wanne waendesha pikipiki kwa kuwanyonga, kisha maiti zao kutupwa maeneo tofauti. Tukio hilo la aina yake limevuta simamanzi kubwa kwa mamia ya wakazi wa jijini hapa ambao walifurika kwenda kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa-Mount Meru.

  Ili kutoa nafasi kwa wananchi kuitambua kwa mara moja, miili ya marehemu iliwekwa nje ya jengo la kuhifadhia maiti huku mojawapo ikiwa imefungwa minyororo mikono yote. Baadhi ya watu waliwatambua vijana hao wanaokadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 35, kwamba walikuwa ni waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda. Hadi kufikia majira ya saa nane hivi, maiti tatu zilikuwa zimetambuliwa na kuhifadhiwa hospitalini hapo wakati mmoja alikuwa hajatambuliwa.


  Maiti zilizotambuliwa hadi muda huo ni zilitajwa kuwa ni za Jumbe Saitobi, Elly Loti na Boshu Maombi. Hata hivyo haikujulikana ni wakazi wa maeneo gani jijini hapa. Maiti hizo hazikuonyesha majereha isipokuwa mikwaruzo kidogo maeneo ya shingo zilizokuwa zimevunjika, hivyo kuashiria huenda walinyongwa. Kamanda wa Pilisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, hakuwepo ofisini na alipopigiwa simu mara kadhaa hakuwa akipokea simu.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  No finally at the end of the day ... we will need a clear and precise details of really what happened ... and not this shallow statements from the Police eti chanzo hakifahmiki, nani hayuko ofisini etc ..!! This is about life Bwana!!!
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
  ukiangalia kwa makini unaweza kugundua kuwa sura za hawa watu zinashabihiana. labda ni ndugu
   
 4. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  So sad!RIP wapendwa.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mungi@, sipati jibu nini kinaendelea Arusha na mazingira ya vifo hivyo, kuna kitu nyuma yake. Lakini ukombozi wa kweli una gharama yake.
   
 6. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Pia kuna ujambazi umefanywa maeneo ya sombetini- Ngusero Arusha.

  Kuna kundi la watu 9 walikuwa wanapita na kuvunja maduka.

  sasa wenye maduka na vijana wa maeneo hayo wakawa na Kikao cha kuanzisha Sungusungu (Ulinzi shirikishi), Akatokea mwenyekiti Wa Kitongoji akasema hakuna cha ulinzi shirikishi hapa, nyie si mnajifanya Peoples power, sasa jilindeni.

  Inasemekana ni Mpango wa chama kimoja kikongwe kilichoshindwa ubungu Arumeru, sasa wanawatisha wananchi.

  Na hii habari ni kwa mujibu wa Radio Sun Rise ya Arusha.
   
 7. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Loh poleni sana wafiwa. Kama mauaji hayo kwa namna yoyote yana mkono wa kisiasa basi ni lazima umma uamke na kuchukua hatua stahiki sasa.

  Poleni sana.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mpaka muda huu watu wanajiuliza maana hawapati picha, ni jinsi gani hawa watu waliuawa, tena kwa kunyongwa kwa kamba shingoni.

  Ninachoamini ni kwamba kama vifo hivi havitokani na usalama wa taifa, wauaji watapatikana kutokana na kwamba marehemu wote wana macho. Macho yao yanaweza kutumika kugundua wauaji kama hawajavaa masks.
  Lakini kama yametokana na kitengo cha usalama itakuwa ngumu kujua wauaji.
  Lens ya macho zitatumika kuwajua wauaji, kwani sura zao huhifadhiwa na lens za macho
   
 9. N

  Njele JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wameshindwa ssa wameamua kuinua majambie, hapo wananchi ndio watawakimbia kabisa kwa vile kubaki magamba si shari tena. Umwagaji wa damu huu utazidi kuwaumbua.
   
 10. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huyo mwenyekiti wa kitongoji alipaswa kuanza kula kipondo palepale ali aitambue vizuri peoples power..Na hii inadhihirisha kuwa kweli CCM kinaelekea kufa..Maana haiingii akilini kuwaza kulikomboa jimbo la Arusha mjini kwa kufanya mauaji ya raia na kupora mali zao.
   
 11. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Jambo hili limetushtua sana tulikuwa tumezoea kuona majambazi yakiuawa namna hii ila leo tunashuhudia watu wetu wema wakiuawa na wahalifu au wa kisiasa au majambazi. Siyo tukio la kutolea maelezo mepesi eti RPC Andengenye hayupo ofisini bali ilitakiwa mpaka sasa suspect wawe wamejaa pale central polisi kwa mahojiano. Polisi hawako serious wao wako barabarani kukamata Fuso amabazo hazihatarishi usalama wa raia ila wahalifu wanaoua watu hawatafutwi.

  Kama ni mauaji ya kisiasa itafahamika siku si nyingi na impact yake itakuwa imeasurable kwani ukweli ni kuwa CDM ni wengi kuliko CCM na kama CCM wameamua kulianzisha inaweza kutokea political cleansing badala ya ethnic cleasning.
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Hawa itakuwa walikuwa mstari wa mbele kkwenye masuala ya kampeni za cdm, so wakawekwa alama. Ulinzi unahitajika visije vikatokea vifo vingine
   
 13. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Duh!Mungu awapumzishe marehemu mahala pema peponi!Arusha hapa katikati ilikuwa imetulia sana kwa matukio ya kikatili naona sasa yameanza kurudi tena kwa kasi!!Mimi sihusishi vifo hivi na mambo ya kisiasa,mauaji ya madereva wa bodaboda yamekuwa yakiripotiwa nchi nzima wala si Arusha peke yake,huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine hasa ukizingatia marehemu hawakuwa na influence yeyote ile kwenye upande wa siasa!!

  Poleni sana wafiwa na mwenyezi mungu awatie nguvu kwenye kipindi hiki kigumu,polisi fanyeni kazi yenu iliwahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria!!
   
 14. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It pains so much......why?...How?....and what is behind this????? Imeniumiza sana......I don't really understanding what to say by the time being. But I believe that every happens for reasons...there is a reason for this....if it's really not due to political matters....we shall know all what happened and the reasons for this...but If...Ohhh God...why????
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Hii ndiyo nchi ambayo ni kisiwa cha amani?
   
 16. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Nimeona imeniuma,cjui pikipiki zimeibwa..intelijensia ya mwema hapo imeshindwa na hao ni wapigakura wa chadema.
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  The big challenge ni kwa jinsi gani wote wameuawa kwa kunyongwa kamba?
  Labda kama walitekwa na kundi kubwa la wauaji, then wakawanyonga kwa zamu.
  In fact haiingii akilini
   
 18. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,460
  Likes Received: 3,715
  Trophy Points: 280
  Toba Mungu tusaidie tuepushe na unyama huu. RIP vijana wa leo
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Vigumu kuamini kauli yako ukizingatia kwamba mauaji hayo yametokea wakati mmoja, ni dalili tosha ni kitu cha kupangwa. Hivyo ningeamini kauli uliyosema kama tukio ni moja au mawili, lakini kufikia idadi ya waendesha pikipiki watano kwa wakati mmoja ni jambo linaloibua maswali mengi.
   
 20. m

  mkizungo JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 247
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanzania taifa langu,,,,,ya nini laana hii,,,,,,,mauaji ya nguvu kazi ya taifa lako mwenyewe,,,,,,,,,,hivi ni kweli ama ninaota,,,,,,,,,,mungu wangu,uyaone machozi yangu unijibu hima,,,,,,vijana hawa nini wamekosa hadi iwapase kifo,,,,damu yao,,uhai wao,,kwa kumfurahisha nani,,,,mbinu gani ilitumika,,,mamlaka gani,,ilisimamia hata wasijitetee,,,,,,,ee mola ujuaye siri hii tufunulie,,tunusuru na taifa la utekaji nyara na mauaji,,,,,,naililia tanzania,,,,,,nawalilia vijana hawa,,,,,,lalen pema pepon,,,,,,burian,mmekufa mkiuhitaji uhai,,mkipingana na umasikini,,,,,,eeemen,,,,,,,
   
Loading...