Arusha - Mauaji ya kutisha jana tishio kwa wimbi la mageuzi?

Mpaka muda huu watu wanajiuliza maana hawapati picha, ni jinsi gani hawa watu waliuawa, tena kwa kunyongwa kwa kamba shingoni.

Ninachoamini ni kwamba kama vifo hivi havitokani na usalama wa taifa, wauaji watapatikana kutokana na kwamba marehemu wote wana macho. Macho yao yanaweza kutumika kugundua wauaji kama hawajavaa masks.
Lakini kama yametokana na kitengo cha usalama itakuwa ngumu kujua wauaji.
Lens ya macho zitatumika kuwajua wauaji, kwani sura zao huhifadhiwa na lens za macho
Mkuu acha kutazama sana sinema za CSI zitakuzingua akili...
 
Hivi ule wimbo wa TAZAMA RAMANI,bado unatumika?AU kuna wimbo mwingine,tz siyo nchi nzuri tena. R.I.P Wana.
 
Tazama ramani utaona nchi nzuriiii
Yenye mito na maziwa mengi ya nafakaa
Maisha yetu haya yangekuwaje sasaaa
Utumwa wa nchi Nyerere ameukomeshaaa

Mkuu huu wimbo umenikumbusha mtungaji wake Brigedia Mosses Nnauye (R.I.P.), ambaye ametuachia kichwa nazi Nape.

Hivi ule wimbo wa TAZAMA RAMANI,bado unatumika?AU kuna wimbo mwingine,tz siyo nchi nzuri tena. R.I.P Wana.
 
Soo sad, but one day the truth will come out. Hakuna siri chini ya jua. The system that was behind it is under curse of the innoncent blood.
 
Vigumu kuamini kauli yako ukizingatia kwamba mauaji hayo yametokea wakati mmoja, ni dalili tosha ni kitu cha kupangwa. Hivyo ningeamini kauli uliyosema kama tukio ni moja au mawili, lakini kufikia idadi ya waendesha pikipiki watano kwa wakati mmoja ni jambo linaloibua maswali mengi.

Enyi wana ccm msio na akili ni nani aliyewaloga?
 
Ni muhimu kutoa heshima kwa ndugu hawa waliokutwa na maafa. Hata hivyo kabla haijathibitishwa, sio sawa kuhusianisha vifo hivi na mambo ya kisiasa. Tutoe nafasi ya watu kuyaangalia mambo katika taswira halisi pasipo kuelekeza kila jambo pasipo ushahidi wa kutosha kwenye siasa. Amani haipo, lakini haifai kuhukumu kabla ya kuchunguza hasa kwa suala zito kama hili linalogusa maisha ya vijana ambao ndio kwanza wanaelewa maana ya maisha. :crying:
 
Back
Top Bottom