Arusha kwa sasa KWISHNEY! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha kwa sasa KWISHNEY!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GeniusBrain, Jun 26, 2012.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nashukuru na nimeliona limeandikwa pia kwenye blog ya michuzi. Tuacheni utani na masihara mji wa Arusha kwa sasa una hali mbaya sana. Hali ya mji wa Arusha kiuchumi kwa sasa sio maridhawa kabisa. Nilijaribu kutembelea maeneo mengi ya kibiashara km sokoni ambapo kuna maduka mbali mbali . Ikifika saa 10 tu jioni wanaanza kufunga hakuna wateja, hata zile siku za kawaida za kazi. Biashara za taxi , ma-bus ndio usiseme, karibia 90% ni mbovu mbovu sana. Hali ya usafi wa mji ni mbaya sana. Kwa kweli , wana JF tuna haja yakuutizama upya mji huu, GENEVA OF AFRICA INAPOTEA KWENYE RAMANI
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  We unasema Arusha. Nchi imekwisha hii, kila kona ukienda watua ni wakali kweli. Hali ni mbaya kweli kweli. Utapeli umezidi, yaani nashukuru tu kuna amani.
   
 3. m

  majebere JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Watajuta kwanini walimchagua yule kichaa, sasa hawana hata wa kuwa wakilisha Bungeni
   
 4. RUBERTS

  RUBERTS Senior Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maisha ni magumu, watu hawana fedha. Ni tatizo la uchumi wa nchi. Nahisi wewe unataka kuunganisha Arusha na siasa za CDM. Mtwara kuna maisha mazuri? Kuna biashara nzuri toka asubuhi hadi usiku?
   
 5. m

  majebere JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Utapeli hata huko nchi zilizo endelea upo ndugu yangu.
   
 6. Wikiliki

  Wikiliki JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 529
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hali ni mbaya nchi nzima. wewe unashangaa arusha. hata hayo unayosema sii sahihi hali ipo kama kawaida.
   
 7. m

  majebere JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Sio watu hawana hela, sema wewe huna hela.
   
 8. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Sio arusha tu,...mbona dar ndio zaidi
   
 9. h

  hans79 JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Kamradi ka matofali toka bmoyo kataleta tofali kuanzia kesho, si umemwona jakaya alivyoanzisha bonge la mradi wa matofali huko bmoyo!
   
 10. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Hii nayo thread?
   
 11. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  kuzorota kwa biashara ya Tanzanite kwa KIASI kikubwa imeathiri Hali ya uchumi katika jiji la Arusha, na hili limetokea baada ya mwekezaji..... Lakini pia utalii kwa Sasa sio kiviile na low season ndo hiyo inaishia na pia kukosekana kwa viwanda vingi IDADI Kubwa ya watu haina ajira.... Lingine pia ni Kuwa Sasa upatikanaji wa bidhaa umekua rahisi zaidi unamfikia Mtu hadi nyumbani so watu hawana time ya kwenda madukani mjini, tembelea katika viunga vya mji wa Arusha Kama kijenge zote Mwanama na ya juu, ngarenaro, sekei, ngulelo, kwa mrefu, sakina, kwa iddy, ilboru...... Kote huko Unakuta "Visuper Market" pamoja na vihardware, so tathimini yako ya kuangalia maduka ni irrelevant ingawa kiukweli uchumi wa Arusha umeshuka
   
 12. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sinafuu ya Arusha je moshi maisha kwa kweli yamekaba na sio miji hii tu karibia nchi nzima
   
 13. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Acha ushamba mkuu si vyema kumwita mh. Mbunge G. Lema Kichaa. Je walikochagua wenye akili timamu hali za majimbo yao zikoje ukilinganisha na Arusha? Hivi huyu anayelalamika alitaka akipita mjini watu wamnunulie soda na chips ndo ajue hali ya Arusha ni nzuri? hli ya Arusha haina tofauti kiuchumi na mikoa mingine. Kigezo ambacho angekitumia ni kwenda TRA kuangalia kama mapato yameshuka kwa kiasi gani kutokana na watu kufunga biashara. Ujinga alioleta hapa hatujui unalengo gani kwani hata mikoa kama Mwanza, Morogororo na Dar hali sio nzuri je huko nako kuna Vichaa wabunge?
   
 14. m

  majebere JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 566
  Trophy Points: 280
  Rekebisha kidogo hapo, ni Lema sio mheshimiwa mbunge. Halafu hivi wewe umeenda Mwanza hivi karibuni? Nakushauri uende ukaone biashara inavyo kwenda.
   
 15. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  I support you 100% kama mkazi wa Arusha. Uchumi umeshuka kutokana na machimbo ya Tanzanite kupewa Makaburu tofauti na zamani wakati wazawa ndo walikuwa wachimbaji kiasi kwamba impact ya wao kuwa na kipato ilionekana mji mzima . Makaburu wanapeleka hela zote SA kwa hiyo asilaumiwe Mbunge kwani yeye si TIC wanaouza nchi.
   
 16. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Whatever you call it ukweli unajulikana kwani hata waalimu na mabalozi wastaafu huendelea kuitwa Mabalaozi why don't we respect our MP ambaye rufaa yake haijamtupa. Chuki binafsi zitakupunguzia umri mkuu try to show love even to your enemy
   
 17. d

  dguyana JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo mnataka kusema shauri ya CHADEMA ili musikilize watu wanasemaje? Hali ni mbaya kote sababu ya CCM.
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,728
  Trophy Points: 280
  Tatizo la nchi nzima.
   
 19. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280

  Mbona juzi juzi tuu jiji la Arusha na Manispaa ya Moshi imetajwa kama miji misafi hapa nchini? Huwezi kupima uchumi wa Arusha kwa kuangalia uchangamfu wa biashara katika maduka ya stendi ndogo hasa msimu huu ambao siyo wa sikukuu.
   
 20. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,760
  Trophy Points: 280
  Uchafu ni sahihi ila swala la ugumu wa maisha ni tz nzima.
  Swala la maduka eti kukosa wateja labda utruelezee umetumia analysis ipi kufanya hiyo research.
  Kuhusu swala usafiri naamini umepotoka, sasa watu wasipo safiri shuhuli za kawaida za maisha zinaendaje?
  Mwisho, hapa kwetu pesa ni ngumu na maisha ni juu siku zote tumezoea wewe unashangaa coz ni mgeni hapa.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...