Arusha kwa sasa KWISHNEY!

Arusha kwa sasa KWISHNEY!

Watajuta kwanini walimchagua yule kichaa, sasa hawana hata wa kuwa wakilisha Bungeni

We punguani kweli hao ccm tangu uhuru wamefanya nini zaidi ya kugeuka wakoloni wa TZ na kwa taarifa yako wamerundika pesa uswizi mpaka waswisi wamewastukia!Huko unakopajua wewe penye uchumi mzuri kwa ajili ya sisiemu ni wapi?Mbona unatumia masaburi kufikiria?Nchi yote inahitaji ukombozi kutoka kwa wanukombozi ambao ni watu wenye akili timamu sio nyie mnaofikiria kwa kutumi masaburi!Kuna uhusiano gani kati ya siasa na kushuka uchumi wa Arusha?
Polisi wa arusha kazi yao ni kulinda CCM na majizi wake,watalii wanauawa arusha wanyama wanaibwa na watalii wanapelekwa ulaya eti leo vifaru waliokuwa wamejaa TZ wameisha tunapewa vifaru na waingereza sasa waje kutalii nini wakati wanyama wanao, polisi wanaua watu arusha, Kenya hamna amani elshaabab wanatishia maisha na ndio njia ya watalii, Maisha yamekua magumu kutokana na serikali kutosimamia uchumi kwa kudhibiti mifumko ya bei na kuongeza kiwango cha uhalifu nchini hasa Arusha ambapo utalii ndo njia kuu ya uchumi!Hivyo ndio vimeshusha hadhi ya mji wa Arusha pamoja na kuisha kwa kesi za ICTR za mauaji ya rwanda sio chadema Pusi wee!
 
Unasema Arusha ni nchi nzima sasa hali ni mbaya na hii yote ni uongozi mbovu na udhaifu wa rais
Nashukuru na nimeliona limeandikwa pia kwenye blog ya michuzi. Tuacheni utani na masihara mji wa Arusha kwa sasa una hali mbaya sana. Hali ya mji wa Arusha kiuchumi kwa sasa sio maridhawa kabisa. Nilijaribu kutembelea maeneo mengi ya kibiashara km sokoni ambapo kuna maduka mbali mbali . Ikifika saa 10 tu jioni wanaanza kufunga hakuna wateja, hata zile siku za kawaida za kazi. Biashara za taxi , ma-bus ndio usiseme, karibia 90% ni mbovu mbovu sana. Hali ya usafi wa mji ni mbaya sana. Kwa kweli , wana JF tuna haja yakuutizama upya mji huu, GENEVA OF AFRICA INAPOTEA KWENYE RAMANI
 
Arusha kwa sasa KWISHNEY ! Hii hayo ni siasa?
 
Arusha ni mji unaoendeshwa na wenyeji.tofauti na dar ambayo wazaramo wamesukumwa nnje ya mji.mji hauna wenyewe.hali mnayosema mbaya ya kiuchumi hii ndo hali inayosababisha ccm wasitawale arusha milele
 
Mkuu hakuna uhusiano wowote kati ya mji kuwa msafi na mzunguko wa pesa.

Ndugu yangu Ritz soma vizuri bandiko la mleta mada, amehoji usafi wa jiji la Arusha
 
Last edited by a moderator:

Kama ulivyosema kwamba imeandikwa kwenye BLOGG ya MICHUZI,ni kweli lakini kwanza uelewe kuwa Michuzi wanaongoza kwa upigaji wa picha bora, lakini hawana uelewa mkubwa wa uchambuzi wa mambo ya kitaalamu kama unavyofikiri,Kwa upeo wangu na kwa vile ninavyoijua Arusha, tatizo ni (A)Tofauti ya kitabia- mfano wateja wa arusha hawapendi vitu vya bei rahisi tofauti na miji kama Dar ambako Michuzi ndio anaishi,hii inatokana na muingiliano wa jamii mbali mbali-(B) Serikari haina mipango madhubuti-mgao wa arusha katika maendeleo ilitakiwa uwe sawa na dar,arusha inaingiza pesa nyingi kupitia utalii na madini lkn hela inaenda dar,alafu kikwete anaenda kutesa nazo nje ya nchi! (C) Jamii ya arusha wanaishi nje ya mji tofauti na Dar unakuta watuwengi wapo barabarani wananunua bidhaa nafuu (D) Watu wengi wanamipango ya muda mrefu na wana invest zaid kwenye shule za gharama,viwanja nk (E) Wakazi wengi wanafanya e-shopping na ukitoa Nairobi kwa east africa,arusha inaongoza kwa biashara za mtandaoni sio barabarani-kwa kifupi:Hata kama huwezi amini jamii ya wachaga ambao ni wadau wa mkoa huu,ndio pia wamewekeza katika hiyo mikoa ambayo unadhani iko vizuri.pia wana invest huku. CCM HAIENDANI NA SYSTEM YA ARUSHA KABISA,HUKU WATU HAWAPENDI UBABAISHAJI.
 
Songea ni kilio. Saa moja mjini hakuna watu...huwezi kupata dala dala. Inasikitisha!
 
Acha ushamba mkuu si vyema kumwita mh. Mbunge G. Lema Kichaa. Je walikochagua wenye akili timamu hali za majimbo yao zikoje ukilinganisha na Arusha? Hivi huyu anayelalamika alitaka akipita mjini watu wamnunulie soda na chips ndo ajue hali ya Arusha ni nzuri? hli ya Arusha haina tofauti kiuchumi na mikoa mingine. Kigezo ambacho angekitumia ni kwenda TRA kuangalia kama mapato yameshuka kwa kiasi gani kutokana na watu kufunga biashara. Ujinga alioleta hapa hatujui unalengo gani kwani hata mikoa kama Mwanza, Morogororo na Dar hali sio nzuri je huko nako kuna Vichaa wabunge?
Mkuu usimfukuze tena kichaa aliechukua nguo zako mtoni wakati ukioga maji, utaonekana wewe ndiyo kichaa, waache waropokaji wanaomwita Lema kichaa wakati wanaona ni dhahiri hali ya uchumi ni ngumu nchi nzima.
 
wewe una mawazo mgango tu..tena utakuwa unafikiria pafupi sana hali ni mbaya nchi nzima na kama unataka kuhusisha na kuchagua upinzani nenda pwani walikochagua ccm wana nini nenda singida, nenda morogoro ni nchi nzima wewe usiangalie kwa jicho la makengeza kwani hata dar kuna nini kama siyo watu wengi tuu!hali ya uchumi ni mbaya kwa nchi nzima
 
Arusha Ina rasilmali kibao Bali hakuna viongozi wa kuelekeza uekezaji ili kunufaisha jamii nzima na hivyo hali ya Maisha kuendelea kuzorota.Ni wakati Watu wa Arusha wanatakiwa kuwa makini na kuchagua uongozi unaofaa baada ya Lema ili kurekebisha hali hii..Mambo ya kutazama vyama ni Upumbavu..Kwani hata katika uchaguzi
(elections are won by men and women chiefly because most people vote against somebody rather than for somebody)Tusiangalie kumpa yeyote tu ili mradi sio CCM, kutokuwa na nia na hivyo kuendeleza ugumu wa Maisha kwa kumuweka kiongozi tusiyemjua.Watu Kama Kina nyari wanauwezo mkubwa wa kurekebisha hali ya Ugumu wa maisha kwa wananchi,bila kujali maneno ya waongeaji wasio na upeo na wenye wivu na ubinafsi kwa kunena mauvu kuhusu viongozi wanaoonekana kuwa makini katika kazi zao.Kuongelea mambo usiyoyajua ni upumbavu usio na kifani na hatima yake ni kuambukiza wengine ujinga utakaodhuru maisha yao.Nyari aliachiliwa na Mahakama kwa kukosekana na hatia katika kesi iliyotungwa na wapinzani wake wa kibiashara.Uadilifu na utendaji kazi wake ni makini hasa kwa wanaomfahamu vizuri...usiongelee usiyoyajua...Na ni jukumu la Jamii Forums kufuta Matope yanayopakwa kwa watu ambao tayari sheria imeona wana haki na kuacha kutengeneza jukwaa la kukashifiana bila kujali utu na sheria.Arusha inahitaji uongozi na Nyari Anafaa.
:drum::drum::drum:...Haya sasa..ngoma hiyo...cheza ujuavyo.
 
Mi nadhani labda mtoa mada atakua amedondoka toka huko mbele mda si mrefu ndio maana anaona kama vile mji umezorota sana..hali hii ni kawaida kama ulikua nje ya nchi kwa muda flani halafu ukarudi hm.lzima utaona kama vile hali ya maisha imeshuka sana kulinganisha na zamani!!! Zamani imeshapita..sikatai hali imekua mbaya Arusha..lakini mabadiliko ya kiuchumi ya mji wa arusha yametokea kutokana na mambo mawili makubwa....kwanza ..baada ya machimbo ya tanzanite kumilikiswa makaburu na pili...baada ya september 11, na mtikisiko wa uchumi wa dunia...watalii walipungu kwakasi ya ajabu...hivyo kwa kiasi flani uchumi wa arusa umeshuka lakini sio sana ingawa bado kuna masalia ya tanzanite na watalii..lakini ikumbukwe kua idadi ya makampuni pia imeongezeka hivyo ushindani umekua mkubwa pia katika sekta zote..mji pia umetanuka sio kama zamani town ndio ilikua kila kitu..
mkaliwakitaa unapozungumzia September 11 unarudi nyuma mpaka mwaka 2001 ile hali haina uhusiano na uchumi wa Arusha. Kwanza kabisa Uchumi wa Arusha upo juu sana kwani ni ya tatu baada ya DSM na Mwanza. Unaposema utalii umepungua unatumia vigezo gani? Kwa mawazo yako kampuni za kitalii zinaongezeka siku hadi siku au zinapungua? Jibu ni kuwa zinaongezeka; sasa kama watalii wamepungua hizo kampuni zinahudumia kina nani? Mahoteli na Camping sites zimeongezeka sana na kila moja inapata wateja wa kutosha hivyo ushawishi wenu hauna nguvu. Miaka miwili iliyopita Arusha haikuwa na "Traffic Jam" leo Jam kila kona; hayo magari yameokotwa kama Arusha Kwishney?

Najua hitimisho la hoja yenu inahusu Ubunge wa Arusha mjini
 
Ni wakati wa Tanzania kuangalia upeo wa kiongozi tukijua ni wapi tunahitaji kwenda.Kiongozi wa mwisho tuliyekuwanaye ni Mwalimu Julius Nyerere na bila shaka waliomfuata hadi sasa wanaonekana tu kuwa "officials"ambao kwa bahati mbaya au nzuri wamepata fursa kuingia ofisini. Hawajawahi kuwa na hata chembe ya sifa ya Uongozi...Sasa ni wakati wa kuachana na mambo ya CUF,Cha-Dema.Chama Cha M****:confused2:.Cha Nani! Hakuna Cha mtu...huo ni ubinafsi...Tuchague Uongozi na Chama Kitakachotoa VIONGOZI wengi basi kishinde.Lahaula!Asiyekubali kushindwa na si mshindani.
Tunaangazia sasa kuwa na Umoja wa Afrika Masharika na hivi punde Rais wa Jumuiya nzima...Umoja wa Africa Unatusubiri...Tunahitaji kumaliza maswala ya Nyumbani mapema ili tuweze kuangalia maslahi yetu katika Afrika.Siasa Za penny mbili haitatupeleka mahali...
 
Rekebisha kidogo hapo, ni Lema sio mheshimiwa mbunge. Halafu hivi wewe umeenda Mwanza hivi karibuni? Nakushauri uende ukaone biashara inavyo kwenda.
Uongo wa CCM kumbe upo hata ndani yako. Pole Majebere. CCM Ziiiiiiiiiiiiiiiii, Chadema Oyeeeeeeeeee!
 
Nashukuru na nimeliona limeandikwa pia kwenye blog ya michuzi. Tuacheni utani na masihara mji wa Arusha kwa sasa una hali mbaya sana. Hali ya mji wa Arusha kiuchumi kwa sasa sio maridhawa kabisa. Nilijaribu kutembelea maeneo mengi ya kibiashara km sokoni ambapo kuna maduka mbali mbali . Ikifika saa 10 tu jioni wanaanza kufunga hakuna wateja, hata zile siku za kawaida za kazi. Biashara za taxi , ma-bus ndio usiseme, karibia 90% ni mbovu mbovu sana. Hali ya usafi wa mji ni mbaya sana. Kwa kweli , wana JF tuna haja yakuutizama upya mji huu, GENEVA OF AFRICA INAPOTEA KWENYE RAMANI

Hali unayoiona Arusha halafu wewe unasema ni mbaya, ingekuwa ni Mtwara basi wamakonde wengeona wako peponi , Mtwara ukiamuka asubuhi unataka ukanunue Mswaki utakuta maduka bado yamefungwa, Arusha saa za kunywa chai hotelini Mtwara ndo hoteli zinafagiliwa, wewe Arusha acha tu kitu usichokijua ni sawa na usiku wa giza.
 
Back
Top Bottom