VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Imesemwa kuwa jiji la Arusha litatikiswa kesho na Lowassa. Ya kwamba Lowassa atatangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM. Ya kwamba mtikisiko huo utatokea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapa Arusha. TeamLowassa imekuwa ikitangaza mitandaoni, luningani na magazetini. Inatangazwa Jumamosi ya kesho,tarehe 16/5/2015. Mambo hapa ni tofauti sana. Hata mimi nimeshangaa mno. Watu wa Arusha hata hawajui kama kuna jambo hilo.
Nimefika hapa jana jioni. Nmezunguka jijini Arusha na kuzungumza na wenyeji wa Arusha. Wakaazi wa Arusha hawajui lolote kuhusu kesho. Nikadokezwa kuwa kama jambo hilo lipo basi wahudhuriaji wataletwa kwa mabasi, malori,ndege na kadhalika. Si wenyeji wa jiji la Arusha. Kwa ninachokishuhudia hapa, naamini nilichoambiwa na wana-Arusha.
Yawezekana Lowassa meshauriwa vibaya. Ya kuwa anakubalika Arusha nahivyo atangaze nia hapa. Amedanganywa. Arusha si uwanja wa kutambia kwa Lowassa na hata CCM yetu. Arusha si uwanja vutizi kutamba na kijni kibichi(ndugu zangu Lunyungu, Bramo Elli na MANI wanajua).
Nasubiri kuona na kupokea wageni wakutikisa Arusha na nchi kwa ujumla hiyo kesho!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Arusha)

Last edited by a moderator: