Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Arusha, 22 Machi 2025 – Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Japheth Asunga (Mb), ambaye pia ni kiongozi wa msafara wa Kamati hiyo, ameongoza ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Arumeru.
Katika ziara hiyo, Kamati imeeleza kuridhishwa na kukamilika kwa mradi huo wa kimkakati, na kuipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) kwa usimamizi bora wa utekelezaji wa mradi ambao umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 500 kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Akizungumza na vyombo vya habari, Japheth Asunga alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeleta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. “Sasa hivi uzalishaji wa maji AUWSA umefika lita milioni 200 kwa siku, wakati mahitaji yako chini ya kiwango kinachozalishwa. Kwa hiyo kuna ziada ya maji, hivyo wananchi wanapaswa kuhamasishwa ili waweze kuunganishiwa huduma”, alisema Mhe. Asunga.
Wakiwa katika eneo la Mto Themi – Njiro Atomic, Kamati ilikagua bomba la majisafi linalovuka kwenda kutoa huduma upande wa pili wa mto pamoja na bomba kubwa la majitaka linalosafirisha majitaka hadi mabwawa 18 ya kutibu majitaka yaliyoko umbali wa takribani kilomita 30 kutoka eneo hilo. Aidha kamati alisisitiza umuhimu wa kuilinda na kuitunza miundombinu ya mradi huo kwa kuwa imejengwa kwa gharama kubwa.
Kamati pia ilitembelea jengo jipya la Makao Makuu ya AUWSA lililopo Kata ya Olmoti, jirani na eneo linalojengwa Uwanja wa Kimataifa wa Mpira (AFCON), ikiwa ni ishara ya uwekezaji katika miundombinu ya taasisi na utoaji bora wa huduma.
“Tumeipongeza sana menejimenti. Tumeona kazi nzuri. Kwa ujumla wake, katika miradi yote – huu wa majitaka, usambazaji wa majisafi na ujenzi wa jengo hili – Kamati yetu tumeridhika na tumeona kwamba kuna thamani ya fedha zilizotumika”, alisema Asunga