Arusha: Jaribio la kumteka Katibu wa Chadema Jiji la Arusha kwenye Ofisi za Halmashauri ya Jiji hilo zashindikana

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,260
2,000
FB_IMG_1550996502710.jpg


Siku ya Ijumaa tarehe 22/02/2019 kuanzia saa 5:41 asubuhi - 6:10 mchana nilikuwa kwenye jaribio la kutaka kutekwa kwenye Ofisi ya Afisa Uchaguzi/EO wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Nilipigiwa simu na Afisa Uchaguzi akiniambia kuna jambo la dharura na la umuhimimu la kutaka kuonana na mimi (Katibu wa CHADEMA Wilaya Arusha Mjini) na mimi kwa fikra/mtazamo wa kwanza nilidhani ni wito kuhusu kikao kinachohusu maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. At first sikupata hofu wala chembe ya mashaka kwa sababu Afisa Uchaguzi huyu nimeanza kumjua tokea mwaka 2014 akiwa kwenye position hiyo hiyo mpaka leo 2019.

Nilienda Halmashauri nikiwa na Diwani mmoja wa CHADEMA ambaye alinipa lift kwenye gari yake na yeye akiwa anaenda Halmashauri kwa shughuli zake na tulipofika Halmashauri tulimkuta Diwani mwingine maeneo ya reserved parking ya Mkurugenzi na Meya na tukasalimiana na Mimi nikamwambia "... Kaka nimeitwa na Afisa Uchaguzi hapo Ofisini kwake ngoja nimuone inawezekana ikawa ni mambo ya Uchaguzi ..." yule Diwani wetu wa CHADEMA akanijibu kuwa "... inawezekana maana mimi nilikuja kumuona Mkurugenzi ila nimeshindwa kumuona kwa sababu pale Ofisini kwake yupo kwenye Kikao na nimeona watu wa usalama wengi kama kuna kikao fulani hivi ..." basi Mimi nikaingia kwenye Ofisi ya Afisa Uchaguzi na nilipofika kama nikamsalimia akanikaribisha lakini alikuwa ananiuliza maswali mengi mengi mfululizo kuhusu maandalizi ya CHADEMA kwenye Uchaguzi na kunichangamkia sana (isivyo kawaida kumbuka nimewaambia huyu Mama nimeanza kushughulika naye kuanzia 2014 kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014, 2015 kwenye Zoezi la Uandikishaji wa Wapiga Kura, Uchaguzi Mkuu wa Udiwani, Ubunge na Urais 2015, Uchaguzi Mdogo wa Mbunge Arusha Mjini Dec 13,2015, Uchaguzi wa Marudio wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Mitaa 8 ya Jiji la Arusha 2016, Uchaguzi Mdogo wa Marudio ya Udiwani 2017, Uchaguzi Mdogo wa Marudio ya Udiwani 2018 na Vikao vingine vingi vya Halmashauri nilivyohudhuria kama Katibu wa CHADEMA Wilaya Arusha) na last kabla hali haijachafuka aliniuliza "... Inno mwanangu huwezi kuacha Siasa, angalia wajukuu zangu (akimaanisha watoto wangu/yeye huwa ananiitaga Inno mwanagu) wasije wakashindwa kuishi, hizi Siasa hizi ...".

*Ghafla simu yake ikaita akaniambia "samahani ninaomba nipokee hii simu" akatoka nje kuongea na hiyo simu then akarudi ndani akaniambia ngoja nikuandalie Chai nikamshukuru kwa kumwambia Ahsante niko sawa, palikuwa na Karanga kwenye meza yake akaniambia kula basi hata hizi Karanga, nikaokota punje kadhaa za Karanga, akaniambia samahani nakuja (alitoka nje) baada ya muda mfupi sana alirudi ndani/Ofisini pale aliponiacha nikaona watu watatu wanakuja (nilipokuwa nimekaa nilikuwa natazamania na dirisha hivyo kila anayekuja nilikuwa ninamuona) kati ya wale watu watatu mmoja nilimtambua alikuwa ni DSO wa Wilaya Arusha (ninamfahamu kwa sabubu wakati Uchaguzi unaanza huwa kinafanyika kikao cha Briefing (Makatibu wa Vyama vya Siasa Wilaya, OCD, DSO, RO, RO1, RO2, RO3, ARO, EO na wengine).
DSO alikuwa ameambatana na watu wengine 2 lakini hao wawili kwa kwa first impression yangu, body language na body morphology zao ni MANYAMERA/TASK FORCE.

Afisa Uchaguzi akaanza kusalimiana na DSO kwa salamu zisizoisha (zenye kujirudia rudia) na baadaye akamwambia "... Mkuu karibu muendelee na kikao" huku akiwa anampisha kiti DSO akae. (DSO na yule mtu mmoja waliingia Ofisini kwa Afisa Uchaguzi then mtu mmoja kati ya wale waliokuja na DSO alikuwa amesimama mlangoni) kwa mazingira hayo unaona kabisa nilikuwa chini ya Ulinzi tayari lakini good enough wakati haya yote yanaendelea nilikuwa ninawaona Madiwani wetu wa CHADEMA wawili niliowaacha pale kwenye eneo la parking ya Mkurungenzi & Meya na hata lolote lingitokea ndani ningeweza kuwaita na wangekuja kuni rescue.

*DSO alijeuka akaangalia nje kupitia dirishani then akamwambia yule Mama Afisa Uchaguzi ngoja kwanza tukamuone Mkuu hapo juu (Kwa haraka nilielewa anataka kumuona Mkurugenzi maana Ofisi yake ndiyo ipo juu kule ambapo gesture ya mkono wa DSO ulielekeza).

Kitendo cha wale mabwana kutoka tuu pale Ofisini nilimwambia Afisa Uchaguzi ngoja nikamuone Mh ... pale nje narudi sasa hivi. Sikusubiri ruhusa nilitoka kwa haraka nikamkuta Mh Diwani pale nje nikamwambia "... Mh ... tafadhali tuingie kwenye gari na tutoke eneo hili haraka sana kuna hali mbaya hapa" basi bila kusita Mh Diwani aliwasha gari tukaondoka pale Halmashauri kwa Haraka sana na kuelekea kwenye Super Market ya yule Diwani.

Tulipofika tuu Afisa Uchaguzi alimpigia simu yule Diwani akimwambia Mkurugenzi anataka kuongea na wewe "Mkurugenzi alipoanza kuongea akaanza kumfokea Mh Diwani nani amekuruhusu uondoke hapa ninakupa dk 5 tuu uwe umerudi hapa la sivyo nitakuweka ndani na hauta toka simu ikakatwa.

Kuna maelezo mengi baada ya hiyo simu lakini let's me end here.

Ninawaomba Viongozi wenzangu na Wanachama sasa tuchukue tahadhari kubwa ya Kiusalama.

*Mimi nilikuwa nitekwe na kama Chama kingejitokeza na kusema mara ya mwisho Katibu wetu wa CHADEMA Wilaya alionekana Halmashauri alipokuwa ameeitwa na Afisa Uchaguzi, wao wangekuja na hoja ya utetezi wangesema mtu hawezi kutekwa kwenye eneo la Halmashauri mchana kweupe na Halmasahuri kuna CCTV camera.

Lakini what if Watekaji wangeniweka chini ya ulinzi pale pale kwenye Ofisi then wakaninyang'anya simu zote then nikafungiwa chooni mpaka muda wa usiku then nikatolewa nje ya eneo la Halmashauri kwenda kuteswa au kuuwawa huko pasipojulikana.

*Kwenye hili jambo kwanza kuna MUNGU kwa sababu mimi mwenyewe ninaamini hivyo then kingine kilichosaidia ni wale Madiwani wawili waliokuwepo kwenye eneo la Reserved Parking ya Mkurungenzi na Meya kwa sababu ukiwa kwenye Ofisi ya Afisa Uchaguzi unachokiona kupitia Dirisha la Ofisi yake ni hiyo reserved parking ya Mkurugenzi na Meya.*

*Simu DSO aliyompigia Diwani (aliyenitoa na gari pale Halmashauri) jioni baada ya tukio hili kutokea inadhihirisha shahiri kuwa DSO ana guilt conscious kwenye hii issue, I have to declared this public kuwa sina urafiki wala undugu na DSO zaidi nimewahi kuonana naye kwenye vikao kadhaa Mimi nikihudhuria kama Katibu wa CHADEMA Wilaya Arusha

Glory be to the Almighty GOD
Zaburi 34:19 - 22

KISANYAGE INNOCENT J
KATIBU
CHADEMA WILAYA ARUSHA
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,470
2,000
Inatisha saaana aiseeeee, viongozi msitembee alone, at least mtu awe anakufuata kwa mbali Kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu yule mwenye mwenyekiti kule Kigoma kupotea kwake amehusishwa DSO, na hapa anatajwa DSO, jee sasa iwe wazi kuwa hawa ma DSO ndio watu wanaoteka na kuua wenzao?
Kule Tarime walio jaribu kumteka Zakaria usiku walikuwa maafisa usalama sema Mkuria yule akashtukia mchezo akawatwanga shaba mpaka wakajitambulisha, lakini ilikuwa imetoka na tungempata kwenye viroba.
Jee wananchi sasa wajue huwa hawa maafisa ndio wabaya wao? Kweli nchi ifikie hapo jamani?
Zamani hakuna watu walikuwa wanapendeka kama ikigundulika wewe ni UWT, Lakini sasa unaogopa hata kujulikana hivyo kwani unakuwa huna tofauti na mumiani mbele za raia.
Awamu ya Tano imepatwa na nini?
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
40,187
2,000
It is à matter Of time....
Mkuu yule mwenye mwenyekiti kule Kigoma kupotea kwake amehusishwa DSO, na hapa anatajwa DSO, jee sasa iwe wazi kuwa hawa ma DSO ndio watu wanaoteka na kuua wenzao?
Kule Tarime walio jaribu kumteka Zakaria usiku walikuwa maafisa usalama sema Mkuria yule akashtukia mchezo akawatwanga shaba mpaka wakajitambulisha, lakini ilikuwa imetoka na tungempata kwenye viroba.
Jee wananchi sasa wajue huwa hawa maafisa ndio wabaya wao? Kweli nchi ifikie hapo jamani?
Zamani hakuna watu walikuwa wanapendeka kama ikigundulika wewe ni UWT, Lakini sasa unaogopa hata kujulikana hivyo kwani unakuwa huna tofauti na mumiani mbele za raia.
Awamu ya Tano imepatwa na nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

IKINGO

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,853
2,000
Hongera saana Kamanda Mungu alikusimamia.
Uliwazidi ujanja hao, ungejikuta uko peke yako na CHATU bro.
Sasa hivi ukiona mwanausalama yupo mahali basi kuweni naye makini sana kabla hajasabisha hasara kwa jamii ya hapo.
Hao watu ndo wauaji first class.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom