Arusha: Hukumu ya kesi inayomkabili Lengai Ole Sabaya imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2021

Uko sawa, leo anahukumiwa kwa kosa la unyang'anyi kwa kutumia silaha.
Wakati Kesi ya Uhujumu Uchumi ikiendelea. Na Ile ya Utakatishaji fedha ikiwa inamsubiria, hizo ni kwa mkoa wa Arusha, bado kule Kilimanjaro ana kesi kibao za kujibu
.
Akichomoka kwenye hizi kesi zote mtaani nina hakika hata chomoka.
Duh
 
Kwanini lakini baadhi yenu mnatumia neno H mbele ?
Inakera kwa mtu anaejua kusoma na kuandika halafu unaandika kwa makusudi kabisa

Au ni lugha mpya
uko sahihi ila na wewe ukiwa kama msomi ungeelezea unamaanisha nini Kuongezea H mbele kwa maneno yapi with reference to maandishi ya muanzisha mada.
Nina uhakika kuna watu hawatakuelewa unataka umaanishe nini
 
Uko sawa, leo anahukumiwa kwa kosa la unyang'anyi kwa kutumia silaha.
Wakati Kesi ya Uhujumu Uchumi ikiendelea. Na Ile ya Utakatishaji fedha ikiwa inamsubiria, hizo ni kwa mkoa wa Arusha, bado kule Kilimanjaro ana kesi kibao za kujibu
.
Akichomoka kwenye hizi kesi zote mtaani nina hakika hata chomoka.
Mtaani atakutana na wakina kingai
 
Kesi ya Unyang'anyi kwa kutumia silaha iliyokuwa inamkabili Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili Daniel Mbura na Sylivester Nyegu imeahirishwa mpaka Oktoba 15, 2021.
 
uko sahihi ila na wewe ukiwa kama msomi ungeelezea unamaanisha nini Kuongezea H mbele kwa maneno yapi with reference to maandishi ya muanzisha mada.
Nina uhakika kuna watu hawatakuelewa unataka umaanishe nini

Kichwa cha habari na habari yenyewe imebadilishwa kabisa
Najua hawatanielewa kwa sababu nilijibu kwenye uzi ulioandikwa na mtu tofauti na huyu
Mods wamebadilisha
 
Wanajukwaa nawasimu,

Hongereni kwa kuendelea kuchapa kazi na kulijenga Taifa letu.

Kama nitakuwa ninakumbuka vema, ilisemwa tarehe ya leo (1/10/2021) Ni siku ya hukumu ya Kesi ya Lengai Ole Sabaya ( Kesi ile ya mwanzo).

Je kumbukumbu zangu ziko sawa?.

=========

Mahakama ya hakimu mkazi Arusha inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya Unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai ole sabaya na wenzake wawili.

Sabaya na wenzake wanatuhumiwa kutenda makosa hayo February 9 mwaka huu katika duka la Saad store linalomilikiwa na Mohamed Saad lililopo katikati ya jiji la Arusha wakidaiwa kuvamia na kupora wakitumia silaha.

Kesi hiyo iliendeshwa mfururizo takribani siku 35, mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Odiro Amworo kutoka mkoani Geita, ambapo upande wa serikali uliwasilisha mashahidi 11 na vielelezo kadhaa, hivyo Leo kesi hiyo inatarajia kufikia tamati kwa kutoa hukumu kwa washtakiwa hao watatu .

Washtakiwa wengine wanaotarajiwa kuhukumiwa hapo kesho ni Silvester Nyegu na Daniel Mbula

2948393_FB_IMG_1628770975220.jpg

==========

UPDATE:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kutoa hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Hukumu imeahirishwa hadi Oktoba 15, 2021
Bado ana week 2 zaidi za KUNYEA NDOO
 
Back
Top Bottom