Arusha hakuna ukarimu kwa wateja

Arusha hakuna ukarimu kwa wateja

Nazani unaiongelea Zanzibar kwa Arusha big NO! Nakubali chache hazikosekani na labda bahati yako mbaya ukawa unatembelea hizo sehemu zenye huduma mbaya..

Lakin Arusha ni sehemu yenye huduma nzuri, wachakarikaji wengi, ushindani ni mkubwa wa biashara.So kila mtu anajitahidi kutoa huduma bora ili kuwavutia wateja wengi.

Pia sehem nzuri zenye huduma na bidhaa bora zinajulikana usijiendee tu sehem ni sehem.ova
huu ni unafiki mtupu
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Paki Landcruiser unapohitaji huduma utapata huo ukarimu
 
Wako karibu na kenya. Lugha ya naomba imegeuka kuwa leta

Wewe umemaliza kila kitu. Kuna rafiki yangu sana ni m-Kenya naishi naye hapa Arusha, huwa anashangaa sana kwenda dukani unasema 'naomba'! Yeye anasema 'Utaombaje kitu dukani wakati unalipa pesa'? Na huwa wanaendana na hawa watu wa hapa ile mbaya.

Kinyume chake kuna mnya-Rwanda tulikuwa tunaongea naye aka challenge customer care ya watu wa Arusha na akasema kama ingekuwa kwao Rwanda biashara zingekufa fasta.
 
Watu wenye tabia hizo wakifika Dar wanajifanya wanajua ustaraabu huu ama ule, kukosoa wenyeji wao wastaaraab waliotukuka. Karibuni nyote Dar mjifunze heshima ya kuwasiliana na wateja
 
Nazani unaiongelea Zanzibar kwa Arusha big NO! Nakubali chache hazikosekani na labda bahati yako mbaya ukawa unatembelea hizo sehemu zenye huduma mbaya..

Lakin Arusha ni sehemu yenye huduma nzuri, wachakarikaji wengi, ushindani ni mkubwa wa biashara.So kila mtu anajitahidi kutoa huduma bora ili kuwavutia wateja wengi.

Pia sehem nzuri zenye huduma na bidhaa bora zinajulikana usijiendee tu sehem ni sehem.ova
Arusha njaa tupu na watu wake njaa kama kenya...
 
Ukiishi sana mwituni na wanyama lazima utaiga tabia zao. poleni wafugaji mtapata shida sana mpaka mje mkae kwenye mstari wa kistaarabu
 
ni kweli aisee mimi ni mzaliwa wa arusha lakini sasa niko huko nyanda za juu kusini watu wana heshima acha unakuta kijana tena wa kiume unapomlipa hela anapokea mikono miwili, na kike anainama kidogo... nashangaa sana na ninaona aibu sijazoea kabisa
Dah.... Ni kweli kabisa huko Arusha hakuna utamaduni wa kuinama/kubend kidogo....!!! Sio tu wakati wa kupokea pesa.... Hata wakati wa salamu etc...

Haya tunayaonaga kwa wenzetu wasukuma, wanyakyusa.... Mpaka una-admire....!!!
 
Wanaume wa Dar mnapendwa kubembelezwa sana.
Makonda anawasubiria mkatoe matumizi ya Hawara zenu.
 
Yes nakubaliana na michango ya watu humu. Arusha imekua influenced kwa kila kitu na Nairobi. Kuanzia kuzungumza na tabia nyinginezo ni athari za muingiliano na wakenya. Na by the way, hata Mara pia ni kama Arusha hawana kabisa customer care.
 
Jamii za kifugaji nyingi sio wakarimu...
Sijafika Arusha ila huko naona ndio wamezidi.
Naendaga Musoma ni Tofauti kabisa na Masasi , yani ukienda masasi utatamani ukae huko moja kwa moja.. wana ukarimu sana...

Wengine wanyakyusa nmechangamana nao sana huku nnakoishi sijui huko kwao.. jamani ni wakarimu mnyakyusa ukimpa kitu hio asante yake mpaka unaweza kulia.

Kama hujafika Arusha huwezi kuinenea mema au mabaya yake .. wewe ongelea jambo unalolijua kiundani..
 
Dah.... Ni kweli kabisa huko Arusha hakuna utamaduni wa kuinama/kubend kidogo....!!! Sio tu wakati wa kupokea pesa.... Hata wakati wa salamu etc...

Haya tunayaonaga kwa wenzetu wasukuma, wanyakyusa.... Mpaka una-admire....!!!

Tabia ya kuinama si nzuri kwa watu wanaojitambua na kuheshimu tamaduni zao....
 
Ni kweliiii hawana costumer care kabsa arusha huku


Ni miji mingi Mkuu ina hilo tatizo, ukitoka Kenya ukaingia Arusha unaona mambo yapo kinyume kabisa, ukaribu upo Songea na Tanga tu kwa nchii hii
 
Habarini wana wa nchi wenzangu,

Naomba leo nishee jambo kidogo kuhusu hili jiji la Arusha.

Ni takribani mwaka sasa nimekuwa katika jiji hili la Arusha kikazi, kabla ya hapo nilikuwa naishi Dar. Waswahili husema "mteja ni mfalme", hii kauli nahisi inatofautiana katika viwango vya kuthibitika kati ya eneo ya eneo.

Niwe specific kidogo kwamba hapa nazungumzia hasa maisha ya chini na ya kati, yale ya juu ya kwenda hotels za nyota 5 huko sinazo sana taarifa zake. So hapa ni kwa maeneo ambayo nimekuwa nikienda sana( mama ntilie, muuza mihogo, migahawa ya kwaida, pubs, vioski, duka la bidhaa za vyakula, ETC)

Ni hivi kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja nilichokaa nimegundua kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya maeneo niliyowahi ishi say Dar es Salaam na huku katika ukarimu kwa wateja.

Mara nyingi ukienda sehemu ama kununua bidhaa au kupata huduma thamani yako huonekana ndogo, sijajua hawa wauzaji huwa wanawaza nini, lakini unaweza enda dukani au mahali upate kinywaji lakini hata karibu huipati, yani neno karibu limekuwa gumu kwa watoa bidhaa wengi wa huku, sijajua wakilitamka linawapunguzia nini.

It happened zaidi ya mara 8 kwamba nimeenda katika mgahawa nipate chakula lakini badala ya mtoa huduma anikaribie na kunisikiliza mimi nimekuwa ndiyo wa kumkaribia mtoa huduma na kumwambia kuwa nataka huduma gani(hayupo bize wakati huo) sidhani hata kidogo kama hili ni sawa.

Kiukweli iliponitokea siku za mwanzo nilifikiri ni baadhi au wachache tu wako hivyo ila kadiri siku zilivyosonga nikaja gundua asilimia kubwa ya wafanya biashara huku Arusha hawana ukarimu kwa wateja wao, iwe ni duka la bidhaa za kawaida, pubs, vioski, migahawa au pengine ni nadra sana kukarimiwa kama mteja (poor hospitality).

Najua wengine mnaweza pinga ila mimi sioneagi mtu kama wale wengine nimejaribu kuwaambia kile ambacho kwa sehemu nimeona kipo huku Arusha.

Ndugu zangu wana Dar es Salama nawamisi sana kwa ukarimu wenu wa biashara, huku mambo ni tofauti kabisa.

Haki Mungu hakupi vyote watu wa Arusha kuna vitu wamejaliwa lakini pia kuna vitu hawana, hiki ni kimojawapo kati ya vile wasiokuwa navyo.

KAMA WATANZANIA KUNA MAMBO YAPASWA TUAMBIANE ILI TUREKEBISHANE, VINGINEVYO TUTAPIGWA BAO SANA KIBIASHARA NA MAJIRANI ZETU NA UKIANGALIA WAKUBWA WASHADONDOSHA SAHIHI KWENYE FREE TRADE AREA YA AFRICA.

DONE
wananyenyekewa wanaokata mkwanja wa nguvu, wewe kachala unayeenda kula kwa mama ntilie wali sahani moja buku nani akunyenyekee?. Nenda Novotel, Arusha hotel,au Ngurdoto uone kama hawatakunyenyekea.
 
Jamaa amesema haoneagi mtu, na jamaa ni CDM kabisa huyu ila kaamua kuwaambia wenzake ukweli tu. Hivyo kuna ka ukweli flani ktk malalamiko yake
Hiv kwa nn tumeadhiriwa na akili finyu kias ichi? Mm sijaona sehem hyo mtu kazungumzia yy ni mwana chama wa chama gan!!! ila kazungumza swala zuri ambalo wausika wakilifanyia kaz has a walegwa inaweza boresha huduma paspo kujali hao watoa huduma ni wanachama wa chama gan!!! Sasa cjui ndo huwa tuna siasa za ajabu mpaka mambo ya msingi tunaweka ujinga
 
ni kweli aisee mimi ni mzaliwa wa arusha lakini sasa niko huko nyanda za juu kusini watu wana heshima acha unakuta kijana tena wa kiume unapomlipa hela anapokea mikono miwili, na kike anainama kidogo... nashangaa sana na ninaona aibu sijazoea kabisa
Huu ni ushamba tu hamna heshima wa cha nini ukuku wa hivi siafikiani nao kabisa
 
Back
Top Bottom