Malingumu
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 616
- 429
Habarini wana wa nchi wenzangu,
Naomba leo nishee jambo kidogo kuhusu hili jiji la Arusha.
Ni takribani mwaka sasa nimekuwa katika jiji hili la Arusha kikazi, kabla ya hapo nilikuwa naishi Dar. Waswahili husema "mteja ni mfalme", hii kauli nahisi inatofautiana katika viwango vya kuthibitika kati ya eneo ya eneo.
Niwe specific kidogo kwamba hapa nazungumzia hasa maisha ya chini na ya kati, yale ya juu ya kwenda hotels za nyota 5 huko sinazo sana taarifa zake. So hapa ni kwa maeneo ambayo nimekuwa nikienda sana( mama ntilie, muuza mihogo, migahawa ya kwaida, pubs, vioski, duka la bidhaa za vyakula, ETC)
Ni hivi kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja nilichokaa nimegundua kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya maeneo niliyowahi ishi say Dar es Salaam na huku katika ukarimu kwa wateja.
Mara nyingi ukienda sehemu ama kununua bidhaa au kupata huduma thamani yako huonekana ndogo, sijajua hawa wauzaji huwa wanawaza nini, lakini unaweza enda dukani au mahali upate kinywaji lakini hata karibu huipati, yani neno karibu limekuwa gumu kwa watoa bidhaa wengi wa huku, sijajua wakilitamka linawapunguzia nini.
It happened zaidi ya mara 8 kwamba nimeenda katika mgahawa nipate chakula lakini badala ya mtoa huduma anikaribie na kunisikiliza mimi nimekuwa ndiyo wa kumkaribia mtoa huduma na kumwambia kuwa nataka huduma gani(hayupo bize wakati huo) sidhani hata kidogo kama hili ni sawa.
Kiukweli iliponitokea siku za mwanzo nilifikiri ni baadhi au wachache tu wako hivyo ila kadiri siku zilivyosonga nikaja gundua asilimia kubwa ya wafanya biashara huku Arusha hawana ukarimu kwa wateja wao, iwe ni duka la bidhaa za kawaida, pubs, vioski, migahawa au pengine ni nadra sana kukarimiwa kama mteja (poor hospitality).
Najua wengine mnaweza pinga ila mimi sioneagi mtu kama wale wengine nimejaribu kuwaambia kile ambacho kwa sehemu nimeona kipo huku Arusha.
Ndugu zangu wana Dar es Salama nawamisi sana kwa ukarimu wenu wa biashara, huku mambo ni tofauti kabisa.
Haki Mungu hakupi vyote watu wa Arusha kuna vitu wamejaliwa lakini pia kuna vitu hawana, hiki ni kimojawapo kati ya vile wasiokuwa navyo.
KAMA WATANZANIA KUNA MAMBO YAPASWA TUAMBIANE ILI TUREKEBISHANE, VINGINEVYO TUTAPIGWA BAO SANA KIBIASHARA NA MAJIRANI ZETU NA UKIANGALIA WAKUBWA WASHADONDOSHA SAHIHI KWENYE FREE TRADE AREA YA AFRICA.
DONE