Arusha hakuna ambulance

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,222
764
Jana usiku kwenye majira ya saa tano nilienda kupeleka mgonjwa hospitali ya kwa Dokta Mohamed hapa Tank la maji Arusha. Mpgojwa wangu alikuwa anaumwa sana. Wakati akiwa anapatiwa matibabu akaletwa mgojwa mwengine anaitwa Charles Malay wa Malai freight. Huyu bwana alikuwa hoi bin taaban. He was serious sick x 1000. Alipatiwa huduma ya kwanza kwa haraka sana. Alipata oxygen, drip na huduma zote. big up wahudumu wote.

Kwa kweli hali ya bwana Charles iliendelea kuwa mbaya sana sana ikabidi ma doctor wa pale washauri mgojwa apelekwe KCMC kweli ndugu zake wakakubali. Shida ikaja kwenye Ambulace, pale ipo ila driver alikuwa hayupo. Mini nikajitolea kwenda AICC hospitali kwenda kukodisha ambulace. Nilivyofika nikaambiwa kwamba ambulace inapaki AICC headquarter. Nikatoka nikaenda Mount Meru Hospital hapakuwa na msaada kabisa.
 
Mbunge wenu kila siku anahangaika kutafuta sifa. Hana muda wa kutatua kero za wananchi.
 
Back
Top Bottom