Bubu huyo ni miongoni mwa washukiwa wa makosa ya uhaini waliopandishwa leo kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi. Yupo pia mwandishi wa habari wa Millard ayo aitwaye Thomas pamoja na watoto ambao ni chini ya umri wa miaka 18.
Swali langu, bubu anawezaje kufanya uhaini?
Swali la pili, Ikiwa chombo cha habari Cha Millard Ayo hakireport habari za mwandishi wake aliepata matatizo akiwajibika katika kazi zake, ni picha ama taswira gani ambayo wananchi tunaipata? Je vyombo vya habari havipo huru? Ama ni Ile SHERIA ambayo mwandishi akikosea anawajibika yeye. Je SHERIA hii ni kandamizi?
Swali la tatu, Kwanini watoto wadogo wanapelekwa mahabusu na rumande wakichanganywa na watu wazima? Je serikali inalitazamaje hili na inawajengea watoto hao picha gani, watoto ambao ni taifa la kesho? Ni nani atawajibika kwa uharibifu huu wa akili na ukosefu wa haki za watoto?
Mh.Rais alitangaza msamaha katika hotuba yake wakati akifungua bunge. Je kwanini watu hawaachiwi mpaka leo? Ama bado upelelezi unaendelea??