Arusha Bila Trafic Inawezekana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Arusha Bila Trafic Inawezekana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndallo, Jul 6, 2012.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,133
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  WanaJF wenzangu habari za leo na habari za mihangaiko ya kilasiku katika kutafuta riziki yako pamoja na riziki ya familia zetu. Husika na kichwa cha habari hapo juu ni kua dukuduku langu ni kwa Matrafic japokua sio wote kama watakuwepo na moyo kama wakutojali dukuduku langu kuhusiana na kero hii nitakayo iwekeka hapa mbele.

  Jiji la Arusha kwa sasa hivi ni vurugu kila kona kuhusiana na miundombinu tunayoiona katika ujenzi wa kuzikarabati barabara zilizopo katikakati ya jiji letu, kwahiyo ninaposema ni vurugu natumaini unaelewa namaanisha nini kwasisi waedeshao magari hususani waendesha Bodaboda/Baiskeli na hata waenda kwa miguu.

  Sasa nirejee kuhusiana na mada husika hapo juu kwa hawa Askari wetu wa usalama barabarani! kwauzoefu wangu wakuendesha gari barabarani hapa Arusha Trafic kwakipindi hiki wamekua ni kero tupu, wanaelewa kabisa kua katika barabara za katikati ya jiji zimechimbuliwa kabisa na hazipitiki kwahiyo barabara mbadala ni zile ambazo ni chache kama vile barabara kuu itokayo Kijenge/Njiro kuja mjini ambazo ndio kiungo kikubwa kwa wafanyakazi wanaofanya kazi katikati ya jiji.

  Barabara nyingine ni kama hii itokayo kwa Mkuu wa mkoa kuja Polisi hadi stendi kuu ya mabasi panda juu kuja Mianzini kuunganisha na barabara kuu ya Arusha Moshi na Arusha Nairobi, na nyingine ni hii barabara itokayo Philips kuja Sabasaba hadi Round About ya Impala Hotel. Kwahiyo kwakuangalia harakaharaka kuna barabara kama 7/8 hivi ambazo ndizo zinazotumika katika jiji hili achana na hizi barabara za Makao Mapya ambazo nazo ziko katika ukarabati.

  Sasa basi, kilio changu kwa hawa Matrafic wa jiji la Arusha sio kwamba hawaelewi kua saa za asubuhi na jioni msongamano wa magari kwa wanaokwenda makazini asubuhi na kurudi jioni ni balaa mno hata zile Trafic Lites zimekua hazina tena msaada, sikatai kua Trafic hawa huwa wanatoa msaada kwenye mataa yale. Tatizo kubwa linalokuja hapa ni kua utakuta msongamano wa magari ni mkubwa mno halafu wakati huohuo Trafic kasimamisha Lori bila kuzingatia msongamano huo! Je nikwamba hawajali muda wa watu kurejea majumbani au kwenda kazini? na kuepusha msongamano huu wanaouona? Au kama gari hilo linamakosa hamna utaratibu wa kuwaandikia Notification wakaenda kulipa na wasipolipa then mchukue hatua nyingine kama vile kumpeleka mahakamani?

  Njoo barabara hii ya Sokoine ukitoka maeneo ya Shoprite kuja Clock Tower tuanze na hapa Shoprite kuna Trafick wanne! ukipanda kidogo hadi hapa Posta ya Meru utakuta Trafic wanne! panda tena hadi hapa Friends Coner kwenye Tuta, wako watatu hadi wanne! twende panda juu hadi hapa Naaz Hotel karibu na mnara wa saa nao tena wako wanne! Kaa ukielewa kua hii ni barabara moja tu ambayo hupitisha magari mawili namaanisha sio Double road, jumlisha waenda kwa miguu/waendesha Bodaboda/waendesha Baiskeli! hapa sasa umeshanielewa ni vurugu ya aina gani tunayo hapa Arusha.

  Trafic bila kuzingatia muda wa watu kufanya kazi wanasimamisha magari hadi matano katika barabara hii moja tu, je ni vurugu ya aina gani tunayoipata kama sio kuna mazingira ya Rushwa hapa? Na pia sipingi kauli yangu ya Rushwa La hasha rushwa imeenea sana katika barabara za jiji hili. Na rushwa hii ukitaka kuijua kua ipo kwa hawa Matrafic wetu wewe angalia saa moja asubuhi hadi saa nne za asubuhi, utaona Trafic wako bize kwelikweli sio kwenye kuongoza magari na kuondoa misongamano hapana, yaani wako bize haswa kwenye kuyasimamisha magari pembeni nakujifanya kuyakagua pasipo kujali muda wa watu kuwahi makazini kama sio mazingira ya rushwa ni nini???

  Muda wa saa nne baada ya pilikapilika za kukusanya hiyo rushwa, njoo hapa maeneo ya Naaz Hotel kama nilivyokuelezea hutakosa Trafic wasiozidi wanne, ingia Hotelini ndani hapa Naaz utakuta Trafic walewale waliokua bize kujifanya wanayakagua magari bila kuzingatia muda wa watu kuwahi makazini bila kusahau misongamano, Trafic huyuhuyu ninayemjua ni muajiriwa wa serikalini wanakunywa chai na KUKU! Chai ya hapa Naaz Hotel kwamimi ninavyoijua ukitaka kushiba chai kweli ya hapa basi sio chini ya Shilingi elfu 8000 hadi 10000 kwa mtu mmoja! Anayeishi hapa Arusha na aliyewahi kunywa chai ya hapa Naaz naomba anipinge. Baada ya chai ya saa nne Trafic hawa hutawaona saana kwenye barabara hizi tena kwa wingi kwakua muda huu ni muda wa watu wako makazini na magari wameyapaki, muda huu utaenda mpaka kwenye saa nane hadi tisa.

  Funga kazi ni muda wa watu kutoka makazini hapa ndio vurugu mechi wao wanasema ndio funga kazi! Sina mengi ya haya bali hii ndio Arusha ninayoijua kuhusina na Matrafic wetu.

  Wito wangu kwenu kwa Matrafic, jamani barabara tunazozitumia kwasasa ni chache mno kama nilivyobainisha hapo juu, zingatieni muda wa watu kufanyakazi bila kusahau kuepusha misongamano kwa wanotembea kwa miguu/Bodaboda na waendesha baiskeli, kama kweli mtu gari lake linamakosa basi muandikie Notification aende polisi akalipe na sio kusimamisha gari pembezoni mwa barabara na mnavyojua barabara zenyewe ni nyembamba! Sina mengi zaidi ya haya lakini nalipenda sana jiji langu la Arusha na pia naipenda sana nnchi yangu Tanzania bila kusahau tutokomeze rushwa kwakua rushwa ni adui wa haki.

  Nawatakia sikukuu njema ya Sabasaba yenye furaha na weekend njema. Asante napia nikipenda NAWASILISHA!
   
 2. T

  Turbulence Senior Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Uliyoyasema ni sahihi kabisa! Hawa polisi traffic wa ni hovyo. Pia wanaohusika na ujenzi wa barabara ni hovo! Sijawai kuona ujenzi holela kama huu. Barabara nyingi za mjini zimefungwa! Kero tupu. Kwa nini wasijenge kwa awamu???
   
 3. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu. Hayo kwa system tuliyonayo kwa sasa ni ya kuvumilia sana. Kikubwa uzima. Ukitaka kuchukia traffic police anzisha safari ya Singida au hata Mwanza. Utasimamishwa Majengo, Duka bovu, Mti mmoja, Makuyuni, Minjingu, Mbuyu wa mjerumani, Magugu, 2kms before babati, 2kms after Babati, Dareda, kuna vituo viwili tena kabla ya Katesh, na kabla ya kuingia Singida, ukitoka Singida hapo Mzani, misigiri. Ukitoka misigiri inakuwa nafuu. Unabakisha road bumps au humps. Ila Mkoa wa Manyara unaongoza kwa traffic wala rushwa na nasikia wanapeleka hisabu kwa wakubwa wao. Basi likitokeza tu elfu mbili inaondoka. Ni aibu.
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,133
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Kama tunavyojua kua huwa kuna siku rasmi waliyoipanga ya siku ya usalama barabarani na huwa tuyapeleka magari yetu vituoni nakwenda kukaguliwa halafu baada ya wao kuyakagua wanatunapa Stiker! Kulikoni kuanzia January mpaka December nikusimamishwa barabarani kama sio mazingira ya RUSHWA???? Inaniuma sana:frusty:
   
 5. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,133
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Kuna mwaJF mwenzangu ameniPM nakuniuliza hiyo chai ya bei mbaya kama hiyo ni kweli nimemuhakikishia ni kweli na kama haamini aende hapo Naaz Hotel na maadhi ya kwenye mabaa ajionee hiyo chai na supu zinazonywewa hio mida ya saa nne asubuhi!
   
 6. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,120
  Likes Received: 10,469
  Trophy Points: 280
  Nimemiss Arusha yangu jamani...
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ndallo ukitaka kwenda kazini kwa sasa hapa arusha kama unaingia saa mbili uwe saa kumi na mbili ushaingia barabarani maana kila siku kama ni kimemo utakikuta cha kuchelewa
  hakuna barabara hata moja yenye uafadhali hapa arusha na isiyo na foleni
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,133
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Mr Rocky hususani mimi naishi maeneo ya Sakina kwa Idd huwa saa nashuka mida ya asubuhi kuna wale Matrafic wako pale Tripple A wananjaa na kiu balaa!
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Mkuu Ndallo sisi tunaotokea maeneo ya kijenge huku na moshono ni balaa unaweza kutana na foleni kuanzia kule depot ya coca cola na traffic wapo kuanzia masai camp wengine hapa njia panda ya kuigia kota za AICC na wengine unakutana nao hapa Kibo palace bado wa mnara wa saa bado wa hapa CRDB yaani ni kero tupu mkuu
  Na sometime wao ndio wanasababisha foleni kabisa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,133
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Halafu angalia kwa umakini sana utakuta maeneo ambayo hawa jamaa wanapenda kusimama na kutusimamisha hapakosi baa au Hoteli fulani wanapenda kula mno ndio maana Trafic anayetokea mikaoni akaja Arusha baada ya miezi 6 lazima awe na Kitambi! na hata kwa Matrafic wa kike nao ni hivyohivyo baada ya miezi 6 utawaona nao wanavaa sketi Mayenu! Hiii nchi bwana.
   
Loading...