Sijui wewe unaishi wapi hadi uwe mgumu kuelewa, lakini kwa ufupi mji wa Arusha uko katika Next Level!
Wana Arusha wana uwezo wa kufanya japo kitendo chochote ili kuonyesha wanachoamini na kusimamia mioyoni mwao.
Nimeshudia leo dereva mmoja wa magari yanayoenda kwa jina la MILANO(wanaoishi Arusha wanayajua sana), akigomea maelekezo ya traffic waliokuwa wanaopanga magari eneo la gereza kuu Kisongo, ili kuupisha msafara wa JK.
Dereva huyo amebebwa juu juu na wanausalama wa msafara huo kwa Tanganyika -jeki na kuingizwa katika gereza kuu la hapohapo Kisongo, na majaliwa yake ni Jumatatu ambapo huenda akapata mzamana!...mbaya zaidi kijana huyo haonyeshi kujutia kitendo chake!Usipime na Wana-Arusha jomba!