Arusha bado ngoma nzito kwa JK!

Kazi kweli kweli! Hizi ni hisia au? Angepita town wangemfanya nini? Anyway ni mawazo yako tu screenmaster haikuwa hivyo.

Itakuwa ni ivyo ndo maana hata ulemkutano aliopanga juzi kati alienda makamu wake kwa woga wakukumbana na kile kilichomkuta mbeya ushauri kwa Jk `If u can't fight them join them` na sio kuwakwepa Cdm na watu wenye uchungu na nchi yao
 
Hivi Akipita Arusha kutatokea nini?Acheni Siasa za Uhasama nina hakika JK akija huko sioni kitakachotokea sanasana Ninawaomba siku akitua AR mjipange barabarani kumpokea kwa shangwe na nderemo kama enzi hizo lengo ni kuepusha Uhasama
Usiokwisha
Id name yako na akili yako ni SAWASAWA.
 
Wakuu,

Leo hii JK alikuwa huko Monduli Arusha kutunuku kamisheni za Maafisa wa Jeshi.

Taarifa za kuwasili kwa JK Arusha zilianza ziku chache zilizopita ambapo ilikuwa apitie uwanja wa ndege wa KIA, ndipo aingie kwenye msafara wa magari hadi Arusha, kutokana na sababu kuwa kiwanja cha ndege cha Arusha kipo matengenezoni, na njia ya kurukia ndege imefupishwa.

Lakini wasaidizi wake walistukia mpango huo, ambao ungemlazimu JK kupitia Arusha mjini ili aende Wilayani Monduli, na wakatumia nguvu ya dola kuepusha JK kupita Arusha mjini kwa kulazimisha wajenzi wa kiwanja cha ndege cha Arusha kuondoa makatapila ya ujenzi kwenye njia ya kurukia, na wakatakiwa kushindilia njia ya kurukia japo temporarily, ili mzee apitie uwanjani hapo, na kwa jinsi hiyo kuepuka kabisa kupita Arusha mjini.

Hakika Arusha ni tishio kabisa kwa mkuu huyu!
Ikiwa ni hivyo watafanyaje kampeni katika uchaguzi wa madiwani ikiwa mkulu wao anaogopa au inadhaniwa anaweza kuabishwa kwa kuzomewa n.k?
Suluhisho ni kufanya siasa za safi.
 
Mimi nimekuwa nikisema hapa jukwaani siku zote. Jk hawezi kuja Arusha. Hata Monduli amekuja kwasababu za kiitifaki. Graduate wa Monduli huwa wanatunukiwa vyeo na rais tu. Hawezi ku deligate kwa mtu. Ameamua kupitia juu kwa juu. Na ninaamini kama kungekuwa na uwanja wa ndege Monduli, basi hata uwanja wa Arusha asingetua. Hakuna kiongozi yeyote wa ccm anayeweza kuja Arusha hadi sasa. Najiuliza kampeni za uchaguzi wa madiwani waliotimuliwa sijui ni nani wa ccm atakayekuja kuwapigia debe!? Yangu macho!

Haliwaumizi chochote kwani wanajua Ar hawana jipya
 
Unauliza wangemfanya nini?
Waulize wasaidizi wake wakwambie kwanini wameamua kum'risk kwa kumpitisha kwenye kiwanja kilicho kwenye ujenzi, wakati KIA ipo na inaendelea na operations!
Mbali ya ujenzi, Arusha ilikuwa na Weather mbaya kabisa asubuhi alipotua, lakini altenative ilikuwa ni Arusha tu....not KIA!

Nimelipenda jibu lako mkuu na huyo alouliza wamgemfanya nini asipolikubali atakuwa mnafiki
 
Ni kweli Monduli ni jimboni kwa Lowassa lakini hakuwepo muda wote JK alipokuwa pale maana mimi nilikuwepo uwanjani na suala la yeye kutumia uwanja wa kilimo Anga lilipingwa tangu na wanausalama waandamizi wakishauriana na wale wa makao makuu na ilikuwa ashukie KIA kutokana na uwanja huo wa Arusha kuwa kwenye matengenezo lakini kutokana na wao kuona inawezekana kuutumia kwa dharula ndipo ametumia uwanja huo.

Jk leo alikuwa akionekana mpole sana sana na hakuwa na raha na alisema maneno machache sana tena ya kusoma wakati wa kuwatunuku maofisa hao ila wakati mafahali yalipomalizika alionekana kuwa na ka uchangamfu kidogo na aliweza hata kuwaita watoto wachache walikuwa pembezoni mwa barabara za uwanja wa gwaride na kuongea nao kidogo na kuendelea na mambo mengine.

Mali ya pua yanamfika ndo anajifanya mkarim hee! Na bado hiyo ni rasharasha tu
 
Hivi Akipita Arusha kutatokea nini?Acheni Siasa za Uhasama nina hakika JK akija huko sioni kitakachotokea sanasana Ninawaomba siku akitua AR mjipange barabarani kumpokea kwa shangwe na nderemo kama enzi hizo lengo ni kuepusha Uhasama
Usiokwisha

Utafanya ivo wewe na familia yako mnaofikiria kwakutumia masaburi na sio wana Arusha walioelimika na kujua haki zao
 
Jk unalo limekuganda chakufanya ili tuje kukumbuka kwa jema jiuzu (resign)
 
Mbeya waliandika bango Mbeya nchi rais Sugu, Arusha nayo itakuwa nchi rais Dr. Slaa!
 
Mnaochangia hii mada mnataka kutuambia Rais Kikwete hakifika Arusha wana Chadema watampiga?
Hayo umesemA wewe, lakini jiulize kwanini hakatizi mjini!..
Last two weeks ilikuwa aje kuzindua chanjo za measles, na magari ya matangazo yalitangaza mpaka D-Day, lakini dakika za mwisho wanaompenda walimwonya kuwa asijaribishe kusogeza pua yake A-Town!...na kwa usikivu wake aliamua kumtuma Gharib Bilal, na yeye akabaki Ikulu!.Mia.
 
Sijui wewe unaishi wapi hadi uwe mgumu kuelewa, lakini kwa ufupi mji wa Arusha uko katika Next Level!
Wana Arusha wana uwezo wa kufanya japo kitendo chochote ili kuonyesha wanachoamini na kusimamia mioyoni mwao.

Nimeshudia leo dereva mmoja wa magari yanayoenda kwa jina la MILANO(wanaoishi Arusha wanayajua sana), akigomea maelekezo ya traffic waliokuwa wanaopanga magari eneo la gereza kuu Kisongo, ili kuupisha msafara wa JK.

Dereva huyo amebebwa juu juu na wanausalama wa msafara huo kwa Tanganyika -jeki na kuingizwa katika gereza kuu la hapohapo Kisongo, na majaliwa yake ni Jumatatu ambapo huenda akapata mzamana!...mbaya zaidi kijana huyo haonyeshi kujutia kitendo chake!

Usipime na Wana-Arusha jomba!

Tumechoka. Na JK anajua. na RC anajua kavamia jiji. kama CCM haitaamini waje kwenye kampeni waone watakavyoachwa.
 
Back
Top Bottom