Arusha; Baba aokolewa akitaka kujinyonga baada ya mtoto kubebwa na mafuriko

Arusha; Baba aokolewa akitaka kujinyonga baada ya mtoto kubebwa na mafuriko

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
10,414
Reaction score
18,438
Kijana mmoja ajulikanae Kwa jina la jimmy au almaarufu Baba Adriana, mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa Lemara ameokolewa akitaka kujinyonga baada ya mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 6 aliyekuwa nae kwenye pikipiki yake kusombwa na maji wakati wakivuka mto.

Tukio Hilo limetokea njiro mtaa wa Dabo B ambapo mvua kubwa na ya aina yake ilinyesha jioni ya jumapili jijini Arusha na hivyo kusababisha mito kufurika maji na barabara kujaa maji na baadhi ya mitaa maji kuingia ndani,.

jimmy baada ya kutoka katika kazi zake alipitia watoto wake walipokuwa wameshinda Kwa bibi Yao ili aende nao nyumbani lakini mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 4 alikataa katakata kuondoka , na hivyo kuondoka na mtoto mkubwa ambae ndo huyo Adriana huku mvua ikinyesha walivyofika sehemu yenye mto ili avuke daraja baadhi ya watu akiwemo mtoto Wake(mtoto alimwambia baba tusivuke maji ni mengi haya) walimkataza Kwa kumwambia kuwa maji ni mengi hivyo asivuke daraja lakini jimmy hakusikia.

Akiwa darajani maji yalimzidi nguvu mtoto akaanguka kwenye pikipiki na kubebwa na maji. Hadi Leo mtoto hajapatikana Bali begi lenye madaftari na nguo zake TU ndio vimepatikana, ila mwili Bado.

Baada ya tukio Hilo Jimmy alichanganyikiwa na hivyo kwenda kujitundika kitanzi baada ya watu kuingia ndani na kumkuta akining'inia ndipo walipomuokoa na kumfunga kamba miguuni na mikononi baada ya akili kumruka.

Hadi Sasa Bado Hali ya Baba huyo haijawa sawa na Bado kafungwa kamba miguuni na mikononi ili asijidhuru.


Update...........


Hatimae yule mtoto aliyesombwa na maji Fuvu lake limepatikana Leo tarehe 11 yaani siku ya nane baada ya mtoto huyo ajulikanae Kwa jina la Andriana mwenye umri wa miaka sita kusombwa na maji wiki iliyopita wakati akiwa kwenye pikipiki yeye na babayake.
Ni baada ya watu waliokuwa wakichunga ng'ombe kuona fisi akimalizia kula kitu kama fuvu la binadamu, ndipo walipomfukuza fisi huyo na kukuta ni kichwa Cha mtoto kimebakia sehemu kidogo TU ya kichwa huku ubongo nao ukiwa umeliwa.
 
Aliyataka .

Watoto walikuwa kwa Nini Yao ,Mvua imenyesha kilikuwa na ulazima Gani ya kuwalazimisha kuondoka nao??

Haya umeondoka na huyo mtoto mmoja akaona maji ni mengi akakuambia tusivuke na Wananchi wakamwambia tusivuke maji ni mengi yeye akalazimisha matokeo yake mtoto maji yakamshinda , Sasa huyu akitaka kununua mtoto waje labda utajili siyo Bure .

Ndo maana uniform zionekane na madafutari lakini mwili haujaonekana huenda hiyo kujifanya kachanganyikiwa ni Gresha tupu.
 
Aisee vijana wengi wa Arusha wanakunywa sana visungura, serikali ya CCM imeharibu maisha yao kabisa.
Sasa hapa serikali inahusikaje,na Una uhakika muhusika ni mlevi?

Au ni kwasababu moyo wako usio na huruma wenye hila na udanganyifu unakwambia utype hivyo
 
Apumzike Kwa amani mtoto... amesababishiwa kifo cha uzembe na mzazi mjinga..
 
Wamuulize anataka akazikwe wapi akishakufa? Wamuache aende safari asokua na marejeo
 
Mwaka 1994 Ndugu yangu yaani kaka yangu ambae tumepisha mwaka Mmoja katika kuzaliwa alisombwa na maji mbele yangu.

Lile tukio mpaka leo ni kama naliona hivi, naogopa sana maji, sithubutu kuvuka katika maji hata kama ni madogo kiasi gani, sithubutu kuogelea hata iwe kwenye beseni.

Hata familia yangu nimepiga marufuku kuogelea au kuvuka maji.
 
Aisee vijana wengi wa Arusha wanakunywa sana visungura, serikali ya CCM imeharibu maisha yao kabisa.
Ingekuwa ni wewe, ungefurahia kifo Cha mwanao?
Pole sana mfiwa.
 
Back
Top Bottom