Arumeru Mashariki hawaitaji sera wanaitaji porojo - Mwigulu

magufuli hajaenda Arumeru kuahidi daraja kama alivyofanya Igunga? jamaa wa igunga wanasikiliza tu madaraja redioni baada ya uchaguzi!
 
Katika hali isiyo ya kawaida na wala haikutegemea kusikia kauli kama hii kutolewa na kada na meneja wa kampeni kwa mgombea wa ccm kwenye uchaguzi wa jimbo la arumeru mashariki mwigulu kuwa sababu inayowafanya ccm kampeni zao zitawaliwe na matusi na siyo sera zenye kujibu matatizo ya wanaarumeru ni kuwa kama wakitoa sera ambazo zitakuwa na uchambuzi wa kiuchumi basi mkutano utakaofuata watakosa watu ndiyo maana wanapiga porojo zilizojaa matusi,dhiaka na kejeli.
Mytake.
Kama ccm inajengwa na vijana mithili ya mwigulu basi kwishenie

yuko sawa! kwa mfano ingekuwa wewe uko ccm ungetangaza sera gani? si bora utukane? kuwa ccm kunaendana na kuwa mjinga!
 
Nashangazwa na kauli ya mwigulu aliyoitoa Arumeru kwamba kuna vijana wa Chama fulana wamenga kukimbia na masanduku yakura ili kuwapunguzia CCM kura.

Jambo hilo nimeshindwa kulielewa nikaliona kama mawazo ya kitoto kwasababu kura zinapigiwa vituoni na kuna ulinzi ambao ni wa Magamba, sasa itakuaje hao vijana ambao nadhani watakuwa labda hawana akili timamu kunyanyua sanduku la kura na kukimbia nalo au hayo masanduku ya sasa hivi yanaingia kwenye mfuko wa suruali?

Kama bwana Nchemba huna jambo la kuongelea nakushahuri mkapunzike kwasababu tunakoelekea unaweza ukazidi kuchemsha zaidi.
 
Kinachonifurahisha ni Mwigulu Nchemba, anavyocheza na akili za wana Chadema.
 
ccm na chadema wote wananunua vitambulisho vya kura.mwenye dau kubwa ndiye mshindi.
 
magufuli hajaenda Arumeru kuahidi daraja kama alivyofanya Igunga? jamaa wa igunga wanasikiliza tu madaraja redioni baada ya uchaguzi!

Bado hajaja yupo yule mzee wa kutoa povu aliyekimbizwa na nyoka kanisani aka mwanri
 
mwigulu ni anti virus ya ccm nitamwapudate asilete uchafu wake ndani ya nguvu ya umma.watanzania cku hz khanga tshirt na kofia ni rb ya polisi kwani utavivalia wapi na vilana walivyochoka na maisha magumu yaliyosababishwa na sisiem huku wao wakijineemesha na wengine wakiibiwa hotelini wakifanya ufuska?
 
Subirin tar 1 April tutajua aliyeishiwa sera. Mimi sina shaka na kama nimeishiwa na cdm wanataka kushinda ndio kweli wananishauri niondoke. Kilio cha nini kama CCM IMECHOKA? AM CONFIDENT CCM ITASHINDA

Kichekesho ni kuwa Mwenyekiti wako wa taifa analamba miguu ya wafadhili (wazungu) akitembeza kibakuli. Najua kwa nini unasema Nasari hana NGO, si unajua hiyo ndo inaonekana kuwa sera yenu ya CCM. Kila mke wa bosi anayeingia ikulu anapaswa kuwa na NGO ili aweze kuwarubuni wanawake ukianzia na Mkaa-hapa
 
magufuli hajaenda Arumeru kuahidi daraja kama alivyofanya Igunga? jamaa wa igunga wanasikiliza tu madaraja redioni baada ya uchaguzi!
Hajui kimeru...kule igunga alienda kuongea kisukuma ndo ilikuwa kazi yake maana hilo daraja wala halipo.....huyu Mwigulu au Mbinguni naona anadhihirisha kule ndani ya CCM kumejaa watu wanautumia masaburi
 
Toka kampeni za Arumeru zianze mwanzoni mwa Machi nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana dhidi ya wapiga debe wa CCM,wako watu wenye heshima na waliokabidhiwa madaraka makubwa sana kwnye chama na umma kwa ujumla. Hawa ndio wamekuwa mstari wa mbele katika kuendesha kampeni zinazotia kinyaa huko Arumeru. Baada ya kuona hali imekuwa mbaya hasa wiki jana ndipo nilipoanza kuamini pengine ndani ya CCM kumeanzishwa kiengo kipya KITENGO CHA MATUSI, hasa baada ya vitengo vingine muhimu kufeli.Kama ndivyo basi kitengo hiki chini ya katibu wake hodari na chapakazi Mwigulu Mchemba Madelu ndicho kitengo bora na maridadi ndani ya CCM. Sijaona kitengo kinachofanya kazi vizuri kama hiki toka mwanzo wa kampeni mpaka sasa. Hiki ndio kitengo pekee kinachopewa meno na sauti kwa sasa,ndicho kilichopewa umuhimu huko AM, na ndicho chenye bajeti nzuri kuliko vingine, nani anabisha? Ndicho kitengo kinacho-make headline kwenye magazeti ya serikali na chama. Magazeti hayaandiki tena kuhusu kilimo kwanza, yaandika habari nzuri za kitengo hiki. Mwenyekiti mstaafu rais Mkapa ametimiza wajibu wake kutoa sapoti kwa kitengo hiki. Katibu wake Mwigulu yupo pia humu JF akiwajibika ipasavyo, hivi punde tu atakuja hapa JF kuendelea na harakati za kitengo chake,amekoga nyoyo za wana JF kwa matusi na majitaka. Wasiwasi wangu ni je kitengo hiki kinamsaidia Sioi Sumari huko AM?
Hongera CCM,hongera katibu wa Kitengo cha Matusi CCM Lameck Mwigulu, kazi ni nzuri
 
mwigulu ni anti virus ya ccm nitamwapudate asilete uchafu wake ndani ya nguvu ya umma.watanzania cku hz khanga tshirt na kofia ni rb ya polisi kwani utavivalia wapi na vilana walivyochoka na maisha magumu yaliyosababishwa na sisiem huku wao wakijineemesha na wengine wakiibiwa hotelini wakifanya ufuska?

Mkuu hakuna cha tshit wala kofia wamejinarrow down wanagawa vitambaa vya kufunga kichwani kwa kinamama
 
Kuwa na NGO ndiyo sifa ya kuwa mbunge?
Mi nadhani hata msukuma mkokoteni anaweza kuchaguliwa kuwa mbunge, maadam ametimiza sifa zote.

mbona hata mganga wa kienyeji maji marefu ni mbunge??
 
yuko sawa! kwa mfano ingekuwa wewe uko ccm ungetangaza sera gani? si bora utukane? kuwa ccm kunaendana na kuwa mjinga!

Kwahiyo matusi ndiyo sera alizotumwa na chama kuja kuwatukana wameru?katika vitu ambavyo havipo kwenye mila za wameru ni matusi.
 
Kuhusu kutokuruhusu maswali ndugu yangu kwanza muda ni kikwazo pili huyu ndio kwanza anaomba ubunge angekuwa anaomba mara ya pili kuna la kujibu tatu mikutano ya hadhara kuna matatizo sisi huwa hatufanyi vurugu mikutano ya wenzetu ila kwetu ukiruhusu hayatakwepo maswali ya maendeleo bali namna gani mgombea abomolewe. Kuhusu porojo ndg yangu ndicho watu wanachotaka kusikia. Mimi first class economist nikishusha mambo ya growth models na inflation targeting siku inayofuata sipati watu mkutanoni. Samahani kama jibu halijatosheleza mengine ni utaratibu wetu kwamba tujibu kwanza kashfa alizozushiwa mgombea badala ya yeye ili mgombea aseme sera tu
Pamoja elimu yako mbona huna msaada katika kuukomboa uchumi wa nchi, kama kweli unachokisema katika maandishi mekundu hebu acha kuongea pumba waachie pumba waongee kina Lusinde!!!
 
Back
Top Bottom