Uchaguzi 2020 NCCR Mageuzi watikisa Arumeru Mashariki

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mgombea Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama cha Nccr Mageuzi Evva kaaya amezindua kampeni zake kwa kishindo huku akimwaga Sera ya kusaidia wanawake watoto kupata haki sawa na kuimarisha Afya kwa kila kata kupata zahanati.

Akizungumza katika viwanja vya shule ya msingi Nkoanrua Evva amesema kwamba kikubwa kilicho msukuma kugombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki ni kusaidia wananchi kupata maendeleo katika kipindi cha miaka mitano cha utumishi wake.


Amesema jimbo hilo kwa muda limekosa mwakilishi mwenye uchungu wa maendeleo na wengine waliopota kuwa wabunge wamekuwa wakijinufaisha wenyewe na sio kuleta maendeleo.

Aidha amesema endapo atachaguliwa atakikisha anafanya kazi ya uwakilishi ya kuleta maendeleo kwa wananchi baada ya kuwatumikia vyema kwa mika mitano akiwa Diwani wa ambapo ameleta maendeleo makubwa katika kata Nkoanrua

Naye msimamizi wa uchaguzi kupitia Nccr Mageuzi Taifa Atonny Komu ambaye pia ni Mgombea Ubunge jimbo la Moshi vijijini amesema chama chao kimemsimamisha Evva kwani historia ya jimbo hilo lilisha ongozwa na chama hicho Mwakab 1995 hivyo wananchi wana imani kubwa na Nccr Mageuzi

Amesema watajikita kutatua changamoto za wananchi katika majimbo yote walio simamisha wagombea nchi nzima kwani sera yao ni kutumikia wananchi na kupata haki sawa na maendeleo.

Kwa upande wao wananchi waliojitokeza kusikiliza Sera katika ufunguzi wa kampeni hizo wamesema kwamba wamekuwa na utuba za mgombea na wana imani endapo watamchagua wqtakua wamemoata mwakilishi sahihi wa kutatua matatizo yao.

IMG-20200911-WA0020.jpg
IMG_20200911_175459_3.jpg
 
Binti huyo mwenyewe kimo cha inchi kadhaa kutoka usawa wa bahari amesema kuwa hata mwenyekiti wa chama hicho "mama Tanzania" hana uhakika wa kurudi bungeni kutokana na madudu aliyofanya jimboni kwake!
 
Nampongeza kwa kudhubutu kugombea, hongera zake. Kwa monekano, huyu hawezi mikikimikiki ya kampeni. Angegombea kwanza uenyekiti wa serikali za mitaa, kijiji au udiwani.
 
Nampingeza kwa kudhubutu kugombea, hongera zake. Kwamonekano, huyu hawezi mikikimikiki ya kampeni.Angegombea kwanza uenyekiti wa serikali za mitaa, kijiji au udiwani.
Alikua diwani CHADEMA, akaunga mkono juhudi! Sijui kwenye juhudi ilikuaje, lakini ameandika kitabu, Magufuli ni Mpango wa Mungu, alimtuma Jerry Muro ampelekee Baba! Labda kitabu hakikusomwa pia!
 
Alikua diwani CHADEMA, akaunga mkono juhudi! Sijui kwenye juhudi ilikuaje, lakini ameandika kitabu, Magufuli ni Mpango wa Mungu, alimtuma Jerry Muro ampelekee Baba! Labda kitabu hakikusomwa pia!

Ni aibu kwa binti kama huyu na umri wake kujikombakomba kwa viongozi, hasa wa ccm.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom