Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hayo yanakuja baada kufungwa?, tusingesikia haya kama wangeshinda game, na Kuna gemu arsenal wameshinda bila Gyokres na Eze kuanza
 
Endelea kushangilia mpira mkuu hadi siku Arsenal itakapokuuwa ndipo ukiwa kaburini utaelewa nilichokiandika!
Ebo! Sababu ya kifo iwe mpira? Napigwa bomu uwanjani au?!Tubali mpira unabadirika kila zama mkuu. Kuna mda ulikuwa vipaji,ukaja pesa sahizi ndo haueleweki maana unaweza kuwa na kibunda ila sokoni wamejaa avarage players tu. Mchezaji bei kubwa ila ni wakawaida viwango vya wachezaji wanaonunuliwa Madrid sahzi wanaweza kushindana na Astonvilla.
Uko zama zipi mzee au hushangai sahzi timu nyingi kubwa karibu kila ligi zinapata shida sana hasa EPL Unajua ni kwanini? Mipira umebadirika sana kwa kila nyanja so tusitafute visingizio rahsi.
Utakufa wewe usiebadirika kulingana na dhama za jambo husika. Usikariri!!
 
Mmh we jamaa ni big critic wa Arsenal, ila uweke akiba ya maneno
Akiba ya maneno kwa arsenal? Hii arsenal tunaijua nje ndani mkuu siwezi kuweka akiba ya maneno kwa team kama arsenal.

Team nzima hakuna mchezaji mwenye goals 5+ halafu uchukue kombe , vitu vingine ni kuchekesha tu.
Attacking ya arsenal ipo hivi gyokeres 0 non penalty goals in last 11 appearances, saka 0 goals in last 13 appearances , martinelli 0 goals in last 13 appearances, madueke huyu ndo kabisa hana goal la epl, trossard 1 goals in last 11 appearances in all comps.

Nan anafunga magoli ya arsenal? Ni mchezaji gani arsenal ikiwa imezidiwa itamtegemea kwenye kufunga magoli au kuonyesha individual brilliance kama alionyesha salah, halland ,KDB , mahrez, vard, rooney, drogba na hazard .
Bukayo saka ndio captain si masihara haya wazee😆😆, arsenal ni kituko kuanzia team, wachezaji, kocha mpaka mashabiki.
 
Habari za asubuhi wajalana.

Kama ilivyo ada kukumbushana mara kwa mara

Msimu wa 25/26

FALSE HOPE FOOTBALL CLUB

1. Carabao cup: FALSE HOPE🔞
2:EPL loading: FALSE HOPE🔞
3: UEFA loading: FALSE HOPE🔞
4: FA Cup : FALSE HOPE🔞
 
WC players waliopo Hapo ni kwenu ni

Raya
Saliba
Rice

Sio Ode, saka, Victor wala martineli..hizo ni takataka!' Alafu mnataka ubingwa ? Ngoja Pep awapelekee moto vizuri ....
 
Alafu kuna kiazi kipo ndukweta huko kitakuambia Arteta ni miongoni mwa makocha bora duniani....
Ukikiuliza hicho kiazi Arteta ameshinda nn kumfanya kuwa miongoni mwa makocha bora the likes of Carlo, Pep, Fergie, Mou, Conte hakina majibu ....

Msimu wa ngapi mko kwenye phase ? Board imemsapoti sana sana kusajili wachezaji anaowahitaji

Fungu la kukosa , Shenzi kabisa !
 
Kwa miaka almost minne tulikua tunasema ubingwa unahitaji bahati pia kwakua unaweza ukajiandaa unavyoweza ila bahati ikiwa haipo upande wako wewe hautoboi.

Sasa Arsenal analaumiwa kwamba akishinda atakua anaonea wenzake kwakua ni wabovu. Liver hua inataniwa ilichukua kombe la COVID-19 na msimu uliopita ikasemwa wamebeba kombe kwakua immediate opponents were shit.

But who gives a fvck? Ndiyo wameshashinda tayari. Bahati itakuja kivyovyote na kama kwetu imekuja kwa mtindo huu tena imekua bahati ya mpaka CL, FA na EFL basi sawa wakina Scholes ongeeni tu.
 
Hata wiki tatu hazijaisha vizuri tangu watu waanze kupoint kwamba Doku ni unstoppable, Foden hashikiki.

Leo tupo wapi? Bernado Silva? Savinho? Katik kila timu unaweza kupata orodha ya wachezaji ambao kwao kuscore imekua changamoto.

Isipokua inategemea muda huo agenda imeegamia kwa nani.

Niliku naangalia mashabiki wanalalamika kwanini Nwaneri ameenda Marseille kwa mkopo. Wanasahau Saliba pia alitolewa kwa mkopo misimu miwili mfululizo. By that time hoja ilikua kama Fofana (huyu aliyepo Chelsea) walicheza wote na wote wameletwa Uingereza na Leicester inamtumia Fofana kwanini sisi hadi tumtoe Saliba kwa mkopo? Na Saliba alikua kapteni wa Fofana.

Majibu tunayo mpaka saa hii.

Now ni sahihi kuhofia kwakua siyo kila mkopo utarudi na matunda yanayotarajiwa. Vieira, Mari, Marquinhos, Tavares, Denis hawa hawakudevelop zaidi. Lakini Nwaneri ana shida ya kutrack back same problem kwa Eze, sasa Nwaneri ni academy so kumtoa kwa mkopo ni rahisi.

How about Eze? Utamtoa kwa mkopo akajifunze kutrack back? No, atakomaa hapo hapo msimu wote kisha umuone msimu ujao. City walifanya hivyo kwa Grealish, if all turns to shit ama ni hivyo au kumuuza.
 

Captain wetu nasikia kwenye mechi 20 consecutively za Arsenal ana goli moja ?

Huyu ndio tuliambiwa ni best AM Epl? Mnaumwa, na kocha kamuelewa kila mechi panga pangua !

Huyu zaidi ya back na sideways passes hana kingine ..... hawez ku_unlock parten .. (kiswahili tunaita pasi za upendo, pasi mpapaso ... pasi jicho ] huyu angekuwa hata na robo IQ ya mesut Ozil mnengukuwa mbali sana
 
Hata kwa Magnifico maestro Bruno hanusi yule dogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…