Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Chelsea kushika nafasi ya pili (kwa muda) wanajiona nao ni team bora ee
 
😂😂😂
Wakati Caicedo amehojiwa Leo kuelekea mechi na Arsenal akaulizwa na daily Mail kwanini aliichagua Chelsea na si Arsenal alivyokuwa anawaniwa vilabu vyote viwili
Caicedo: Niliamua kusubiri offer ya Chelsea japo Arsenal walikuwa wa Kwanza kuonesha wananihitaji sababu iliyomfanya niichague Chelsea kwasababu Wana big ambitious na kuchukua makombe hiyo ilinivutia kujiunga nao
 
Hii ni AI, angalia nembo ya gemini chini kulia
 
Hamna kitu, Arsenal walikuwa washamchukua Rice mwezi mmoja kabla. Kwanza mlimaliza wa 12 kabla ya dirisha hilo. Sijui hiyo ambition aliiona wapi
 
Hamna kitu, Arsenal walikuwa washamchukua Rice mwezi mmoja kabla. Kwanza mlimaliza wa 12 kabla ya dirisha hilo. Sijui hiyo ambition aliiona wapi
Mkuu nenda kafatilie vizuri mlitoa pound 70m Brighton wakakataa, sio tu Caicedo huo msimu tulimleta pia Enzo Fernandez ni kweli hatukuwa kwenye nafasi nzuri kwenye ligi but history ya kuwin Mataji ndio ilikuwa inatubeba Hadi Sasa na project yetu inauzika kwa wachezaji
 
Hamna kitu, Arsenal walikuwa washamchukua Rice mwezi mmoja kabla. Kwanza mlimaliza wa 12 kabla ya dirisha hilo. Sijui hiyo ambition aliiona wapi
Sasa kwani kumaliza nafasi ya 12 ndo nini mkuu au umesahau tulishawahi kumaliza nafasi ya 10 akajaga conte tukachukua kombe la epl msimu uliofuata hyo ndo maana halisi ya ambition
 
HApa kuna kitu cha uongo umeandika. Caicedo alisema 'I was dying to join Arsenal' au 'I nearly get sick waiting for Arsenal' akiamini Arsenal ingepeleka ofa.

Arsenal haijawahi kupeleka ofa kwaajili ya Caicedo. Mlikua mnashindana na Liverpool.

Mnapata faida gani kuandika uongo nyinyi watu?
 
History ya kuwin mataji? Ile mikataba ya miaka 7 inayosababisha wakina Mudryk wasitake hata kukata rufaa unadhani ni jambo dogo?

Cut the crap bruv
 
Yaani unaweza kumchukua Zubimendi au Caicedo halafu unamchukua Caicedo? Kwa namna mpira wa Arsenal ulivyo Zubimendi ni enforcer mzuri kuliko Caicedo.

Mimi nimeanza kumuona Caicedo kipindi hicho anacheza LM, kabla ya Brighton, wakati huo sisi tuna wakina Guendouz. Na kipindi kile niliamini anatufaa kwakua Caicedo ana akili ya kwenda mbele kushambulia.

Kwa sasa tuassume yupo sehemu nzuri. He is happy, we are happy. Everyone wins
 
Sasa kwani kumaliza nafasi ya 12 ndo nini mkuu au umesahau tulishawahi kumaliza nafasi ya 10 akajaga conte tukachukua kombe la epl msimu uliofuata hyo ndo maana halisi ya ambition
Kipindi hicho cha kina Leicester ni sawa ila sahivi hakuna miujiza ya namna hiyo
 
Nyumbu wanakutana na timu ambayo imefungwa magoli machache msimu huu ikiifuatia Arsenal. Hii ni ya kuitazama
 
Walikuwa wanamtaka Caicedo walikuwa watatu Arsenal, Chelsea na Liverpool. Arsenal ilikuwa ndio team ya Kwanza kutoa offer na walitoa paund 70m Brighton wakakataa ndipo Liverpool ikaingia na sisi ndio tukafata mkuu ebu kuwa na kumbukumbu vizuri
 
History ya kuwin mataji? Ile mikataba ya miaka 7 inayosababisha wakina Mudryk wasitake hata kukata rufaa unadhani ni jambo dogo?

Cut the crap bruv
Tangu kuanzia miaka 2000 mpaka Sasa hajawahi kupita misimu miwili bila kuwin trophy. Mechi ya Leo nakuomba aanza kuangalia game mwanzoni kabisa kabla mpira hujaanza huone atmosphere ya Stanford bridge najua mashabiki watawadhiaki vibaya mno mabango yatakuwa Kama yote
 
Arsenal katika Dirisha dogo la January 2023 walikutana na Kambi ya caicedo pamoja na caicedo mwenyewe na kumalizana nao kila kitu kuhusu personal term's

Bahati mbaya Brighton wakajua na hawakupendezewa na tabia ya Arsenal kukutana na mchezaji wao, Arsenal wakapeleka dau la kwanza £60 Brighton wakapiga chini, Arsenal wakarudi tena na £70 pia Brighton ikapiga chini hiyo Offa na kusema Rasmi kuwa Caicedo hauzwi na ikawapa onyo Arsenal wakiendelea na huo mchezo hawatafanya tena biashara nao,

Dogo akagoma kuingia kambini na kufanya mazoezi akishinikiza kuuzwa Arsenal, Brighton ikamsimamisha kwa makosa ya Nidhamu hadi 1 February ndio akarudi Tena kuitumikia club yake, mwezi wa 3 akasaini mkataba mpya wenye release clause ya £100

Lilipoingia dirisha kubwa la usajiri July Chelsea na Liverpool ndio wakawa wanamtaka, Arsenal hawakurudi tena kumtaka kwa kuogopa kuharibu mahusiano yao na Brighton lakini muda huo wakiwa washaandaa mazingira ya kumpata Rice

Arsenal July 15 wakamsaini ramsi Decline Mchele na 14 August Chelesea ikamsaini Caicedo, kwahiyo story yako ni either unaipindisha makusudi au hukuelewa uhalisia ulivokuwa
 
Walikuwa wanamtaka Caicedo walikuwa watatu Arsenal, Chelsea na Liverpool. Arsenal ilikuwa ndio team ya Kwanza kutoa offer na walitoa paund 70m Brighton wakakataa ndipo Liverpool ikaingia na sisi ndio tukafata mkuu ebu kuwa na kumbukumbu vizuri
Wewe unachanganya nyakati, wakati Arsenal wanamtaka Caicedo ilikuwa ni Dirisha dogo ndio wakatuma offa mara mbili Brighton wakagoma na kusema hawamuuzi

ilipofika dirisha kubwa vita ikawa ni Chelsea na Liverpool, wakati huo Arsenal yeye anachuana na Man City katika kupata Saini ya Decline Rice

Kwahiyo kama Brighton asingeweka Ngumu, Caicedo angeenda Arsenal since January
 
Caicedo ana quality zote za kwenda mbele kurudi nyuma, kutoa pass na kufunga pia ulivyokuwa unamuona Kante ndio the same na Caicedo ila kwa Maresca anamtumia chini ni kwasababu tuna Enzo Fernandez ambaye ndio ambaye anafanya Hilo jukumu kwasababu kwenye no 6 tuna upungufu Essugo ni injury, Lavia injury, na beki zilikuwa Zinashake ndio maana akaona Caicedo akae chini ili asaidie mabeki na eneo la katikati zaidi. Ila kuanzia mechi zinazofuata utamuona huyo Caicedo insyomuhitaji kwasababu Essugo kapona, Santos yupo on fire Baada kuanzia kumchezesha 6 hii inatoa uhuru kwa Caicedo kwenda mbele hata pia anapocheza na James Kati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…