Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Dah!, wanangu nikiangalia nyie muna Saliba halafu nikigeukia kule kwetu tuna Ibu Konate naumia sana. tugawieni hata Mosquera
Unaishiwa PAWA kabisa sio😀😀😀....nilivyoangalia mechi yenu jana nikawa nasema hiiiiiii😀😀😀....j2 tunakuja shehe....mkicheza kama jana mmekwisha ndugu zangu....
 
Piero Hincapie,matajari wa arsenal safari mbona siwaelewi kabisaaa chuma kipya hicho
Itakuwa wameona jinsi C115Y na sasa Livakuku wanavyomwaga mpunga bila madhara yoyote wakaona nao wasiachwe nyuma. Huyu akija naona atamwuweka bench Calafiori pale LB. Nimesoma mahali kuwa tunataka kumchukua kwa 'loan with obligation to buy' kwanza ili tukwepe adhabu za PSR. Litakuwa kama dili la Raya.
 
Weekend hii mobutu seseko, atafunga kwenye game vs Burnley
Ila matokeo yatakuwa tofauti sasa....Burnley 3 vs Sesko 1😀😀....hawa jamaa imeniingia huruma kwlikwli kuwaonea.....nilikuwa naangalia highlights za mechi ya Burnley juzi na Sunderland...kiukweli Manunu wajiandae....wale wajinga wanakuja kama nyuki yaani
 
View attachment 3454693

Hatuko vibaya sana. Tuko vizuri tu on paper. Ila wenzangu akina Flano na akina Mkohoti sasa...
Hizo ni takwimu za kujifariji za kwenye makaratasi, hazina tofauti yoyote na zile takwimu za biashara ya matikiti maji.
Ukitaka kujua kua mambo ni magumu ingia sokoni sasa uone, utashangaa Ødegaard hauziki zaidi ya £20m, Saka £25m Saliba £35m hapo ndio unajikuta unaishiwa power.
Kwa Brighton kidogo biashara yao inaonekana ina uhalisia maana tayari wameshafanya vizuri sokoni na bado bidhaa zao zina uhitaji mkubwa mpaka dakika hii, ila Arsenyau tokea kuumbwa sidhani kama wameshawahi kuuza mchezaji kwa zaidi ya £50m.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…