Arsenal (The Gunners) | Special Thread

False hopers mpo , season hii vipi ?? hii ndo phase ya makombe Au tusubiri nyingine?
Amsha amsha hamna kabisa wengine ndo kabisa wamekimbia jukwaa hili wapo kwenye jukwaa la dini 😅.
Naona usajili umefanyika haswa mnashindwa nini kutoa hela kwa eze pale atleast atawasaidia maana Kwenye swala la creativity naona mwanenu Odergard hawez kupiga pasi za mwisho zikamfikia baunsa gyokeres .

Msimu naona mapema sana mtashikana mashati si Castr si Henry sio mkorea na transfer mlianza kuongelea wakati wenzenu wanasherekea ubingwa
 
Kenge na nyumbu kwaio mmeona humu ndio sehemu ya kufanya mazungumzo yenu?

Sasa Nyumbu ntakupiga 3+ hili jukwaa utaliona kituo cha polisi
Kenge dawa yako ipo jikoni, mshukuru mpo mbali kwenye ratiba ya kukutana na sisi
View attachment 3441322
Ntaamini tunachukua PL pale tu tutapopata replacement ya huyu odegaard tunahitaji more aggressive AM na a real team leader…lakinj sioni hiko kitu kwake he is more a second option to me
 
Mambo vipi mkuu, siku hizi naona unapotea sana humu jukwaani.
Wewe ndio mfariji wao usipoonekana humu vijana wanakua wanyonge sana.
Habari mbaya ya kusikitisha ni tokea usajili wa Madueke ndugu yetu Castr amesusa na kulikimbia hili jukwaa.
 
😂😂😂 castr katupa taulo kaingia mitini nilikua napitiapitia nikaona , nimeumia sana sana.
Sababu za kuingia mitini eti kisa madueke winga hatari kabisa mwenye world club medal ametua pale emirates , jamaa amechoka false hopes anamuangushia madueke lawama. False hopes fc pale wamekuja kina squilaci, lukonga na Marquinhos hajaondoka leo madueke kaingia na yeye kaingia mitini😂😂
 
Sema tokea msimu ulioisha walipofanya sajili za Kai Harvez na Rahim Sterling Castr alikua anajikaza tu kushabikia hiki kikundi cha baikoko, zile false hope za msimu huu huenda tunachukua ndio zilimfanya walau aendelee kubaki akijipa matumaini, ila baada ya kuona sajili za msimu huu pia ni zilezile reject za Chelkenge kina Kepa Arrizabalaga na Noni Madueke mwamba akajikatia tamaa mazima na kuamua kutupa taulo chini.
 
Nimejiandaa kukata rufaa castr arudi humu , sijakubaliana na sababu zake zisizo na mashiko za kuingia mitini msako utafanyika pori kwa pori thread kwa thread kumpata false hoper huyu.

Naona yule mwingine hamis amefuata ushauri wako kaamua kufungua kanisa yupo kwenye thread za dini na israel , Naomba kanisa likiwa kubwa akuweke kama mhasibu maana ushauri ulitoka kwako.
 
Masingeli sasa hivi ni next level, yuko deep sana katika kuusoma na kuuchimba uislam ili apate points za kukusanyia sadaka pale asimamapo madhabahuni.
Nakuhakikishia hamis77 baada ya miaka yake miwili tu ya utumishi anaingia kwenye list ya mabilionea wakubwa hapa nchini, kwa sasa mwamba anatumia nguvu zake zote kuhakikisha anaagana na umasikini.
 
Wewe kule kwenu vipi? Kila mnaeyemtaka anawatolea nje na Isak ndiyo huyo nae ameamua kwenda Liverpool angalau achezee timu kubwa kabla ya kustaafu soka.

Sisi tuko vizuri tu, japo tunazingua kinoma. Eti hatutaki kulipa hela ya Eze na tunajipa moyo kuwa eti tuna Nwaneri. Madueke kamkimbiza Castr siyo tu jukwaani hapa, bali kwenye ushabiki wa mpira kwa ujumla kabisa. Sijawahi kuona uamuzi mbovu kama huu lakini najua, muda si mrefu, Madueke huyo huyo atamrudisha mwamba jukwaani.

Ila nyie kikundi cha vurugu mijusi milia sijui msimu huu mtakuwa na hali gani. Natabiri vilio na kusaga meno tu kwenu.
 
Ila mwanangu Henry wewe una imani sana, kwa imani yako hio jinsi ilivyo madhubuti nakuhakikishia tunaweza kukupa jiwe ukaligeuza kua mkate.
 
Jitu la futi 6.5 likiwa kwenye mazoezi ya set pcs kwa ajili ya mechi ya jumapili.
 
Hii siyo kuhusu uzuri au ubaya wa Madueke tushakua na wachezaji wabovu kuliko Madueke. Mustafi, Jenkinson et el.

Chelsea ni rival, na katika kuhakikisha anadhoofisha wapinzani wa karibu Chelsea amewahi kupora wachezaji kwa timu mbalimbali. Recent example kwa sisi ni alivyoteka deal la Mudryk. Chelsea went the lengths hadi kudhamini silaha ili kuhakikisha Mudryk haji Arsenal.

Fast forward mwaka mbele, Chelsea ina rundo la wachezaji na anapambana kuwapunguza. In less than 48 hours unapeleka ofa ya 55M kwa rival halafu unachukua na kipa, bailing them out of the mess which they happily got themselves into.

Am aware kwamba inawezekana kabisa Chelsea hajalipwa hii pesa kwa mara moja. Lakini how stupid are we? Why the *** would you bail them out every time? Watu wanadai Chelsea anamuuzia Arsenal rejects, kwa Madueke hapana. He is not that bad ila bending over kwa timu ambayo haijiulizi mara mbili kukumess up ni weakness.

Do it kwa Brentford, it's fine. They agreed to lose their important keeper with cheap arrangements na wanakupa kapteni wao.
 
Mambo vipi mkuu, good to see you around. Naiman mitikasi zinaenda poa pande hizo

Nakumbuka ulisema utapunguza kufatilia soka na sio kuacha kabisa
Jukwaa letu la arsenal kwasasa linakuhitaji zaidi ya kipindi chochote kile mzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…