Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Yani tunaongeza Magalactico tu, now Saliba, Saka, Rice, Zubi hii ni special kwa zile UCL nights against Real Madrid
 
Broo ukiwa unaongea nao asikae nao karibukaribu, sasa hivi wanatembea na visu mifukoni, tahadhari ni muhimu sana kipindi hiki.
Jana kuna mmoja alikua anaongea mwenyewe barabarani halafu kabeba mabetri, kila akipishana na gari anarusha betri kwenye kioo cha mbele, amewatia hasara watu wengi kabla ya kudhitiwa na kupelekwa kituoni.
 
Fainali ya Manyumbu na Tottenham iko hovyo kwetu. Yeyote atayeshinda, tutajaziwa nzi humu.

Kwa Arsenal, nadhani mashabiki, haswa wa England, wataona ni bora washinde Manyumbu maana kelele zao tumezizoea, wao vyura sisi tembo. Ila Tottenham wakipata kombe, jeuri yao haitakuwa ya dunia hii.
 
Na nyie si mtawaringishia zubimendi mkuu.

Ila arsenal bwana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Tukimalizana vizuri, naona huyu ni mbadala Jorginho. Hatutanunua DM hata Partey akiondoka maana Arteta atamfanya Lewis-Skelly kuwa mbadala wa Partey.

Sasa tupate mbadala wa Odegaard na Trossard, Saka na Martinelli. Pia striker mmoja kumsaidia Kai maana nadhani Jesus hatacheza tena mpira. Then tumalize na kipa.
 
Hao wote wanajuta sahizi ni vile hawasemi, wote wamepishana na medali.

Hivi huwa mnaamini kabisa, mchezaji kaikataa madrid, bayern, city, liva au chelsea aje Arsenal?? kweli kabisa mnaamini???

Tuseme wewe sasa ndio mchezaji unaweza kufanya huo upuuzi?
 
Bila ya kutafuta kocha wa kueleweka na kuendelea kumuamini Tetea Kiwigi hata mkimsajili Pedri, Yamal, De jong, Bellingham, Vitinha, Kvara na Mbappe mtaendelea kua wapenzi wasindikizaji tu.
 
Masta huwaga una hoja nzuri sana za kimpira ukitoa "UNAZI" Yani unawadhihaki Timerlane na Joh Doe katika hili!!

Hakuna PROJECT Ya mpira inayozidi miaka 3. ARTETA Sasa anaenda miaka 7 kombe 1 na ametumia karibu 800m, Sajili zaidi ya 30 kwa kombe 1?? bado huamini kwamba ni Ishu pia Inahusiana na 'Mentality" zaidI
ARSENAL haina tatizo la kimbinu wala Ubora, Timu kubwa zimekosa matokeo kwake muda tu, Unadhani kwa nini timu haichukui makombe. (Game kubwa mentality yao inabadilika )

Sporting CP wameitoa ARS Europa, Bayern mbovu imekutoa UCL, PSG (Ilobadilika Mentality) Imekutoa UCL.
Ukitaka jua thamani ya MENTALITY katika mpira itizame Fainali ya mwaka huu, Inter na PSG ni timu ambazo umekutana nazo zote na ukaonyesha ubora, ila wao wamefika hatua wanataka zaidi kukushinda.

Shida kubwa ya Arsenal ni 'CHARACTERS' hakuna watu kama Keane, Vieira, Rodri, Wazza, Drogba, et al.

RICE Mnamsifia baada ya FK zake na Madrid, ila ni huyu huyu anafunga goli la kusawazisha na UTD anakimbilia kunyamazisha mashabiki (Wenzake wanaotaka ushindi huwa wanabeba mpira kurudi kati chap kutafta Ushindi)
Unaisingizia CITY ya treble kuwa bora, haikuwa namna hiyo maana hata fainali ya Inter ni ubovu wa kina Lukaku zaidi ya Ubora wa mpinzani, Fainali yake na FA ni De gea aliwazawadia magoli ya Gundogan. (City bora ilikuwa ya msimu kabla ila MENTALITY yao ilikuwa ya kutaka zaidi)

Granit Xhaka kuondoka kwake ni makosa makubwa sana. Hakuna mwenye kuonyesha Kutaka Ushindi zaidi mnapiga pasi hata maeneo ya ku-shoot!!
 
Hapa mkorea anakwambia hesabu zake bado zipo valid, Liverpool watamkamata February, halafu kati ya Uefa au Epl kombe moja lazima wanaruka nalo.

Uzuri ukifika muda wa kukabidhiwa chenji zao wote wanalikimbia jukwaa lao.
Yaani kabisa uchukue Uefa au Epl kocha ni Tetea Kiwigi?
Hivi wakati mnajigea hayo makombe mnakuaga mpo sawa au tuilaumu gambe?
 
Huyo ni mnazi wa hamis77
(kakimbilia kwenye utumishi na kujifanya anachambua holy books)
 
Huyo ni mnazi wa hamis77
(kakimbilia kwenye utumishi na kujifanya anachambua holy books)
Kuna yule chawa mwingine arsenal2004 huyo ndio kasusa kabisa kuingia humu hataki tena kusikia habari za mipira, tokea Masingeli alivyowaahidi msimu ulioisha watabeba treble halafu wakatoka mikono mitupu jamaa alitia kiberiti jezi zake zote, halafu akaenda zake kwa Mwamposa kupata wokovu, sasa hivi muda mwingi anashinda zake kanisani tu, anakwambia hii mipira ni ubatili mtupu, anadai mpira ni mpango wa Lucifer kupambana na wokovu.
 
Sema fuentte unawajua vizuri mashabiki wa Shenali utafikiri wewe ndio baba yao mzazi.
Ila alichokifanya Pep kuwauzia Tetea Kiwigi ilikua ni daylight robbery, halafu mpaka kesho ukimsikiliza Pep jinsi anayomsifia Tetea kinafki unaweza ukacheka mpaka ukaharibu bandama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…