Arsenal (The Gunners) | Special Thread

🤣🤣🤣


Kwenye sala zao waombe sana tukose Kombe la Europa league

Otherwise watatuambia msimu huu walikuwa wanafanya nini sasa🤣🤣🤣
 
Naelewa unachozungumza ndugu, pia hata mimi nimfuatiliaji wa soka la wanawake.

kwa msingi wa hoja yako, kumbuka hata sisi tumetoka kumfunga Lyon tena nyumbani kwake ambaye hajapoteza mechi hata moja tangu msimu unaanza, na huyo Lyon amekuwa ni mbabe wa barcelona miaka nenda miaka rudi, ni mwaka jana pekee tu ndio barcelona alimfunga Lyon, sasa kama tumeweza kumnyanyasa Lyon tena kwa kichapo heavy, basi tunaweza kumfunga na huyo barcelona kwenye hiyo fainali, na hasa ukizingatia hakuna kombe lingine tunalotarajia zaidi ya WCL makombe ya ndani yote chelsea amejimilikisha.
 
Arsenal yaenda shimoni
Baada ya kuona Liverpool ananyanyua kwapa tena ndani ya miaka michache tu
Huku arsenali akiwa mshindwa sugu, Mwaka wa 20
No epl

Kaenda kutafuta faraja kwenye soka la akina Dada ambalo hata sisi akina dada hatuna mzuka nalo.
Hujui tu, Arsenal Women wanacheza soka safi na la kuvutia kuliko hata liverpool ya akina Mo salah.

Karibu jumatano wanacheza na Aston villa ujionee burudani, na sio mpira wa kuchoshana kama ule uliozoea kuuona pale anfield ambapo akina Luis Diaz muda wote ni kukimbia tu, na kuna muda wanakimbia mpaka wanasahau mpira.
 
Ni aibu kubwa wanaume ligi imewashinda mnabadilisha gia hewani kujidai ni mashabiki wa ligi ya kina Mama😂
Wewe unawivu tu kwa sababu wanawake wenu si lolote si chochote kwenye boli huku wakwetu ndiyo vinara. Hapa najua wote mnaomba Barcelona watuchape ili mpate la kusema.
 
Sisi tunashabikia mechi za wanaume wa shoka
Nyie ligi ya akina Mama, mmemkacha Aterta
Basi badilisheni kabisa thread
Iwe arsenal queens😂
 
YOur fellow fools opted out hawajasema kitu
Inasikitisha sisi ndio tunawaona nyie wehu kumbe nyie hamjitambui ndio fools, kuwa shabik wa Arsenal lazima kuna fuse zinakua zimepga shoti mahala.

Hapo na msimu huu mtatoka patupu, mtakuja kumsifia Arteta kuwa mmetolewa kwnye hatua nzuri, hizo ni akili??
 
Sasa unaniulizaje lakini? Ok, assuming akili huna mi ntafanyaje sasa?
 
Sisi tunashabikia mechi za wanaume wa shoka
Nyie ligi ya akina Mama, mmemkacha Aterta
Basi badilisheni kabisa thread
Iwe arsenal queens😂
Mbona makasiriko mama, sis huku timu zetu zote mbili zinaelekea kwenye climax ya kutupa furaha kubwa sana kiasi kwamba vilabu vingine vyote vitatuonea wivu.

Vuta picha hilo parade lake litakavyokuwa baada ya timu zote mbili kutawazwa wafalme wapya wa ulaya.... vibe lake ni zaidi ya hicho kiEPL mlichochukua kwa msaada wa PGMOL

Nyie timu yenu ya wanawake(liverpool women) haijawahi hata kushiriki WCL na ndio maana huna habari nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…