Andrea Berta, aliyekuwa Sporting Director wa Atletico Madrid, anakaribia kujiunga na Arsenal kama Sporting Director wetu, akichukua nafasi iliyoachwa na Edu.
Nadhani wengi wetu hatujui masuala ya masporting director ila tuliuona umuhimu na mchango wa Edu katika kuturudisha top 4 na kupambania ubingwa. Naweza kusema kuwa nadhani msimu huu tumekutana na majanga ya majeruhi, dhulma, kupoteza form na bahati mbaya nyingi zilizoyumbisha msako wetu wa msimu, ila kumpoteza Edu November mwaka jana nalo ni pigo moja wapo kwetu msimu huu.
Je, mnadhani Berta, kutoka timu iliyofanikiwa Spain akiwa nao, atatusaidia kupiga hatua mbele ya tulipofikia hapa sasa?