Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nimeingia JF ili tu kukushitua umuone mwanetu jesus, huwezi mfananisha na kiazi kai.
Kama anaaminiwa kama msimu wakr wa kwanza ule, jesus bado ni msaada, shida yake ni pancha tu, tofauti ya hilo ni bonge la mchezaji.
Pancha ndiyo changamoto kubwa ila no mchezaji wa level ya juu kwa Kai
 
Second half ilikua very promising.

In 10 seconds Dean akakutana na shots 4 zote zinahitaji majibu.

Hawa watu wazima wanawafundisha vibaya vijana, unaona Nwaneri idea yake ni kusogea mbele na mpira anaupata anaitoa anatangulia mbele aletewe mtu anapiga back pass.

Tierney was superb pamoja na kua nje kwa muda mrefu ila alikua very solid, anafanya overlap za maana isipokua alikua hagewi mipira. Jamaa ni mzuri sana kwenye krosi sidhani kama tuna LB anayemzidi kwenye accuracy ya long balls.

Dhidi ya Sporting Kiwior alishindwa mbio na ubavu na Gyokeres ambaye kacheza dakika zote huku yeye akiwa mpya hana dakika mbili na Gyokeres akagongesha mwamba. Mateta akampa same treatment na akascore. Pace na upande vyote vilevile Kiwior akashindwa kumpa majibu Gyokeres siku ile na Mateta jana.

Nafikiri physically itakua ni challenging kwa Kiwior akikutana na STs ambao wana pace na nguvu. Aimprove huko

Tumejitahidi ila inabidi kusajili January
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…